Napinga sehemu ya malipo ya Lema...

Napinga sehemu ya malipo ya Lema...

Mzee wa kuaga kwao alisema hataki posho kumbe yupo anaiandaa PM7. Siasa ni mchezo mbaya sana
 
bwana vikwazo mimi naunga mkono hoja ya kuwa na sheria makini ktk suala hili. Tatizo la hoja yako ni timing. Umeleta hoja wakati uliposikia hayo madai ya mh. Lema. Sasa tunajiuliza malipo mengine hewa yaliyokwishafanyika huko nyuma na ambayo yanaendelea kufanyika mbona uliyanyamazia? Mfano ni malipo ya EL kama wazir mkuu mstaafu wakati alijifukuzisha mwenyewe, dowans, mishahara na posho kwa wakuu wa wilaya wasiokuwa na manufaa kwa nchi, posho za vikao maofisini na bungeni, nk.
 
Kwa hiyo Chadema mnachaguwa zile sheria zenye maslahi kwenu mnaziacha zile ambazo zinawabana kama za maandamano ndiyo mnapambana nazo. Lema anakuchuwa pesa ya mafuta wakati ajaendesha ilo gari la mbunge. Halafu anajitapa anataka kuwakomboa...
sheria mbaya kuwepo kila mtu anasema hata magamba wenyewe wanalalama kuwepo kwa sheria mbaya sasa kwanini tusizitoe mbaya na kuzisema kwa nguvu zote?Ni wewe tuu na CCM yenu hutaki hizo sheria mbay azitolewemkiamin kuwa siku moja zitawasadia.Bahati mzuri utambuzi wenu hautoshi kuwapa nafasi ya nyie kuzitumia hata vibaya tuu
 
Mkuu nakubaliana na wewe,na ndo maana namwomba allah ccm idondoke haraka iwezekanavyo,kuna sheria na kanuni nyingi za kulinda mfumo wa dhuluma. Wabunge wengi wa CCM ni mzigo ndani ya bunge letu tukufu.
 
IMEFUTWA....Neno la kudhalilisha
PAW
Hii masalia inaweza fanya watu wanyimwe haki zao za msingi
labda Ben Sanane anaweza saidi kama hii ni moja ya masalia

Anyway nenda kasome hizo nyuzi na masalia kuna comments zangu nyingi tu zitakupatia mwelekeo.
Tutachotetea ni nini? kwa nini Dr Slaa alisema tunaitaji mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 akiingia ikulu kama
sio uozo kama huu? ina maana leo tunakumbatia posho kwa sasa moja ya wanufaika ni Lema? au mwana CHADEMA
, sina tatizo cha chama chochote ila sitokaa kimya ninapoona uozo ndani ya nchi yangu
 
Mkuu nakubaliana na wewe,na ndo maana namwomba allah ccm idondoke haraka iwezekanavyo,kuna sheria na kanuni nyingi za kulinda mfumo wa dhuluma. Wabunge wengi wa ccm ni mzigo ndani ya bunge letu tukufu.

Hiyo ndio kero yangu kubwa, ila leo naona kuna watu wanatetea hivi hivi sheria zinazotoa mwanya mpaka kwa kuongozi wabovu kuendelea na madaraka, sheria zinazoipa mamlaka kubwa ikulu, sheria zinazotua mianya kwa tume ya uchaguzi kufanya uhuni kwenye chaguzi, sheria zinazotumia leo kumlipa LEMA posho ya mafuta kwa gari la kibunge alilosimamisha kulitumia kibunge kwa miezi nane, huu ni uhuni, wachache tunazipiga vita hizi sheria mbovu mpaka misingi imara itakapojengeka
 
Kuna watu wanaleta utetezi kisiasa kwa kuzani kila mtu mwanasiasa, sasa hapa watakwamba hata hoja ya kukataa posho za wabunge itakwama, mantiki kuwe na malipo ya haki kama vile mishahara na sio posho wakati ujafanya kazi.

Posho kama ya mafuta wakati hakufanyakazi kwa miezi 8, sio sahihi

Hivi mbona mnapiga sana kelele kuhusu ya LEMA? mbona hamzungumzii ya Sumaye, Warioba, Lowasa, wanaolipwa 80% ya mshahara wa Pinda wanafanya kazi gani kwa sasa? Tunao Mwinyi, Mkapa pia wapo kule Zanzbar hayo hamyasemi kama sheria kurekebishwa ilitakiwa irekebishwe tangu zamani. Ingawa sio vibaya hata ikianzia hapa kwani itaonyesha jinsi CHADEMA ilivyo na uchungu juu ya matumizi ya fedha yasiyo ya lazima.
 
