Hujaonyesha sawasawa kama unataka mfumo mzima wa allowances na hiyo sheria viangaliwe upya, ila wewe unaonyesha umeguswa na malipo ya Lema. Hilo linafanya hoja yako kuwa dhaifu mkuu.Ndicho ninachopinga, malipo kama haya hapana kama yapo yaondolewe, watu walipwe mishahara yao tu
Mfanyakazi gani alilipwa posho za mafuta baada ya kusimamishwa, na kama wapo ndio tunataka UKURASA mpya sasa, kwani ni lazima tuendelee na mfumo mbovu?
ndio maana nikasema kama lema leo atakuja na kutetea hizo posho, basi asiendee bunge kuhoja matumizi ya serikali kwa lolote maana amelizika nayo, huo unaweza kugeuka unafiki kwa kusema na kutenda tofauti,
WALK THE TALK
[/QUOTE Acha ukomba wa kujikomba kwa ccm mbona hupinga mafuta anayopewa naye kama mbunge hali anatumia magari ya waziri mkuu. hujasikia lowassa ni waziri mkuu mstafu hivyo analipwa marupurupu ya uwaziri mkuu hali ni mbunge analipwa tena hayo mafuta,
kuhusu kulipwa gharama za kesi unachekesha kweli hujui maana ya kulipwa gharama za kesi mawakili waliomtetea umewalipa acha ujinga
Fair enough , lakini posho sasa basi regardless
stahiki ni stahiki
mafuta hupewa wabunge kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wake
garama anazolipwa ni sawa na angekuwa bungeni
hata hivo garama alizotumia kuzunguka nchi nzima kuangamiza magamba ni zaidi ya hiyo
hayo unayosema tuyaweke kenye katiba mpya mkuu
lakini tukipiga kelele kwa lema peke yake au hapa JF haitoshi
if it is according to the law your argument is raw rubbish.
Downs mbona inalipwa hujapinga? ni stahiki zake ni lazima alipwe kwa mujibu wa sheria, Lema hajatunga hizo sheria, unashindwa kuwa na Uchungu na Mabilioni ambayo Downs italipwa unaenda kudai milioni 80.
Ndugu Vikwazo;
Kuna mambo mawili nayaona hapa;
1: Hoja ya kwanza ni ukaidi na maslahi ya CCM na serikali yake, kwamba CDM walipendekeza kutazamwa upya kwa sheria na kanuni zinazoruhusu posho kwa mfumo mzima wa serikali. Lakini bwana Vikwazo utakubali au kukumbuka jinsi wabunge wa CCM walivyo badili mada na kuwageuzia wabunge wa CDM kuwa wanafiki na kila neno la kuwabeza lakini haya ndio madhara yake. Na sio hilo tu hata MISHAHARA ya watumishi wa serikali na idara nyingi inatofautiana sana. Kwa mfano TCRA iliyo chini ya wizara ya Mawasiliano wana salary scale zao, TRA pia hivyo hivyo. Hata posho zao pia zinatofautiana sana. Nakubaliana na wewe kuwa sheria hizi ni mbovu.
2: La pili ni kuwa Lema hawezi kuwa kondoo wa kafara, anapaswa kulipwa stahiki zake zote, tujifundishe hapa sasa. Lakini naona swala moja, kama tunakubali alipwe mishahara yake kwa nini tunakataa posho zingine asilipwe!? Sioni sababu ya kumlipa mishahara yake afu tumkatalie. Hakulipwa mshahara kwa miezi 8 kwa kuwa hakuwa mbunge, ndio sababu hiyo hiyo hakupewa posho ya vikao, mafuta, na hela ya jimbo. Kama anapewa mishahara yake basi imebainika bila shaka kwamba Mahakama Kuu ilifanya makosa hivyo Lema alikua "forced" kuachia ubunge wake hakufanya kwa hiari yake. Basi haikua hiari yake asitekeleze majukumu yake ya kibunge (POSHO), kufanya shughuli za jimbo (MAFUTA na HELA YA JIMBO).
Lakini pia Lema mwenyewe amesema kama milion 60 hivi sio 80 na Katibu wa Bunge, Ndg Kashilila kasema pia wataangalia aina ya mafao/stahiki za kumpa.
