NASA Yagundua Sayari Saba Zenye Kuwezekana Kuishi Binadamu

muvika online

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
374
283
NASA.jpg

Hapo jana shirika la NASA la nchini marekani lilitoa tangazo maalumu kuwa sasa kumepatikana sayari saba mpya, kwa mujubu wa NASA sayari hizo zenye ukubwa sawa na dunia zinauwezekano wa kuishi binadamu na kingine kizuri ni kuwa sayari hizo ziko karibu karibu sana.

Kikubwa na cha-kushangaza kuhusu uvumbuzi huu ni kuwa sayari hizo ziko karibu Karibu sana kiasi kwamba ukiwa kwenye sayari moja unauwezo wa kuona sayari nyingine zikipishana, pia vile vile sayari hizo ziko kwenye sehemu ambayo inawezekana kabisa sayari hizo kuwa na maji hivyo uwezekano wa viumbe hai kuishi huko ni mkubwa sana. Sayari hizo zimepewa jina la TRAPPIST kutokana na jina la darubini ambayo ndio ilitumika kugundua sayari hizo.

Kwa sasa habari pekee kuhusu ndani ya sayari hizo za TRAPPIST ni kuwa sayari hizo inaweza kuwa na barafu pekee uku zikizungukwa na maji mengi sana. Lakini bado watafiti hao hawajaingia ndani ya sayari hizo ila inategemewa kutengenezwa darubini mpya kutoka NASA ambayo ndio itasaidia kuangalia sayari hizo kwa nje pamoja na hali ya hewa ili kuhakiki kama sayari hizo zitafaa kuishi binadamu.

Kwa habari zaidi kuhusu sayari hizi unaweza kutembelea tovuti ya NASA kuangalia picha na video kuhusu sayari hizo. Hii ni habari kubwa sana kwa siku ya leo tarehe 23.02.2017 hivyo hakikisha unapitia tovuti hiyo ya NASA ili kujua zaidi kuhusu ugunduzi huo.
 
"God is dead we have killed him"
Hayo Maneno ya zarathrusta yalinijia sana kichwani nilivyoona hii habari
 
kuna maajabu mengi hayajafunuliwa. tungepewa hata miaka 200 hapa duniani tungeshuhudia mengi.
 
Eti wanatudanganya we baki tu na hiyo kauli mbiu yako ya WANATUDANGANYA. Ndugu hapa juu angani kuna maajabu mazito ambayo hata robo ya ugunduzi wake haujafanyika. Ndo maana hao wansayansi wakigundua kitu kuna akina sisi tusiokuwa na hata darubini toyi tunapinga kwan hatuna vifaa.
 
as long as source ni moja na mimi naungana na wengine kukataa hizi mambo, siku china, urusi, india, japan na wengineo wakiprove nao nitaamini la sivyo tutapigana changa la macho kama mambo ya mweZi hapa.

dunia yetu wenyewe hata robo bado pia hatujaijua, mwaka 2011 kuna scientist waligundua species 20,000
18loxbr9cn23xjpg.jpg

sasa imagine wote hao ndani ya mwaka.

ukija kwenye mineral sidhani kama tumefika hata 5%, kwenye bahari ambayo karibia robo tatu ni yeye nako sehemu kubwa ya bahari hakuna binadamu hata mmoja amefika, au chombo cha binadamu pia hakijafika.
 
NASA.jpg

Hapo jana shirika la NASA la nchini marekani lilitoa tangazo maalumu kuwa sasa kumepatikana sayari saba mpya, kwa mujubu wa NASA sayari hizo zenye ukubwa sawa na dunia zinauwezekano wa kuishi binadamu na kingine kizuri ni kuwa sayari hizo ziko karibu karibu sana.

Kikubwa na cha-kushangaza kuhusu uvumbuzi huu ni kuwa sayari hizo ziko karibu Karibu sana kiasi kwamba ukiwa kwenye sayari moja unauwezo wa kuona sayari nyingine zikipishana, pia vile vile sayari hizo ziko kwenye sehemu ambayo inawezekana kabisa sayari hizo kuwa na maji hivyo uwezekano wa viumbe hai kuishi huko ni mkubwa sana. Sayari hizo zimepewa jina la TRAPPIST kutokana na jina la darubini ambayo ndio ilitumika kugundua sayari hizo.

Kwa sasa habari pekee kuhusu ndani ya sayari hizo za TRAPPIST ni kuwa sayari hizo inaweza kuwa na barafu pekee uku zikizungukwa na maji mengi sana. Lakini bado watafiti hao hawajaingia ndani ya sayari hizo ila inategemewa kutengenezwa darubini mpya kutoka NASA ambayo ndio itasaidia kuangalia sayari hizo kwa nje pamoja na hali ya hewa ili kuhakiki kama sayari hizo zitafaa kuishi binadamu.

Kwa habari zaidi kuhusu sayari hizi unaweza kutembelea tovuti ya NASA kuangalia picha na video kuhusu sayari hizo. Hii ni habari kubwa sana kwa siku ya leo tarehe 23.02.2017 hivyo hakikisha unapitia tovuti hiyo ya NASA ili kujua zaidi kuhusu ugunduzi huo.

Mmmmh!
 
Eti wanatudanganya we baki tu na hiyo kauli mbiu yako ya WANATUDANGANYA. Ndugu hapa juu angani kuna maajabu mazito ambayo hata robo ya ugunduzi wake haujafanyika. Ndo maana hao wansayansi wakigundua kitu kuna akina sisi tusiokuwa na hata darubini toyi tunapinga kwan hatuna vifaa.
Kweli kuna mambo mengi nje ya dunia ila tatizo science ya leo imekuwa corrupted.
 
Back
Top Bottom