Nakubaliana na tatizo aliloliainisha mleta uzi. Lakini hapa tunajadili symptom ya ugonjwa na si chanzo cha ugonjwa wenyewe. Tatizo letu ni tatizo la sheria mbovu, na uholela wa taratibu elekezi

Udhaifu/chanzo cha ugonjwa ni bungeni, kwa kuwa ndio watungao sheria na pia ndio wanaoisimamia serikali katika matumizi yake. Wabunge wasipokuwa wajenga hoja, na wenye utayari wa kukosoa haya yote ni matokeo yake.

Wabunge wengi ni kama maafisa miradi, wako hatihati daraja likamilike, visima vikamilike n.k. ili wachaguliwe tena. Kazi hii si yao ni ya watendaji wa Halmashauri au mamlaka husika (mf. Tanroads).

Hili litukumbushe pia kuna umuhimu wa kuwa na wabunge wenye uwezo wa kujenga hoja na wasioogopa kukosoa serikali.

Ironically wabunge kama hao: Mnyika, Zitto, Mdee, Lissu, Filikunjombe, na kwenye bunge lililopita tulikuwa na Selelii wanapigwa vita na serikali na wana JF walio watetezi wa serikali.

Kisha hao hao wanaleta malalamiko ya symptoms.
 
VIKWAZO;5299760]Sawa lakini na sisi wananchi tuna haki ya kuhoji jinsi pesa yetu ya kodi inavyotumika, kumbuka LEMA ni sehemu tu ya wanaolipwa haya malipo yasiyo na msingi [ hapa naongelea posho na sio mshahara wake
[/MENTION]Bado nataka unijuze uhalali wa kulipwa mshahara ambao hajaufanyia kazi kama zilivyo posho.
 
Bado nataka unijuze uhalali wa kulipwa mshahara ambao hajaufanyia kazi kama zilivyo posho.
Hiyo ni sheria ya kazi kwa ngazi zote tu. Kama alikuwa hayuko kazini tokana na maamuzi ya mahakama, na kisha mahakama ikatengua maamuzi ya awali anapaswa kulipwa pesa iliyokuwa halali yake kama mshahara.

Hii ni haki yake. period
 
Ndicho ninachopinga, malipo kama haya hapana kama yapo yaondolewe, watu walipwe mishahara yao tu
Vikwazo,,jambo hili kwa bahati nzuri, limetokea kipindi kizuri, ambapo tunatoa maoni ya kuunda katiba yetu mpya!

Nakushauri fungukia huko, usilalamike hapa jamvini, tutasoma, tutalaani, lakini tusipoitumia hii fursa tukadai iingizwe kwenye katiba(Sheria Mama), litabaki kutuuma na hakuna hatua ya maana itafanywa zaidi ya sura ya wivu!

Kama waliomfitini walidhani wanamkomoa sasa watashangaa! Mtu alikuwa active katika masuala ya chama chake full time, yet stahili za kibunge analamba pia! Bora wangemuacha weajipange mwaka 2015 kuliko walichokifanya!
 
Kwa sasa LEMA anaweza kukikataa hiyo pesa chafu, kisha kuweka shinikizo ili tuwe na sheria bora, hiyo ni kazi yake ya msingi kama mbunge,
Bora wewe umeliona ili suhala kwa mapana yake

yaani hiyo pesa imekuwa chafu kwa lema Tu acheni hizo bana wangapi washalipwa hizo acheni na yeye apige bingo bana ili iwe fundisho kwa kesi zisizo na msingi ikifunguliwa kesi iwe ni ya msingi na iwe ni uhakika kuwa utashinda acha apate stahili zake kapigika sana jamaa kwanza anahitaji na gari lingine la ubunge maana lile la kwake aliwaachia vijana wamelichosha sana.
mi nashangaa hii sheri imeonekana ghafla kwa lema tu tuache hizo bana sio fresh kuna hela nyingi sna kwenye hii nchi zinaliwa bila sababu tungeanza na hizo kwanza .
pia ndio maana mkiambie mfumo wetu ni mmbovu mnabisha mabadiliko ni lazima ili kuweza kukabiliana sheria kama hizi.
sasa mkiambiwa katiba mpya mnaleta ushainii wa jaji Warioba kuse,ma watu wanakaririhswa mambo ya kusema kwenye tume. tuna mambo mengi sna ya kushughulikia kwenye hii nchi lakini viongozi wamefumba macho wako bise na mbwa mwitu kule serengeti.

