Nasa yatuma bomu kuulipua mwezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasa yatuma bomu kuulipua mwezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ituganhila, Oct 9, 2009.

 1. i

  ituganhila Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF salaam.Naomba mnisaidie kwa hili ni zito.Shirika la NASA limetuma bomu kwenda kuulipua mwezi.Lengo lao ni kupata barafu iliyopo katika mwezi. Je hatua hiyo si hatari kwa wanadamu? Gharama za bomu hilo ni $79 Milioni za kimarekani. Je bomu hilo halitaharibu mfumo wa mwenendo wa mwezi katika axis yake? Je hapatakuwa na madhara ya mfumo uliopo kati ya Jua, Mwezi na Dunia? je kitakachotokea huko juu baada ya kulipua hakitawaathiri wanadamu?Je wamekosa katika barafu huku duniani mpaka waktafute mwezini? Dunia ina matatizo makubwa sana kama magonjwa na njaa, vita, matetemeko typhoon yote haya yanahitaji majibu. Pamoja na hayo Marekani kwenye matatizo ya kiuchumi na ukosefu wa ajira kwao pia.Je ni vema kutumia fedha hiyo kwakutafuta maji ya barafu katika mwezi ni matumizi halali? Japokuwa mimi si mmarekani lakini ni mkazi wa duniani. Je athari zitakazo tokea baada ya mlipuko hazitaathiri dunia nzima?Chembe chembe zitakazotoka huko hazitakuwa na madhara kwa viumbe wa duniani. Au dunia( Nchi zote) zimeshirikishwa kwa hili?
  Wanajamii nisaidieni.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wanatafuta maji...Kero zingine mmhm!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hakuna athari zozote kwa dunia zitakazotokea, ni ungaunga tu utaofika huku, na hauna madhara, maana mwezi ni jiwe/mwamba wa kawaida, hauna sumu!Hakuna athari katika mzunguko wa dunia katika axis yake. Hakuna madhara kwa majira ya mwaka.Hakuna madhara yoyoye kwa viumbe hai wala gesi ya duniani huku.Ni kweli kabisa zoezi hilo ni ghali kwa habari ya pesa, lakini tukumbuke kwamba utafiti ni lazima kwaajili ya maendeleo. Huwa inafikia wakati inabidi tusihesabu gharama kama tunataka kutimiza haja fulani.Unaweza kukuta hatimaye kwambamatokeo ya utafiti huo ni mazuri kuliko uwoga wa gharama wanazotumia, na huenda dunia nzima ikafaidika na watoto wetu wakapata elimu mpya kabisa kuhusu anga hizo za juu!Lets be patient pals!
   
Loading...