ANGALIZO; Siasa na vyama vipo na vitapita tuweke mbele MASLAHI ya TAIFA, hoja ya msingi hata ikiletwa na wabunge wa upinzani ishughulikiwe kwa umakini sio sasa mambo yanavyokwenda CCM against CDM. Tazama hata hoja ya Katiba.
Hujaonyesha sawasawa kama unataka mfumo mzima wa allowances na hiyo sheria viangaliwe upya, ila wewe unaonyesha umeguswa na malipo ya Lema. Hilo linafanya hoja yako kuwa dhaifu mkuu.
Nadhani kunatakiwa uangalifu zaidi katika kufungua kesi kama hizi. Gharama zake kwa taifa ni kubwa kuliko ufahamu wa wengi, hiyo milioni 80 ni chenji ukilinganisha na gharama za hiyo kesi.
Walioianzisha hiyo kesi na waliokubali iendeshwe wanatkiwa kulipia hizi gharama.
argument yako ni ya kiitikadi zaidi na haisaidii kukijenga chama zaidi ya upuuzi kama ule wa zito kabwe na posho hizo hizo kwa wabunge. kimsingi lema anastahili kulipwa kwa mujibu wa stahili ya wabunge (political figure) lakini swala la posho ya jimbo hata kama lema alisimamishwa ubunge arusha walistahili kupewa pesa hiyo labda cha kujiuliza mwandishi wetu wa mwanzo alifanya utafiti wa kutosha? posho ya mafuta huenda sambamba na kazi kama alisimama hawezi lipwa.
Kuna mabo mengi sana pia yanaungana na hii hali. Tunaweza kuwaza kuwa walioshtaki walikuwa wenyewe lakini ukakuta ina uhusiano na chama tawala. Na tunafahamu kuwa njia mojawapo inayotumika ni kuvidhoofisha vyama vya upinzani kiuchumi ili vishindwe kufanya kazi. Ndiyo maana ilitegemewa kuwa baada ya rufaa moja kukubali hukumu ile ya kubatilisha uchaguzi wa Mh. Lema basi Chadema itakuwa hoi na wataachilia mbali.Kiongozi hukumu ikishapita kwa mmoja inakuwa kanuni/maelekezo ya baadaye, kama leo wakikubaliana na sisi kwamba haya malipo sio sahihi inamaana haya malipo ya aina hii yatakuwa dead meat, yatakoma kwa kila mtu, kuna njia nyingi za kushinikiza serikali, kama lema ni mpambanaji wa kweli now is the time to shine and speak loud,
Kuna watu wanatetea kwa kusema mbona ccm wanakula, mbona DOWANS/EPA lakini swali langu ni je CHADEMA inajianda kuwa toleo jingine la ccm? tutawaamini vipi kuwapa serikali kama wasipotekeleza haya kwa vitendo sasa.
Kwa kifupi hii hoja inaipa chadema nguvu zaidi hapo baadaye, wakienda kinyume swali litabaki tutawaamini vipi kwa wao ku embrace mambo ya ki-ccm
Kumbe tunasheria nzuri leo? sasa tunaposema raisi ana madaraka makubwa uwa unaongelea nini? sio kwamba yanatokana na katiba?
Haya ni malipo ya kifisadi, wangelipana ccm argument ingekuwa ni ile ile, yaani matumizi mabaya ya kodi, sheria za nchi ziko wazi mshahara na sio posho kama wanavyodekezana wabunge, sio hawa wabunge walioongezeana mshahara bila sign ya raisi?
Kumbe pesa TAMU, sasa nimeanza kuelewa kwa nini ccm wanaleta dharau, ni kwa sababu hizi hizi sisi wananchi na vyama vya upindani kutokuwa makani
The argument is correct but what need to be changed is the whole rotten system set to benefit some people especially "the class of haves'
kama wabunge wanajiongezea mishahara na malupulupu bila kibali cha rais who do you think is the bogus between wabunge na rais wako? sheria mbovu haziwezi kuondoka bila kuiondoa ccm, ccm must go followed by all bad laws in her grave.
Moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti.
Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu.
Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima.
@VIKWAZO (jina hapo nimebadilisha) ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. @VIKWAZO (Nimedadilsha jina tena) analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.
achukue tu akawalipie ada watoto aliokuwa anawsomesha and then itabidi afanye kazi mara mbili kufidia muda uliopoteaKwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.