Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,580
- 6,123
Nina rafiki yangu ambaye amekuwa akilalamika kwa miaka mingi kuuliwa kwa Wakala wa meli Tanzania yaani National Shipping Agency Company au NASACO.
Ukimsikiliza Mkinga kwenye hizi Video, unakubaliana kabisa kuwa Mkapa na wenzake waliiuwa NASACO ili waanze kuiba pale vizuri. Wizi huu unaofanyika sasa hivi bandarini, umechangiwa sana na kutokuwepo kwa NASACO maana wenye meli ndiyo wanajihudumia pale bandarini na matokeo yake kudanganya na Serikali kutokulipwa kodi au bidhaa kama meli ya ndovu kuja kushikiwa Vietnam maana usimamizi wa mizigo hapo bandarini unafanywa na watu binafsi.
1.
2.
3.
Ila pamoja na kumsikiliza Mkinga, inabidi nikiri kuna mengine ana CHAPIA kidogo. Nafikiri kwa maswala ya NASACO, hilo atakuwa analijua sana ila kwa maswala ya nje, simwamini sana.
Kama Mtaalamu wa maswala ya Usafiri, angelijua kuwa MAERSK ni meli za Denmark na siyo Sweden. Pia hili swala la Texas sina uhakika sana nalo.