Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Miaka michache iliyopita serikali ya China ilitaka kununua haki zote za uwakala wa meli za Marekani, huku ikiahidi kutoa dola bilioni 200. Marekani ililikata ombi hilo na pamoja na kuyumba kwa uchumi wa taifa hilo kubwa bado kazi ya uwakala wa mizigo ya bandari inafanywa na marekani yenyewe. Vipo vitu ambavyo serikali makini inaweza kuingia ubia na serikali nyingine, lakini sio suala la umiliki wa shughuli za bandari zikiwemo zile za uwakala wa mizigo ya bandarini. NASACO iliuliwa na kilichoiuwa ni ukosefu wa uzalendo. Madhara ya kifo cha NASACO ndio hizi hujuma ambazo nchi hii inafanyiwa kila kukicha.
Awamu ya tano imekuja na falsafa ya kuitanguliza nchi na maslahi yake kwanza, NASACO ifufuliwe upya, haya makampuni yenye kufanya shughuli zote za uwakala yaende yakatafute shughuli nyingine huko nje. Wepesi wa kampuni za kigeni kuja nchini halafu zinakuwa na uhuru wa kutoa mizigo, kuipeleka kwenye yadi mbalimbali, kwa kweli ni mambo ambayo yanatudharaulisha kama nchi. Mataifa yote makini yanasimamia bandari zake, yanahakikisha uwakala wa mizigo unafanywa na makampuni yanayomilikiwa na serikali kwa asilimia kubwa.
ATCL na yenyewe ifufuliwe kama ambavyo ameshasema mheshimiwa rais. Ndege zinazomilikiwa na nchi moja huongeza heshima, huongeza uhakika wa biashara za kimataifa kwa maana ya wawekezaji wa ndani na wa nje kuwa na uhakika wa kufika moja kwa moja Tanzania. Upatikanaji wa ndege angalau nane ambazo zitakuwa ni kwa ajili ya safari za nje, utachagiza katika ukuaji wa biashara ya ndege ya ndani ya nchi, utachagiza katika upanuzi wa viwanja vya ndege.
Kilichotukwamisha mpaka tukashindwa kupima kwa undani zile hasara zitokanazo na kuachia mashirika nyeti yakaendeshwa kiholela, ni kule kutoheshimu taaluma za watu. Ile tabia ya mkurugenzi kupigiwa simu na mwanasiasa asiyejua a wala b kuhusiana na mambo ya bandari au sekta ya anga halafu akaanza kupewa maagizo ambayo mbeleni yatakuja kuathiri ufanisi wa shirika. Hii tabia ya wanasiasa kuingilia taaluma za watu, inafaa kufa kifo cha kawaida. Ninaiomba serikali iipige vita kwa nguvu zote.
ATCL na NASACO ni mashirika nyeti na muhimu sana kwa Tanzania. Ipo kila sababu ya kuyafufua upya kwa nguvu kubwa.