Napinga sehemu ya malipo ya Lema...

VIKWAZO

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
1,900
Reaction score
581
Kwanza salamu, pia niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.

Hoja ya msingi ni
MALIPO YA LEMA YANAONYESHA UDHAIFU WA MFUMO WETU.

Lema atalipwa milion 85 Tsh/= kama malimbikizo kwa kusimamishwa baada ya kusimamishwa ubunge,
( kwa mchanganuo zaidi soma hapa
Lema kuzoa Sh85 Milioni - Siasa - mwananchi.co.tz )
kama mwananchi nina tatizo na Lema kulipwa hiyo pesa, sioni Value for money kwa sisi kuwa na mfumo dhaifu kiasi hicho.

Tatizo nililonalo Lema kulipwa hiyo pesa ni maeneo yafuatayo:

1.) Milion 20 za mafuta kama Mbunge, Lema aliposimamishwa ubunge shughuli zake zilikoma, hivyo matumizi ya mafuta kwa shughuli za kibunge yalikoma pia!!! kwangu mimi kumlipa Mbunge Milion 20 za mafuta bila kuwa kazini au kufanya kazi ni kudhurumu wananchi, huu ni mfumo onevu, hiyo pesa haipashwi kulipwa,
kwa maelezo zaidi ni kwamba Lema atarudishiwa ghalama za kesi, ni ghalama zipi hizo? hakuna nauli alizokuwa anatumia? na kama ndio balance ipo itakuwaje tukimlipa tena kama umma pesa ya mafuta?
lakini Je Lema kwa wakati huo alikuwa anafanya shughuli zipi? sio M4C ( i embrace M4C but TAIFA kwanza) huko akulipwa chochote?

2.) posho ya jimbo Sh40 milioni ....... jimbo lipi hali kazi ilisimamishwa? jimbo la Arusha alikuwa na mbunge kwa wakati wote wa kesi? lema akufanya shughuli za kibunge jimboni mwake.
Lakini pia kwa kwenda mbali ni kwamba Lema alikuwa na shughuli maalumu ya chama yaani M4C ( no problems) lakini je hapa kuna tofauti gani na wale wafanyakazi hewa? mtu ayupo kwenye kituo cha kazi analipwa tu? hivi sisi tunalipa majina au shughuli/kazi ya mtu? where is the value for my TAX?

3.) Posho nyingine Sh6.6 milioni Kwa kazi ipi analipwa posho? ubunge ulikoma nimeshaeleza hapo juu, ofisi ya mbunge haikuwa na kazi tena kwa kukosa mbunge, na kama ilikuwepo na ina fanya kazi vipi amri ya mahakama kusimamisha ubunge wa Lema, kwa misingi hiyo nina amini hakukuwa na shughuli ya sisi kama taifa kulipa posho.

<<<<<<
Nakubaliana kwamba Lema alipwe malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milion, hii ni haki pekee kwa Lema, sikupaliana kwamba kama mtu umesimamishwa wazifa wako basi umma uendelee kukulipa pesa bila kuutumikia.

CHOMBEZO

HITIMISHO:
Hoja yangu ni tuwe na kanuni zenye macho, zinazothamini kodi yetu, malipo lazima yenye thamani ya kazi, malipo holela ni hatari kwa taifa, napinda haya malipo regardless nani anapewa, msingi ni kuwa na taifa imala lenye uchumi unaonufaisha wote.

Kama kuna sheria zinatoa mwanya huu zifutwe mara moja ili kuongeza thamani ya pesa yetu katika matumizi (VALUE FOR MONEY)

NUKUU



 
Downs mbona inalipwa hujapinga? ni stahiki zake ni lazima alipwe kwa mujibu wa sheria, Lema hajatunga hizo sheria, unashindwa kuwa na Uchungu na Mabilioni ambayo Downs italipwa unaenda kudai milioni 80.
 
Mbona kawaida tu hiyo emu kajaribu kuulizia mfanyakazi wa TRA au bandar akisimamishwa akirudi inakuwaje kama ujaambiwa wanalipwa mpaka ela zao za chai za miaka yote waliokua benchi
 
Mbona kawaida tu hiyo emu kajaribu kuulizia mfanyakazi wa TRA au bandar akisimamishwa akirudi inakuwaje kama ujaambiwa wanalipwa mpaka ela zao za chai za miaka yote waliokua benchi

Ndicho ninachopinga, malipo kama haya hapana kama yapo yaondolewe, watu walipwe mishahara yao tu
 
Downs mbona inalipwa hujapinga? ni stahiki zake ni lazima alipwe kwa mujibu wa sheria, Lema hajatunga hizo sheria, unashindwa kuwa na Uchungu na Mabilioni ambayo Downs italipwa unaenda kudai milioni 80.

Kwa hiyo hii ni kulipa kisasi zidi ya mtoa kodi yaani mwananchi? kwa maana nyingine chukua chako mapema au?
hapa naongelea TAIFA bora, weka siasa pembeni
 
unfortunately sheria zetu ndivyo zilivyo.... Kwa sasa hakuna tunachoweza kubadilisha ila tuhakikishe tunapa katiba mpya SAFI imbayo tutabainisha mambo yote yenye utata kwa sasa.....

