Nashauri dereva wa Lissu apewe ulinzi

Nashauri dereva wa Lissu apewe ulinzi

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
947
Reaction score
690
Natanguliza pole nyingi sana kwa Mh. Lissu pamoja na familia yake kwa tukio baya la kijasusi lenye kuiabisha nchi yetu.

Pamoja na upelelezi unaoendelea, napenda kuishauri Polisi na pia chama cha CHADEMA kutoa ulinzi thabiti kwa dereva wa Mh. Lissu.

Kwenye tukio zima kilichotokea huyu ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kusema aina ya gari namba zake hata sura ya wahusika

Kwanza yeye kama dereva hakuwa katika hatari kubwa kama ilivyo kwa Lissu, alikuwa na muda mwingi hata wa kupiga picha au kusoma namba.

Maadui kwasasa watakuwa wanamwinda huyu dereva ili kupoteza ushahidi

Naomba jambo hili lipewe kipaumbele

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natanguiza pole nyingi sana kwa Mh Lisuu pamoja na familia yake kwa tukio baya la kijasusi lenye kuiabisha nchi yetu.

Pamoja na upelelezi unaoendelea,napenda Kuishauri polisi na pia chama cha cdm kutoa ulinzi thabiti kwa dereva wa Mh Lisu .

Kwenye tukio zima kilichotokea huyu ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kusema aina ya gari namba zake hata sura ya wahusika

Kwanza yeye kama dereva hakuwa ktk hatari kubwa kama ilivyo kwa Lisu,alikuwa na muda mwingi hata wa kupiga picha au kusoma namba nk

Maadui kwasasa watakuwa wanamwinda huyu dereva ili kupoteza ushahidi

Naomba jambo hili lipewe kipaumbele

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hata Lissu mwenyewe alitishiwa kuuawa, na humu JF kuna uzi na video iiliyomtishia maisha yake na muhusika ameonekana live lakini hakuna hatua iliyochuliwa, ndiyo maana watu wanahisi hii itakuwa ni pombe
 
Labda kwa kuwa walisema gari liliwafuatilia kwa muda anaweza kuwa ameona no yake
 
Tatizo namba inaweza kuwa ilionwa,,ila isionekane tena mpaka tukio lingine. Au fake
 
Mbona hata Lissu mwenyewe alitishiwa kuuawa, na humu JF kuna uzi na video iiliyomtishia maisha yake na muhusika ameonekana live lakini hakuna hatua iliyochuliwa, ndiyo maana watu wanahisi hii itakuwa ni pombe
Kuna ukweli ndani yake
 
Yan gari ulilomo ndani linapigwa risasi unawezaje kupiga picha?

Umekifkiria vizuri ulichokiandika?

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
Si ndio hapo jamani? Kwanza hata km alitoka salama nae ni jambo la kushukru sana.
 
Kwa milio ya risasi nina hakika dereva kilichomuokoa ni kufungua mlango na kukimbia
Lissu asingeweza kimbia
 
Mbona hata Lissu mwenyewe alitishiwa kuuawa, na humu JF kuna uzi na video iiliyomtishia maisha yake na muhusika ameonekana live lakini hakuna hatua iliyochuliwa, ndiyo maana watu wanahisi hii itakuwa ni pombe
Kweli pombe haijawahi mwacha mtu salama.inabidi ipigwe marufuku
 
Yan gari ulilomo ndani linapigwa risasi unawezaje kupiga picha?

Umekifkiria vizuri ulichokiandika?

Sent from my Iphone 7 using JamiiForums mobile app
Akili za watu wa Instagram ndugu yangu. Msamehe bure
 
Kwanza naomba kutoa pole kwa wote walioguswa na tukio la jana, lakini pia naomba kwa wale nitakaowakwaza kwa swali hili pia wanisamehe, naelewa kabisa hasira zao. Ila katika kutaka kuelewa tu. Hivi hali ya dereva ipoje kwa sasa? Je wakati gari inashambuliwa alikuwa ndani ya gari au alikuwa ameshuka? Na pia gari iliyowashambulia ilikuwa nyuma yao au ubavuni kwao? Au washambuliaji walishuka ndani ya gari? Pale gari inapoonekana kwenye picha ndio hapo ilishambuliwa au ilisogezwa mbele na je ni nani aliisogeza?
Kulikuwa na taarifa za mtu mmoja kuchukuliwa kwenye ofisi za CDM Morogoro jana usiku, je ni kweli kuwa sasa hivi CDM inafanya kazi saa 24? Au huyu mtu alikuwa anafanya nini ofisi muda huo?
 
Back
Top Bottom