Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Inategemea Unataka maana katika muktadha upi.. Faith inaweza kuwa Multidimensional
Tujadili hizo Posho CHADEMA tulizopiga tuache kujadili Maneno hatupo Kwenye kipindi cha Kiswahili
 
Kuna thread nyingine ukizisoma unajihisi kama upo ulimwengu wa kale! Enzi ambazo fikra za binadamu na za kima na nguruwe zilifanana!! Ukizinduka ndiyo unagundua kuwa unaishi kwenye ulimwengu mpya,wenye watu walio na fikra na mitazamo tofauti.
 
Lema kapwaya sana arusha na anatuangusha chadema bora arudi TLP akaungane na Mrema kudili na wafungwa!!! Chyaa...mbunge hana programu yoyote ya maendelea zaidi ya madongo na maandamano!!! Asee Lema, pita ivi chalangu!
Well said Chalii angu... Inabidi aamke arifu....
 
Wala ww siyo cdm ni ccm ni sisi watu wa kaskazin hatututakaa tuichague ccm kamwe hata kama ccm itatawala hii nchi milele
Ni Mpenzi wa CDM. Sitaki tupoteze jimbo. Programmu za Mbunge na Baraza la Madiwani alieleweki. Gambo kawekwa hapa kimkakati
 
Kweli ndoto za mchana mbaya Sana.Kama Molabani alishindwa n mahela yake sembuse gambo.Tunaimani na Lema na tutamchagua tuu.Angeachiwa afanye kazi zake kwa uhuru Aruxha ingekuwa mbali zaidi ya hapa
 
Teeeeeeee nacheka kwa dharaaaaauuuuuuuuuuu yaania hapo ni sawa na kumwambia mh Lema asijisumbue na kufanya kampeini maana hata akiwa nyimbani kwake tu tayari ni mbunge kwa kura kibao
 
Gambo aendelee kuota tu! Akiamka atashangaa nafasi yake RC anapewa mwingine na yeye ubunge ameukosa!!
 
Gambo akipata hata kura 1000 basi akachinje mbuzi kwa furaha
 
Kivipi,elezea kinagaubaga.
Hakuna Chama chenye hati miliki na Jimbo.

Lowassa ndio aliwaponza ccm kwa kumhujumu Mrema aliekuwa Mbunge na kummbeba Demu wake Batlda kuwa Mgombea

Wachaga wakachukia wakampa Lema kwa hasira japo alikuwa hapendwi maana hana siifa za kuwa Mbunge

Ccm bado wakajichanganya tena wakampa Monaban Maasai wakati wanajua Uchumi wa Arusha umeshikwa na Wachaga.

na hali ya mabadiliko ya kiasiasa yalivyokuwa basi Lema alikuwa hana namna lazima ashinde

ccm wakizinduka wakajipanga vizuri wakaja na Mgombea anaetokea Mgombani mweye akili na maarifa wale wanya viroba hawana namna .

Labda Lema abadilike sana japo siku hizi ameanza kubadilika kuanzia michango yake Bungeni nk.

huo ndio ukweli mchungu wewe Chariiii ya ARA
 
Kweli ndoto za mchana mbaya Sana.Kama Molabani alishindwa n mahela yake sembuse gambo.Tunaimani na Lema na tutamchagua tuu.Angeachiwa afanye kazi zake kwa uhuru Aruxha ingekuwa mbali zaidi ya hapa
Kutumia X badala ya S ni dalili Tosha kwamba haupo Smart. Monaban alikuwa anatumia pesa kushinda. Machalii wanakula tuu. Ila huyu mtumishi mzuri ni zaidi ya pesa. Wananchi wanapenda huduma
 
Wewe huwezi kuwa mwana cdm bali sema umeona ukisema kuwa ni mwana ccm uzi wako utadoda tu
 
Usimsingizie Mrisho Gambo hatagombea ubunge Arusha bali atagombea aibu Arusha.
 
Ccm dhaifu inaruhusu upinzani kumea Bali CCM imara haiwezi kuwafanya wapinzani waonekane.

Mh. Gambo anaweledi na anajua majukumu yake kwa kina na kwa sasa anachofanya kutimiza majukumu yake itapelekea chama mbadala kupoteza hoja za msingi hili litapelekea kupoteza jimbo.

Ameagiza waalimu wote walipwe stahiki zao na tayari baadhi wameshalipwa bado wengine uhakiki ulikua unaendelea Leo pale Arusha Sec. Kwa kweli akifanikiwa kuwatatulia wafsnyakszi Keri zao basi uimara Wa serikali ya CCM utarudi Mara moja na nguvuvya kisiasa iliyopotea itarudi.
Viva Mh.Magufuli ,Viva Mh.Gambo
 

Ahahaha umenichekesha sana kijana. Kwahiyo sisi ni wanywa viroba? Naomba unitajie jimbo lako tafadhali.
 
Wewe huwezi kuwa mwana cdm bali sema umeona ukisema kuwa ni mwana ccm uzi wako utadoda tu
Upinzani wa kukosoa tu hata penye ukweli ndio utatuangusha. Siasa ni Sayansi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…