JOASH MUSSA
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 515
- 199
Napinga ujengwaji wa barabara za juu au flyover Dar, badala yake hizo fedha zipelekwe kwanza Mikoani, Wilayani ambako hamna Barabara, kwa mfano kwenye kuunganisha Mikoa kwa Mikoa kama vile Tabora-Mbeya, Mtwara- Ruvuma, Kondoa-Handeni, Ifakara- Handeni-Lushoto, Arusha- Musoma n.k.
kwa kufanya hivyo kutawezesha pia Watu waishio mikoa mingine kujikomboa kiuchumi, Dar tayari tuko mbali sana kiuchumi ukilinganisha ni mikoa mingine, hivyo haileti maana kuendelea kuwekeza fedha zote hapa Dar!
Halafu isitoshe kabla hata ya kufikiri kujenga hizo flyover kwanza barabara za mitaani zote zijengwe na kupitika kama walivyofanya Barabara za oysterbay,Masaki, ambazo zimewaondelea foleni wakazi wa huko ingawaje uwiano wa watu wenye magali kwa wakazi wa huko ni mkubwa kuliko sehemu yoyote ile ya nchi yetu hivyo basi wajenge kwanza br pia sehemu kama za Sinza, Magomeni, Temeke, Vingunguti, n.k yaani flyover ziwe hatua ya mwisho kabisa.
foleni mijini haimalizwi na flyovers bali kwa kuimarishwa usafiri wa umma, kudhibiti magari madogo yenye abiria mmoja mmoja kuingia katikati ya mji na kutawanya sehemu zinazotolea huduma (masoko, ofisi, magereji, shule, vyuo, viwanda) kwenye mitaa, wilaya na mikoa tofauti vinginevyo foleni itahamia hukohuko juu ya flyovers
Huyo ni UVCCM sio BAVICHA.Bavicha kwao upinzani ni kupinga kila kitu.
Ungetupa angalau projection ya barabara kilometa ngapi zinaweza kujengwa kwa gharama za fly over moja ya tazara.
Kuna watu wao ni kupinga tuu.
Siasa zinaturudisha nyuma sana.
Maendeleo yanawashika pabaya.. that is why kila kizuri mnapinga.. maana dah mnaona vsingizio vina pungua sasa
Wazo lako ni zuri pia ni sahihi!
Dar Es Salaam Haihitaji barabara za juu katika kipndi hiki. Dar inahitaji barabara za mitaa (street roads), Barabara lishi (Feeder Roads) na nyongeza ya barabara tawanyishi (Arterial Roads). kwa mfano hivi Sasa Dar in arterial roads nane tu! wakti zilitakiwa angalau ziwe ishirini kwa uwiano wa safari za magari jijini.
Napinga ujengwaji wa barabara za juu au flyover Dar, badala yake hizo fedha zipelekwe kwanza Mikoani, Wilayani ambako hamna Barabara, kwa mfano kwenye kuunganisha Mikoa kwa Mikoa kama vile Tabora-Mbeya, Mtwara- Ruvuma, Kondoa-Handeni, Ifakara- Handeni-Lushoto, Arusha- Musoma n.k.
kwa kufanya hivyo kutawezesha pia Watu waishio mikoa mingine kujikomboa kiuchumi, Dar tayari tuko mbali sana kiuchumi ukilinganisha ni mikoa mingine, hivyo haileti maana kuendelea kuwekeza fedha zote hapa Dar!
Halafu isitoshe kabla hata ya kufikiri kujenga hizo flyover kwanza barabara za mitaani zote zijengwe na kupitika kama walivyofanya Barabara za oysterbay,Masaki, ambazo zimewaondelea foleni wakazi wa huko ingawaje uwiano wa watu wenye magali kwa wakazi wa huko ni mkubwa kuliko sehemu yoyote ile ya nchi yetu hivyo basi wajenge kwanza br pia sehemu kama za Sinza, Magomeni, Temeke, Vingunguti, n.k yaani flyover ziwe hatua ya mwisho kabisa.
Una mawazo ya kupinga kila kitu!
safi GT
tumepiga kelele wee, kama kawaida yao CCM...akili zao ziko matakoni
what is happening now ni shifting of problem from these junctions to other junctions!! then tutajenga tena flyover kwa ajili ya hizo junctions
by the way undeground ways are superior to flyovers. Unaweza kutumia undeground kwa mambo mengi pia, kutoa maji machafu, electric wires, cables, etc!!!
Nakuunga mkono, kwanini flyover dar wakati bado nchi hii inatope badala ya lami huko mikoani na wilayani??
Mambo ya Kitaalamu, waachiwe wataalamu, hii ni sawa na wakati wa Nyerere ambapo alikuwa anafanya mambo ya ki taalamu bila utaalamu na hatimaye ilisababisha hasara kadhaa hata kupelekea uchumi wetu kuyumba, tusiendeshwe na mihemko, mtu unahemka unataka jambo flani liwe bila kuangalia faida na hasara zake
huko mikoni, inatakiwa yaboreshwe mashamba ili tukuze kilimo sababu tuna ardhi ya kutosha tena yenye rutuba