Ujumbe kwa NIDA na Mitandao ya Simu, Kilio cha wananchi

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
Tumepiga marufuku mifuko ya rambo kwa yowe na maneno matam na sasa tunapiga marufuku utumiaji wa laini za simu kwa watu wengi kimya kimya na kwa utaalam mbovu, utadhani na hili ni new world oder (Maneno ya walevi tuyapuuze jamani, akili zao zinakimbia wakilewa zinarudi wakiwa wazima).

Turudi kwenye mstari, tusitoane relini kama wachaga na treni mpya.

Zoezi maarufu kwa sasa katika kila kona ni usaliji wa laini za simu kwa alama za vidole. Bado masaa kadhaa tu wasiosajili kwa mfumo huu-line zao zinaaga dunia. Hasara kwa watumiaji na hasara kwa mitandao ya simu.

Naomba niwalaumu NIDA kwa machache na mutanisamehe kwa hili kwakua haya wanayasema wananchi. Nida imefanya zoezi la usajili wa alama za vidole kwa mda sasa. Lengo kuu ilikua ni kupata vitambulisho vya taifa na baadae suala la ulazima wa kusajili line za simi UPYA Kwa alama za vidole ukisaidiwa na number ya NIDA. Nakazia UPYA kwasababu mwanzo,zoezi la usajili wa Line za simu ulikua kwa vitambulisho vya kawaida na watanzania wengi walifanikisha hili kwakua halikua na ukomo.

Zoezi la usajili wa alama za vidole ni la ukomo na ni la muda mfupi. Kitu gani munaharaka hadi mufungie line za watanzania?... Ingekua bila kusajili kuna hatari inaweza tokea nadhani hata mimi ningewasaidia kuswitch hizo line zisituletee balaa.

Nida imesajili watu, vitambulisho havipatikani
Number ili wananchi waweze kusajili line zao hazipatikani kirahisi pia.
Kabla maamuzi yoyote kufanyika ni lazma vikao vifanyike. Usajili wa Line za simu nna hakika ulihusisha ofisi za Nida /TCRA pamoja na makampuni ya mitandao ya simu.
1. Katika kikao chenu hiki hamkupanga muda mzuri wa kusajili na kumaliza zoezi hili?

2. Hamkupeana njia za kurahisisha zoezi la usajili?

3. kwanini number ya Nida lazima niipate kwenye ofisi za nida ndipo nikasajili line yangu?...

4. Mitandao ya simu, mulishindwa kuomba access ya upataji wa number za vitambulisho ili musajili line za wateja wenu kwa urahisi?

Baadhi ya stationary zinatafutia wateja wao number za vitambulisho na copy za vitambulisho vyao uraia, MITANDAO ya simu imekuja kushtuka wakati giza limeshatanda

Matukio ya hadhara ya kuwakutanisha ma officer wa NIDA na mitandao ya simu yangefanikisha kwa asilimia kubwa zoez hili la usajili. Nimeshuhudia moja likifanywa katikati ya jiji kwa siku kadhaa, sehem ambayo wananchi wake wengi wanaweza kuhangaika japo kwa muda mfupi kupata number na kusajili line zao.
Kwanini zoezi hili lisingekua pana na kufanikisha kwa kila kata?
Tamko la mwenye mamlaka linanguvu kuliko anae miliki leo mimi ndiye ninae miliki laini lakini yupo mwenye mamlaka na hizo laini nae ndiye mwenye mamlaka na vile vitambulisho vya kusajilia laini yangu yeye ndiye aliye sema tuwe na hivyo vitambulisho pia yeye ndiye aliyesema tusajili laini zetu kwakutumia hivyo vitambulisho mimi naamini huyu mwenye mamlaka anatambua changamoto zilizopo huko kwenye kukipata hicho kitambulisho pia anatambua changamoto zitakazo patikana baada ya kuzifunga hizo laini

najiuliza tu niwatu wangapi watakosa kutumia simu na makampuni ya simu yatapoteza mapato kiasi gani na serikali nayo itakosa kodi kiasigani kwa hicho kipindi wat u watakapo kosa mawasiliano?

ninacho amini mimi upatikanaji wa hicho kitambulisho ungekuwa ni waharaka kama kitambulisho cha mpiga kura leo hii wahanga wakufungwa laini zao wangekuwa ni wachache sana.Msione aibu
waombeni msahama watanzania kwa kuwapa msongo wa mawazo, ongezeni muda wa zoezi. Marekebisho na kufikia hatma nzuri ni kusikiliza maoni ya wadau na wananchi. Huwez fanikiwa ukisimama na mawazo ya pekeako😊
 
Back
Top Bottom