Nasa Artemis 1: Majaribio kuanza muda mchache ujao

mike2k

JF-Expert Member
May 12, 2016
1,458
3,127
MAJARIBIO YA ROCKET YA MWEZINI YATAANZA MUDA MCHACHE

Muda mchache kuanzia sasa Majaribio ya urushwaji wa rocket itakayotumika katika safari mbalimbali za mwezini na anga za mbali kwa ujumla utafanywa ambapo tutashuhudia rocket ya Space Launch System ikielekea katika safari yake ya masiku kadhaa kuelekea katika mwezi wetu

Majaribio haya yatalenga kufahamu utendaji wa kazi wa rocket hiyo ambayo imesemekana ni rocket yenye nguvu kwakuwa inasukumwa na engine kubwa kabisa 4 za Rs25

Kufanikiwa kwa majaribio ya rocket hii kutafungua panzia lengine la chunguzi na safari za mwezini linalojulikana kama Artemis mission ambapo awali Apollo mission ndio ilikuwa ikitumia na kutuwezesha kuona wanadamu 12 wakikanyaga katika uso wa mwezini kuanzia miaka ya 1969-1972

Safari za anga za mbali huwa ni safari ngumu sana ambazo zinahitaji umakini wa vitendea kazi ambavyo vitasababisha usalama wa safari nzima kutoka duniani kwenda mwezini na kutoka mwezini kurudi duniani

🔳Rocket haitakuwa na watu ndani yake bali itakuwa tupu na itakuwa ikijiongoza yenyewe yaani autonomous na kwa mara nyengine itakuwa ikipokea command kutoka kwa waongozaji

🔳Safari itaanza katika mida ya saa 15:00 mchana kwa masaa ya afrika mashariki ila kutakuwa na maelezo mbalimbali ya mission nzima kabla ya muda huo kufika

Facebook: Moudyswema
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…