Nasema: CCM acheni mbinu chafu hapa UDOM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasema: CCM acheni mbinu chafu hapa UDOM

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by only83, Apr 29, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ........Awali ya yote napenda kutoa pole kwa wanafunzi 27 wa chuo cha elimu ya kompyuta katika chuo kikuu cha Dodoma kwa kusimamishwa masomo ambako kwa hali inavyoelekea ni kufukuzwa kabisa..kwanini nasema pole,nasema pole kwasababu haya yote ni mbinu chafu za CCM kupunguza wasomi waliofunguka bongo..wanatamani wabakie na vijana katika vyuo wasio na uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kwa upana wake...Baada ya kupata fununu juu ya ubadhirifu wa pesa za mahitaji maalumu kwa wanafunzi hao,uongozi wa wanafunzi uliazimia kufanya mgomo ili kushinikiza uongozi wa chuo kutoa pesa zao..cha kushangaza waliambia kuwa ni mgomo unaosukumwa na CDM..walikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wakati Mbunge Godbless Lema akiwa hapa Dodoma kwenye kikao cha bunge alikutana na wanafunzi hao na kuwapa sumu kuwa wagome,na wakaendelea kusema wanazo taarifa za kiitelejensia kuwa ni nguvu ya CDM ndani ya vyuo...kwa hakika mimi napinga ufukuzaji wa wanafunzi katika vyuo sababu ya migomo..wanafunzi wa vyuo ni watu wanaopaswa kupewa uhuru kwa kufikiri kwa makini."CRITICAL THINKING" ili waweze kuja kuwa viongozi bora katika taifa hili..kwa kusema haya simaanishi naunga mkono migomo la hasha! na maana kuwa serikali wanapaswa kujua kuwa kizazi hiki ni tofauti na kizazi cha miaka ya 1947...ni watu wenye uwezo wa kusoma mambo na kufuatilia kujua haki zao za msingi...kwahiyo kazi ya serikali si kufukuza wanafunzi bali ni kubadilika kulingana na mazingira ya kizazi hiki..siku za karibuni nilimshangaa waziri wa Elimu ya juu alipotoa onyo kuwa wahadhiri wasifundishe siasa madarasani..Je wanafunzi wanaosoma POLITICAL SCIENCE wahadhiri wafundishe nini? Huu ni ubwege wa viongozi wetu ambao unadhibitishwa kupitia kauli zao...Mwisho naomba CCM muache tabia hii kwa usalama wenu..

  NB:MODs naomba msiipeleke thread hii kwenye jukwaa la Elimu..hapa ndio mahala pake kutokana na siasa chafu za CCM vyuoni kwasasa...Nawakilisha!!!!
   
 2. data

  data JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,764
  Likes Received: 6,532
  Trophy Points: 280
  ...siasa na elimu wapi na wapi.. wanachuo someni mikmaliza ingieni ktk siasa .. acheni kuchanganya mambo... na huyu LEMA anawapotosha sana
   
 3. Fpam

  Fpam JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona uwezo wa kufikiri kwako ni tatizo.hiyo ni sababu ya kuzoea kusema ndio mzee hebu rejea maneno ya mwl nyerere kuhu su mtu kuwa chuo kikuu
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Elimu yako itapimwa na uwezo wa kuchambua mambo na kuyaelewa.........sijasema wanafunzi waingie katika siasa la hasha!! nasema wapewe nafasi ya kuchanganua na kuyadadavua mambo..
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kwa upande wangu nadhani kila mwanafunzi mwenye umri wa kupiga kura ana haki ya kikatiba ya kuchaguwa ama kuchaguliwa,kupiga kula ama kupigiwa kula,sasa hivyo vyote vina hitaji uijue siasa hata kama ukiwa ktk mazingira ya chuo,kwani hata viongozi wote wa wanafunzi vyuoni wanapatikana kwa mtindo wa siasa huwezi tenganisha siasa na maisha ya kawaida iwe chuoni ama nyumbani

  Kimsingi haki ina gharama zake moja wapo ni hiyo ya kufukuzwa,kwa hiyo kinachotakiwa si kukata tamaa ni kuendelea kuitafuta haki popote pale ilipo hata kama kunawatakao ikosa baada ya kupatikana
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wanataka wasomi wanaowaza kwa matumbo yao tu ili waendelee kutuibia.
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Siasa zilishaingia kila sehemu. Sasa hivi siasa zimetawaliwa na Uchadema na Uccm. Kwisha kazi. Wanafunzi nao wamo.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya zamani ccm walikuwa na ukiritimba wa wanachama wanachuo, leo kumetokea competition kwenye wanachama wanafunzi wanatweta eti "siasa vyuoni haitakiwi!'' wanaamini kwenye hayo?
   
 9. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Poleni sana wadogo zangu lakini ili kufikia demokrasia ya KWELI ni lazima kuwe na Sacrifice...so iwapo CCM Wanawanyanyasa wanavyuo wenye mlengwa wa CDM ..Then tuchukulie kama COST OF DEMOCRACY na kuangalia watasaidiwaje hata KISHERIA iwapo wananafunzi wana ushahidi wa kutosha
   
 10. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 813
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Kuna mfano wa karibuni kabisa.
  Mapendekezo ya muswada wa katiba yalipelekwa kufanyiwa mlimani, kwa maoni yangu ile ni heshima kubwa na uthibitisho kuwa ni matakwa ya serikali kuona wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata fursa hiyo ya kuchanganua na kudadavua mada kama unavyosema.
  Kwa bahati mbaya hali haikuwa hivyo, walidadavuliwa watu badala ya mada na watanzania wengi walishuhudia.
  Turudi kwenye mada. Unasema kuna wanafunzi wamefukuzwa lakini maelezo yako hayajanyooka kwa mtu kupata picha halisi labda kama yupo udom.
  Labda ndiyo maana nashindwa hata kuelewa unawahusishaje Ccm na tukio la wanafunzi kusimamishwa chuo na huku ukihisi kuwa watafukuzwa moja kwa moja? Ndiyo maana nashawishika kuamini kuwa pengine unapindisha maelezo kwa makusudi ili kupata mashabiki wengi hapa, kwamba pengine kuna makosa wamefanya ambayo kwa taratibu za chuo wanatakiwa wafukuzwe.
  Halafu siyo lazima kila kitu kitakachotokea kwenye nchi yetu hii kwa sasa kiwe na uhusiano na u-ccm vs chadema. Inaweza ikatokea, lakini unapotaka kuoanisha matukio kama haya jaribu kujenga hoja zenye nguvu zaidi na wala usililazimishe.
  Kiuhalisia kwa hali ilivyo sasa naamini kushinikiza uongozi wa vyuo kufanya matakwa yao ni kitu cha mwisho kabisa Ccm wanaweza kukifikiria. Kwa sababu its too risky, i know they know for sure. Too risky...
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Amakweli data unazo data, wasome hata fungu lililotengwa wasilidai maana kulidai ni siasa, nchi hii bwana ...
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  WHAT IS NOT GOING ON RIGHT AT UDOM ALL THIS TIME????

  Kuna kila dalili kwamba pale UDOM kuna leadership incompetency, CCM chauvinism in professional activities and outright elements of corruption that daily keep the ping pong between and among the teaching staff as well as students.

  An eagle eye by JF most seriously need to strain itself on this university. Fukuza fukuza hii something is seriously wrong somewhere.

  Subsequently, in my hypothesis here, it could all come out in NOT A DISTANT FUTURE that the person who is currently chasing others from UDOM is but the very candidate who ought to have been pointed out to the UDOM-Gates long time ago.


  Nasema UDOM kuna tatizo!!!
   
 13. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  kwani uwezo wa mwanafunzi kuchambua mambo unatokana na kupewa nafasi za kugoma? mbona kila uchao Udom inaongoza kwa mogogoro inayotokana na kuchagua viongozi wabovu? Education wanataka kugoma kisa wizi uliofanywa na serikali ya wanafunzi iliyochaguliwa na wao wenyewe.hao ndio critical thinkers wanachagua viongozi wao wanaofaa.
  acheni ujinga someni
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  YA WANAFUNZI 27 UDOM KAMA YA BOUAZIZI KULE TUNISIA: SUBIRINI MTAONA MAJUMUISHO YAKE KITAFA ZIMA HIVI KARIBUNI!!!

  Nadhani katika hili umenena na hivyo pindi hawa wanafunzi 27 watakapowaendea kituo chochote cha wanaharakati nchini na kutufafanulia undani wa nini kinachoendelea pale UDOM basi nadhani wengi huenda wakashangazwa suala hili linapobadilika ghafla na kuwa suala la kitaifa endapo POLITICAL CONVICTION AND ALIGNMENT is the immediate cause.

  Wala sitoshangaa serikali mbalimbali za wanafunzi nchini, BAVICHA, CDM, Mhe Julius Mtatiro wa CUF, Zitto Zuberi Kabwe, Mzee Mwenyewe wa siasa za vyuo vikuu huko nyuma Mhe James Mbatia wakilichukulia uzito unaostahili hili jambo ambalo sehemu ya uongozi UDOM huenda inalichezea miythili ya mtoto na kipande cha kaa la moto mkononi!!!

  Nasema wala sitoshangaa Dr Mumbo wa UDASA wakihoji rationale iliotumika kuwafukuza wanafunzi hawa. Pengine wanafunzi wa vyuo vikuu vya huko Arusha na Iringa wakapendezewa kujua undani wa suala hili hata kabla Waziri Nyambari Nyangwini hajastukia danger iliomo mle.

  Nasema tena, UDOM huenda kuna shida kubwa kuliko hata gamba la nyoka kuvuliwa!!!!

   
 15. m

  mwalimu. Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  suluhisho sio kuwafukuza wanafunzi, naomba wasikilizwe wataelewa. tatizo hawa maprof wetu wanajifanya bize sana. huo ni udhaifu,. kweli akili nyingi huondoa maarifa,
  inamaana udom hakuna hata meneja mahusiano, angewasaidia kuficha hizi aibu.
  kama akina kikula na mlacha wangefukuzwaga wao wangefikaje hapo? ubinadamu kwanza u prof baadaye:help:
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM HAKIWEZI KUFANIKIWA KUKANDAMIZA SAUTI HURU KATIKA NGAZI YA CHUO KIKUU KWA MBINU TU YA FUKUZA FUKUZA NA KUPANDISHIA WANAFUNZI GHARAMA YA KUFURAHIA DEMOKRASIA YAO CHUONI HATA KIKAFAULU!!!

  Eti gharama ya fomu kuombea uongozi katika serikali tu ya wanafunzi ifikie mahala ikawa ni sawa tu na gharama ya mtu kuombea fomu kugombea nafasi ya urais kupitia CCM kweli???

  Kwanza mwanafunzi anayeweza kupata hiyo hela yeye anafanya ka zi wapi, anategemeaje kurudisha hiyo fedha na kama si yeye kutoa fedha binafsi, ni nani (tasisi gani) huyo anayemgharami na kwa mapenzi yapi hasa??? Hivi kweli hapa si CCM kuanza kulea UFISADI tangu chuoni kweli???

  I mean, this issue just is TOO SERIOUS a matter that need to be thoroughly investigated by caring media sections and non-governmental organisations to make headway with the whole issue.

  It is a clear affront to the basic human rights; an affront to FREEDOM OF ASSOCIATION, FREEDOM OF SPEECH and more so an assault on the very purpose of why people need to acquire university education - if at all the results were to be true.

  I think this tells a rather bigger story as to why most of us that take entire studies locally are often too timid, dull to appreciate issues freely and rampant lack of critical thinking by higher magnitudes.

  Professor Mlach, with this do you really trust and believe that you could be preparing so well our brothers and sisters for a first-rate global competitiveness both in the job and own-business markets???

  Think about a lot deeper mzee.

   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Watanzania tunaelekea wapi pindi taasisi za elimu ya juu zilizokua zikiheshimika saaannaa katika jamii kwa uhuru wa fikra krimu pale zinapoingiliwa na kirusi cha uendeshaji kwa misingi ya itikadi za kichama na ufisadi kuchukua mimba nyuma hicho kichaka??????????
   
 18. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Ushauri wako ni mzuri.Hawajagundua kuwa wenzao akina GL wanamaisha,na wao bado wanasafari ktk maisha.Watuulize Waathirika wa siasa na Mivyama yenye SERA ZA MSIMU tuwajuze ATHARI ZAKE.jaman mlio na mtakao salimika na timuatimua hiyo TULIZENI VICHWA MSOME,miongoni mwa wanaowashawishi wame disco kwa misup yao,wanatafuta sababu waonekane nao walikumbwa na opareshen TIMUA!
   
 19. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,063
  Likes Received: 7,529
  Trophy Points: 280
  Mbona umewahusisha CCM na kusimamishwa kwa wanafunzi hao? Kama kweli wewe ni muumini wa fikara huru ungeenda mbali zaidi kwa kuonyesha namna CCM ilivyohusika na tukio hilo.
  Binafsi ninasikitishwa na kitendo cha wanafunzi ha kusimamishwa masomo, ni jambo la kuhudhunisha kwakweli, ila nasikitika pia kuona badala tucangalie namna gani ya kukabiliana na tabia hii ya kusimamisha masomo wananfunzi wanaodai haki zao na kwanini wasisimamishwe kazi waliowanyima au kuchelewesha haki zao! Matokeo yake na wewe umeingia kwenye mtego wa walioanza kuilaumu CDM na wewe kuanza kulaumu CCM tena bila ya vielelezo.
  Tuache kuishi kwa historia, ili kuweza kuleta mabadiliko na mapinduzi ya kweli katika jamii, tunatakiwa tuanze kuishi kwa uhalisia. Kwani ukichunguza vizuri utakuta kati ya waliofukuzwa kuna wana CCM na wasio na itikadi za vyama.
   
 20. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Uliye anzisha hii mada unatuchanganya mimi nilitegemea utuwekee fact tuone ni kwa jinsi gani umeonewa. Halafu umesema pesa zimeibiwa je zimeibiwa na nani si unajua hapa ni JF mwaga data zote hapa. Umesema CCM je pale UDOM CCM wanausikaje? Je viongozi pale ni CCM? ina maana hawatumii sheria? Mwaga data zako basi.
   
Loading...