CHEDEMA wakiwaambia mfumo wa nchi unahitaji overhaul inasema hoo chadema wanaleta fujo sasa wakitumia huo mfumo mmovu wa mchi kulipwa haki zao mnawalilia tena

Kumbuka mwalimu Nyerere aliwahi kusema kutokana na mfumo mbovu na katiba ya magumashi na kuuliwa kwa Azimio la Arusha kunaweza kuzusha kiongozi mmoja mlevi hivi wa madaraka akangangania Ikulu na tusiwe na jinsi ya kumfanya.

sasa hii yote ni mfumo mmbovu waliouweka CCm ili kuiba hela za wananchi
acha ule na kwao kwanini double standard?
 
Sawa lakini na sisi wananchi tuna haki ya kuhoji jinsi pesa yetu ya kodi inavyotumika, kumbuka LEMA ni sehemu tu ya wanaolipwa haya malipo yasiyo na msingi [ hapa naongelea posho na sio mshahara wake]

Acha kujifanya hujui mambo hata madogo...!!

Nani kakwambia HAKI TZ IPO..??! ww zubaa tu...!!
 
VIKWAZO na wewe nenda kafungue kesi yakupinga Hayo malipo coz ndo kazi iliyobaki.
 
Last edited by a moderator:
VIKWAZO

kaka unalilia viela vidogo wakati kuna mahela yapo uswis hata amdai.

Mi naona lema alipwe na wale majaji vihiyo waliotoa hukumu feki ya kumkandamiza lema kwa kulazimishwa na ccm.

Pia alipwe per diem zake mbona wengine wanaenda bungeni kulala kama Wasira na wanalipwa
 
Last edited by a moderator:
Hapa kaka/dada umejichanganya mwenyewe....hakustahili malipo hayo kwasababu hakuwa kazini na kazi za kibunge zilisimama
sasa huo mshahara wa mil 18 alipwe wanini wakat miezi hiyo yote hakuwa mbunge?
 
VIKWAZO

Mfanyakazi yeyote wa serikali anaposhitakiwa hulipwa stahiki zake hadi anapokuwa guilt.

Na iwapo amesimamishiwa stahiki zake wakati kesi inaendelea basi anapo maliza kesi analipwa stahiki zake zote.

Huo ni wivu tu... Kuna mshkaji alituhumiwa kugushi sahihi zap cheque na alikuwa analipwa half salary...sasa.
 
Last edited by a moderator:
Mimi naunga mkono, hii inafanyika popote, kuna mshkaji tunafanya naye kazi alishtakiwa lead kugushi sahihi kwenye cheque kuchukua 18m na kesi ilisikilizwa na mshkaji alikuwa analipwa half salary.

Sasa mshkaji kashinda na anatakiwa kulipwa 36m for being paid half salary, usumbufu mahakamani na mambo mengine mengi. Sasa hizo lead mtazamo wangu ni stahiki zake halali kama wabunge wengine na pia kwa mawakili walio kuwa wanamsimamia hata kama wapo chama kimoja lazima walipwe kwa professional yao.

Hivyo naunga mkono ni juu yetu sasa kibana serikari au juu ya bunge kuibana serikari kwa hasara inazo liingizia taifa.
 
VIKWAZO

KWA HILI HUJAFUNGUKA VIZURI na kama ndo mtazamo wako sahihi hapa umeenda mbali na uhalisia ulivyo,kwani bwana lema sio kama alipenda kuacha kazi ya bunge nakufanya kazi za chama tu,baali ni ufuska wa watu wachache kwa mawazo yao pasipo kuona ukweli wa jambo.

Hawa bwana walijua jimbo wameshindwa kwa uhalali na kuamua kwenda mahakamani na baada yawatu ambao ni majembe katika maamuzi kugundua hilo ndipo wakashini9kiza mahakama kupindisha ule ukweli.hivyo basi mungu hapokei rushwa kesi ndo kama ulivyooona mwisho wake.

So lazima wakubali kwa hasala na faida zote za matapishi yao,ambapo ni shida kwa taifa na baado haijengi kwa wana arusha kwani lema hakufanya vitu vya msingi kwa wana arusha tangu kuondolewa kwenye uongozi wa jimbo.so usilaumu anaekimbia bali laumu anaye mfukuza.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom