Napewa Zawadi hii! Du! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napewa Zawadi hii! Du!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eeka Mangi, Mar 31, 2011.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hello JF
  Kuna zawadi nazawadiwa ila kiukweli duh! Kuan jamaa yangu aliwahi kuachwa na mke! By that time jamaa laikuwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Wakati anaachwa walikuwa na mtoto mmoja wa kike. Jamaa aliteseka sana mwisho akaja nyumbani kwetu (meaning mimi na mke wangu) akiwa na mtoto wake wa kike. Tukaongea tukanywa na kula. Huku nje mtoto kakutana na binti yetu wakacheza mpaka wakachoka mwisho msaidizi wetu akawaogesha wakalala. Baba mtu akawa anaaga lakini mtoto akawa kesha lala. Tukamwambia wacha alale tu tutampeleka kesho yake.
  Mtoto kuamka kesho yake tukapanga kumpeleka kwao, kilio alichoangua Mungu ndo anajua. Ikabidi tumwache na kumweleza baba yake. Mwisho tukakubaliana wacha tuishi naye. Mwaka mmoja baadaye baba wa huyu mtoto alifariki na tukamzika. Wakati anafariki mtoto alikwa na miaka 6. Tukaangalia ni nani wakukaa na huyu mtoto! Hatukuona ni busara kumwacha na bibi mzaa baba yake kwa kuwa alikuwa mzee sana. Shangazi mtu alikuwa kama naye anaona kinyaa vile kukaa na huyu mtoto maana walivumisha kuwa wazazi wake wana ukimwi. Ilibidi tukae na mtoto. Tangu wakati huo nimeishi naye na pia kusimamia mali za huyu mtoto baada ya ndugu wa karibu kuniruhusu kuishi na kusimamia hizo mali. Nimemsomesha huyu mtoto hadi kufikia level ya university. Mbaya zaidi bila hata kunishirikisha yeye na binti yangu wameamua kubadilisha u-bin na sasa anatumia wa kwangu. Kwake yeye ni baba yake wa kumzaa haambiwi kitu. Niko katika hatua za kummilikisha nyumba za baba yake kwa sasa maana na mimi sijui siku wala saa ingawa yeye hataki na anasema mali zote ni za familia! Meaning kuwa yeye ni familia yangu hivyo chochote kilichopo kitatunzwa na familia.

  Story inaanzia hapa, last week alitokea dada mmoja na kujieleza kwangu yeye alikuwa mke wa marehemu yule rafiki yangu na alikuwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu akifanya kazi umoja wa mataifa. Ametafuta where about her husband na akaelezwa the whole thing. Pia amemtafuta binti yake naye kamwona. Anadai kuwa binti kamkana na wala hataki kumwona kabisa. Kaamua kuja kwangu ili nimsaidie kumuunganisha na binti yake. Jana nimempigia simu huyu binti! Jibu alonipa ni kuwa naquote "BABA KAMA UNATAKA KUNIONA BASI USINAAMBIE TENA HABARI ZA HUYO MAMA LASIVYO HUTAKAA UUONE HATA MFUPA WANGU!". Kusema ukweli niliogopa sana. Nikampigia mama yake na huyu binti ankanambia yuko hotelini alikofikia. Nikaenda hapo hotelini, kufika kaunta nikamuulizia nikaambiwa aaaaaaaaah kumbe ndo wewe kasema yuko no fulani ukija umwone. Infact I didnt even think what she is planning nikaenda kwenye room yake. Nikagonga mlango kwa upole tu akauliza nani? Nikamtajia jina, mlango ukafunguliwa! Ooooooh my God nilichokutana nacho! A naked woman standing infront of my face! eti welcome dear I just want give you a special gift for growing my girl to that level! Phweeeeeeeeeeeee! Niligeuka nikaondoka bila kusema neno. Sasa najiuliza na hii ndo zawadi?
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh huyo mama ni kahaba mkubwa.
  Ndiom maana binti kamtolea nje .
  Mpotezee kabisa aije mfundisha binti uchangu
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sikutaka hata kumsikiliza tena!
   
 4. BLISS

  BLISS Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza nikupe hongera kwa moyo wa ukarimu uliokuwa nao,
  pili huyo mtoto usimwambie tena habari za mama yake,inawezekana kuna jambo analolitafuta kwako, hivyo usimpe nafasi tena hata ya kukukaribia kwa hayo aliyoyafanya.
   
 5. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mtafutie coart injunction (sina uhakika na spelling) ila ni pingamizi la mtu kujihusisha, kushiriki wala kuwa na mahuriano yeyote na akikiuka unaweza kutaja injunction unayotaka au mahakama ikakushauri. Huyo ni tapeli hata kama ni mama yake wa kumzaa, pata ushauri wa Ustawi wa Jamii ili upate official documents za kum-adopt huyo mtoto, na kwakuwa ni ridhaa ya mtoto, please fanya hivyo. mama anataka mali. Pia mshirikishe mtoto haraka kama ndivyo alivyoamua, basi mali hizo zibadilishwe mmiliki na awe familia/wewe kama msimamizi kama matakwa yake yanavyosema. Huyo ni mtoto wako na si vinginevyo, jiweke sawa kisaikpolojia kumpenda na kumtunza huyo mtoto na ondoa kabisa katika mazungumzo yenu kuwa huyo si mtoto wako. OK!
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nashukuru sana kwa ushauri huu. Ni kwa sababu za kifamilia ningeweza kuweka picha za wototo hawa wawili hapa. Ni zaidi ya mapacha. Wako chuo kimoja na wanachukua fani zinazofanana. Hakuna mtu ajuaye sio mtoto wangu. Ni vigumu sana kugundua kuwa sio mwanetu kama sijakwambia. Mara nyingi huwa hatupendi kuonglea mahusiano yetu na huyu binti. Hatukuwahi ni mpaka hizi chokochoko zilipoanza. Kubadilisha umiliki natamani sana niwaite ndugu wa baba yake ili nimkabidhi huyu mtoto kwanza maana ndo mahakama ilivyoshauri kipindi hicho. Kuhusu huyu mama kuwa mbali na huyu mtoto tunalifanyia kzi kwa karibu sana. Nimewasiliana na mwanasheria mshauri wa familia na tunaandaa utaratibu fulani ikiwa pia ni onyo la kiusalama kwa huyu mama ili binti asije kudhuriwa na kitu chochote. Tangu jana nimefanya kazi hii kwa kasi na haraka sana na Mungu akipenda labda tutakuwa na hati ya dharura ya kumwita mahakamani. Binti ameitwa kurudi huku leo na labda atafika wakati wowote maana yeye ndo mwenye nguvu kisheria.
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu hongera sana kwa moyo huo! But kwa mawazo yangu huyo mama hafai kabisa, kwana zawadi yenyewe kimeo tuu!
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Nakupongeza sana kwa moyo na roho nzuri....Mungu akubariki sana mbe!!

  Naomba umsikilize huyo binti,umemlea mpaka hapo na anakuheshimu,usimwangushe kwa kumuweka kwenye mikono isiyo salama yeye au mali alizoacha baba yake. fanyeni uchunguzi kuhusu huyo mama,yawezekana wala si mama yake,ni ngumu mama kuwa mbali na mwanae all that time,sidhani kama kweli alishindwa kumpata anpodai alimtafuta.....Ni vizuri mambo yakaenda kisheria zaidi ili kwa lolote litakalotokea sheria ichukue mkondo wake....nafurahi huyo mama amerudi mtoto akiwa mkubwa na mwenye akili yake,it makes it easier fo fight her....

  Hongera kwa kushinda jaribu lake la kukupa zawadi,Mungu awape ushindi zaidi kwa hayo mnayoyapigania.
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli wastehili pongezi sana. Ni binadamu wachache wenye moyo kama wako na mkeo!

  Mungu abariki kila unachofanya!

  Amina!
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Dah!
  Hongera kwa moyo ulionao wa kumlea huyo binti.
  Hili suala lako limekaa kisheria zaidi.
  Nafikiri ungepata mwanasheria akueelezea kwa case hiyo inakuwaje.
  Inawezekana mtoto akamkana mama yake wakati sheria inamtambua yule mama na haki zote dhidi ya mwanae bila kujali alichokifanya.
  Kwa wakati huu usiwe karibu na huyo mama na wala unapoishi asipajue.
  Kuna watu wana roho ngumu, kama huyo mama hakuwepo ndugu zake walishindwa kufatilia maendeleo ya mtoto.
  Pole sana, na mungu akutie nguvu.
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Aisee wewe ni mume wangu nini??? Maana hiyo story mmmhhh inanihusu sana hebu ngoja kwanzaaaa
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseee!Huyo mwanamke hazimtoshi kabisa.Si ajabu anamendea mali za marehemu tu.Ila hongera sana kwa moyo ulionao kwa kumlea huyo binti na pia kuyashinda majaribu ya huyo mwanamke.Kwakweli we ni mmoja kati wa wachache wenye roho nzuri na msimamo!
   
 13. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haha haaa labda bana siwezi jua
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tunafuatilia kisheria zaidi kwa sasa. kama nivyowahi kusema mshauri wa kisheria wa familia yangu anafanya mchakato wa kuiweka issue nzima kisheria zaidi. Tumemwita binti ili naye tusikie kwa kauli yake na ikibidi aandike kwa mkono wake mwenyewe. Pia naangalia jinsi ya kuwashirikisha ndugu wa baba yake ingawa walikwishatoa baraka kuwa hawana cha kuongeza kwa jinsi nilivyokaa na huyo mtoto. Maamuzi makubwa wanategemea mimi. Mchakato mzima unafanyika kwa haraka na uangalifu mkubwa.
   
 15. e

  ejogo JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hongera sana mkubwa na Mungu akubariki sana!
   
 16. Malunkwi

  Malunkwi JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakika wewe ni mfano wa kuigwa ktk jamii ila jitahidi kumwelewesha huyo binti ili aelewane na mama yake
   
 17. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,521
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Hesabu zake ziko kwenye properties za huyo binti. Utakapomuunganisha na binti, atakachomfanya hutakaa usahau ktk maisha yako kwani obviously ataishia kumuua. Sikiliza sauti ya mtoto na kwa ulichokiona ctarajii kama utafanya kosa.
   
 18. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hello JF members
  Today have been a long day regarding this saga. Have been up and down to make sure everything is going to be fine. Binti aliwasili kama tulivyotegemea. Tulikaa na advocate na kwa pamoja tukakubaliana kuwa habari ya huyu mama ichukuliwe kisheria zaidi. Pia ilibidi tumwone mkuu wa kituo pale central na kumweleza wasiwasi juu ya usalama wa huyu binti. Baada ya maelezo ya kina ilibidi tupewe WP mmoja pale central Moshi kumwona huyu anayejiita mama wa mtoto. Tulipofika hotelini tuliambiwa kuwa aliondoka soon baada ya mimi kuondoka na hajarudi tena. Taarifa imefunguliwa na yeye atatafutwa na kupewa taarifa kuwa chochote kitakachomdhuru binti kwa sasa she is in for it.
  Pia tumezungumzia kuhusu mali zake nazo amesema kuwa watagawana na yule binti yangu waliyekuwa naye kama mimi sitotaka kumilikishwa kwa familia. Ndugu wa baba yake walileta tabu kidogo kwa kudai kuwa nao wafikiriwe. Binti aliwahoji kama kuna mtu yeyote aliyechangia katika makuzi au hata ada basi ajitokeze ili ajue atagawanaje na huyo atakayejitokeza. Hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Tumemaliza kikao jioni hii na wote wameridhia kuwa tufungue kesi ya mirathi na binti ndiye mwombaji. On monday tutafile case ya mirathi pale mahakama ya mwanzo.
  Nawashukuru sana kwa ushauri wenu na Mungu awabariki sana.
   
 19. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mh! mtu mzima ovyoo, mfano hata kama mm kicheche kwa styke aliyokuja nayo, namkataa. Kwa upande mwengine, Mungu awabariki na awajaalie busara ktk muendelezo wa maisha yenu na huyo binti.
   
 20. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #20
  Apr 2, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  mkuu hii story ime nifundisha,kunifurahisha na pia imenionyesha wewe ni mtu wa namna gani.....ila kiukweli utakua umemwelewa huyo mama ni mtu wa namna gani.
   
Loading...