Swali la kizushi... Mheshimiwa wa Monduli bado anapokea posho ya "Waziri Mkuu MSTAAFU?
 
Bila shaka Bunge lina taratibu sheria na kanuni zake zakuwalipa wabunge wanaorudishwa bungeni kwa mazingira kama ya Mh Lema.
Lema hatakuwa mbunge wa kwanza kulipwa hivyo, kama unavyosema endapo kuna mapungufu katika sheria husika basi marekebisho hayana budi yafanyike.
Hapa swali ninalouliza mkuu kama Lema hapashwi kulipwa marupurupu uliyohainisha hapo juu kwa vile hakuwa mbunge kipindi hicho kwa nini unataka alipwe mshahara wa siku ambazo hakuwa mbunge,nilifikiri kigezo ulichotumia kutaka asilipwe stahiki nyingine kwa nini kisitumike pia kwenye mshahara tofauti hiko wapi?.
 
Kwa sasa LEMA anaweza kukikataa hiyo pesa chafu, kisha kuweka shinikizo ili tuwe na sheria bora, hiyo ni kazi yake ya msingi kama mbunge,
Bora wewe umeliona ili suhala kwa mapana yake
 
Downs mbona inalipwa hujapinga? ni stahiki zake ni lazima alipwe kwa mujibu wa sheria, Lema hajatunga hizo sheria, unashindwa kuwa na Uchungu na Mabilioni ambayo Downs italipwa unaenda kudai milioni 80.

Kwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.
 
Sawa lakini na sisi wananchi tuna haki ya kuhoji jinsi pesa yetu ya kodi inavyotumika, kumbuka LEMA ni sehemu tu ya wanaolipwa haya malipo yasiyo na msingi [ hapa naongelea posho na sio mshahara wake]
 
Kwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.

Kuna watu wanaleta utetezi kisiasa kwa kuzani kila mtu mwanasiasa, sasa hapa watakwamba hata hoja ya kukataa posho za wabunge itakwama, mantiki kuwe na malipo ya haki kama vile mishahara na sio posho wakati ujafanya kazi.

Posho kama ya mafuta wakati hakufanyakazi kwa miezi 8, sio sahihi
 
Sasa siku zote ulikuwa wapi kupinga sheria ya kulipa haya malimbikizi?kwann uanze kupinga ulipwaji wa Lema badala ya kuanza kupinga sheria iliyopitishwa na bunge lenye wabunge wengi wa ccm ili kuhalalisha ulipwaji huu wa mamilioni ya shilingi??HOJA YAKO NI NZURI ILA IMEKAA KISHABIKI
 
Kwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.

K amefanya kazi wewe huoni M4C ailizo kuwa akifanya? niambie hawa wafuatao wana fanya nini Bungeni, Wasira kazi kulala, Mohamed E, na wengineo,

Bora Lema alikuwa akipiga M4C, kuliko hao wanaolala Bungeni na wengine kugeuka Mabubu huko
 

Wewe umeona kwa Lema? Hao wanaoumwa mwaka mzima mbona wanalipwa? Wabunge wangapi huwa hawaonekani Bungeni na wanalipwa? Muhimu ni kuwauliza waliotunga sheria na si kumuuliza Lema, Make Magamba hamfikilii kabla ya kuongea, Unaleta Mambo ya Nepi na Kadi wakati yeye Anamiliki ya CCJ
 
.
..umetumwaaaaaaaaaaaaaa...nenda LUMUMBA kama huna ajira...kukusaidia masika imeanza kalime..kilimo ni uti wa mgongo..chukua na hii ya maabara..kilimo moja!!!
Leo tunaitwa wakulima tukihoji matumizi ya pesa yetu sisi wananchi sio?
 

Kasome hitimiosho nililoweka, lema sio objective yangu, ila ni sheria mbovu, kuna sehemu umeona nimeandika kwamba Lema kateka Bunge na kudai malimbikizo yake.

Anyway nimeona kwa lema na sikubalini na malipo ya ovyo kama haya kwa mtu yeyote.
Tunawezaje kuipinga ccm kwa matumizi mabovu lakini tunashangilia inapokuja kwamba yale matumizi mabovu tunalipwa wapiganaji?

HELA NI NZITO kumbe
 

Mkuu Hizo ni Pesa Ndogo sana na alitakiwa apewe zaidi ya Hizo,alitakiwa apewe Bajeti nzima ya Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana, make ni waizara inayo tengewe Pesa bila kuwa na Kazi ya Kufanya, CCM wakiongozwa na Mkuu wao ndo wanatumia pesa bila jasho, Kwa sasa Mkuru yuko Serengeti ana Consume his own Service, Wachumi wananisaidia hapo, Kile kitendo cha Producer kuwa ndo mnunuzi mkuu wa Product/Service yake mwenyewe ndo anacho fanya Mkuru kule Serengeti, Inapaswa uanzia huko kuhoji na si kuhoji Milino 80

 
zinatoka kwa watu wasio na pesa, hata ccm nao wanapotumbua wanasema ni pesa ndogo kwa VIJISENT ukumsikia?
lazima tuwe na sheria/kanuni makini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…