Nasaha zangu kwa chadema kabla ya uchaguzi mdogo wa igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasaha zangu kwa chadema kabla ya uchaguzi mdogo wa igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CR wa PROB, Sep 23, 2011.

 1. CR wa PROB

  CR wa PROB Senior Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote nipende kuupongeza uongozi mzima wa CDM kwa kusimamisha mtu ambaye anaonekana ni makini na mahiri wa hali ya juu, Kiukweli sera zenu na mtizamo wenu juu ya maendeleo ya hili taifa letu unatutia moyo sana hata sisi watu wa lower class ila wenye mtizamo chanya na hili taifa letu.

  Najua ujanja ni kupata bali sio kuwahi na siasa na mchezo mchafu wenye fitina za kila aina, hivyo basi nipende kuwashauri ya kwamba kabla ya uchaguzi kufanyika ni vyema kura zote mzifanyie uchunguzi ili kuepukana na kuletewa zile kura za moto zilizoivua madaraka ngome ya CUF pale temeke miaka michache iliyopita. Hivyo basi fanyeni mfanyavyo ili kuepukana na zile kura za MOTO ambazo mahasimu wenu CCM huwa wanazitumia mara nyingi wanapoona hali ni mbaya ni kwao.

  Mimi kama kijana mzalendo sitopenda kusikia malalamiko baada ya uchaguzi aidha ya kuchakachuliwa au vipi.

  ENYI WAKAZI WA IGUNGA NCHI HII INAHITAJI KIONGOZI JASIRI ATAKAYETETEA WANYONGE WOTE, NA KAMWE HAWEZI TOKA CCM.
   
Loading...