Napendekeza tumuongezee Kikwete miaka 5

Napendekeza tumuongezee Kikwete miaka 5

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,864
Katika uongozi wa Jk kafanya yafuatayo,
1. uongozi wake wanawake wajawazito na waliojifungua kulala kitanda kimoja 4 imebaki historia, mahospitali yetu yanatoa huduma nzuri tena za kuvutia na madawa yapo ya kutosha.
2.Kapunguza deni la Taifa kiasi kwamba bado tuna uwezo wa kukopesheka.
3.Rais wetu kashinda angani akitutafutia watanzania tukimuongeza miaka ataenda nchi nyingi na Tanzania itakuwa nchi ya neema kwa misaada.
4.Rais ana uchungu na nchi ndo maana hataki kuwabugudhi wawekezaji hata kama wakituibia kwani kwa kufanya hivyo kutazuia wawekezaji kuja kuwekeza.
5. Rais wetu amesaidia kurejeshwa kwa pesa EPa zilizokuwa zimeibiwa na akatumia ubinadamu kuwasamehe wezi wale.
6.Ajira kwa vijana zimeongezeka ndo maana zikitangazwa ajira watu hawaendi wengi matokeo yake huchukuliwa watoto wa wakubwa na kuwekwa kwenye nafasi zile maana watoto wa walalahoi hupata ajira pindi wamalizapo masomo.
7.Kila kijana achaguliwaye kwenda elimu ya juu hupata mkopo hata wale 23000 waliokuwa wanasemwa ni chuki za wapinzani kuichafua serikali.
8.Kipindi cha utawala wake kila mtanzania amekuwa na maisha bora na hii hudhihirishwa na foleni za magari Dar.
9.Mikataba yote kipindi cha imekuwa ya wazi isiyokuwa na chembe ya ubadhirifu hata kidogo.
10.Ukisikia Escrow hizo ni chuki za watu wenye kutaka vitalu vya gesi kwani pesa zile si umma lakini amemsimamisha Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini ili kuridhisha bunge
Kwa haya mazuri napendekeza tumuongezee miaka 5 ili amalizie viporo vya kazi yake vilivyobaki.
 
aendelea kwenda kula bata marekani
 
we ni mpinzani-unahatarisha amani ya nchi amani ikitoweka kina mama na watoto ndio wanaoteseka
 
Kaendeleza uchumi na kutengeneza ajira kwa kuwekeza nchini kwa kutumia kampuni ya PAP ambayo kampuni ya SIMBA TRUST ni mbia. Anazalisha umeme wa TEGETA na kumiliki vitalu vitau vya gesi Mtwara - Mnazi Bay. Apewe muda zaidi, naunga mkono!
 
Ama kwa hakika milembe wanakwenda watu wenye akili zao..huku machizi tunaachiwa mitaani.....cha ajabu unaweza kuta huyu ni baba wa familia na anategemewa kwa ushauri kama kichwa familia....hasara...
 
Katika uongozi wa Jk kafanya yafuatayo,
1. uongozi wake wanawake wajawazito na waliojifungua kulala kitanda kimoja 4 imebaki historia, mahospitali yetu yanatoa huduma nzuri tena za kuvutia na madawa yapo ya kutosha.
2.Kapunguza deni la Taifa kiasi kwamba bado tuna uwezo wa kukopesheka.
3.Rais wetu kashinda angani akitutafutia watanzania tukimuongeza miaka ataenda nchi nyingi na Tanzania itakuwa nchi ya neema kwa misaada.
4.Rais ana uchungu na nchi ndo maana hataki kuwabugudhi wawekezaji hata kama wakituibia kwani kwa kufanya hivyo kutazuia wawekezaji kuja kuwekeza.
5. Rais wetu amesaidia kurejeshwa kwa pesa EPa zilizokuwa zimeibiwa na akatumia ubinadamu kuwasamehe wezi wale.
6.Ajira kwa vijana zimeongezeka ndo maana zikitangazwa ajira watu hawaendi wengi matokeo yake huchukuliwa watoto wa wakubwa na kuwekwa kwenye nafasi zile maana watoto wa walalahoi hupata ajira pindi wamalizapo masomo.
7.Kila kijana achaguliwaye kwenda elimu ya juu hupata mkopo hata wale 23000 waliokuwa wanasemwa ni chuki za wapinzani kuichafua serikali.
8.Kipindi cha utawala wake kila mtanzania amekuwa na maisha bora na hii hudhihirishwa na foleni za magari Dar.
9.Mikataba yote kipindi cha imekuwa ya wazi isiyokuwa na chembe ya ubadhirifu hata kidogo.
10.Ukisikia Escrow hizo ni chuki za watu wenye kutaka vitalu vya gesi kwani pesa zile si umma lakini amemsimamisha Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini ili kuridhisha bunge
Kwa haya mazuri napendekeza tumuongezee miaka 5 ili amalizie viporo vya kazi yake vilivyobaki.
Akapime kwanza Tezi Dume!!!
 
Kwanza hiyo miezi 10 iliyobaki utadhani ndio uchaguzi umeisha jana halafu ana mihula 2 kaanza muhula 1 jana tar 01-01-2015! Kwa jinsi utawala wake ulivyonichosha natamani ang'atuke tuingie kwenye uchaguzi sasa badala ya kusubiri hiyo Octoba! Au kama vipi nchi wakabidhiwe wale jamaa wa mabakamabaka yaliyoiva yanayofanana na misitu a.k.a JWTZ hawa jamaa ni wazalendo sana! Jeshi la Polisi livunjwe liundwe upya kwasababu limekuwa ni la CCM! Kitengo cha usalama wa Taifa(TISS) kivunjwe kwakuwa Usalama wa Taifa umekuwa ni usalama wa CCM na mali zao!
 
Ama kwa hakika milembe wanakwenda watu wenye akili zao..huku machizi tunaachiwa mitaani.....cha ajabu unaweza kuta huyu ni baba wa familia na anategemewa kwa ushauri kama kichwa familia....hasara...

Mkuu jamaa ukimsoma vizuri unaweza kumuelewa. Kwa maoni yangu huyu ni jamaa ni smarter than we think. Unachotakiwa kufanya elewa kinyume cha aliyoandika. That is the message he is sending.
 
Kwa hoja tu za uzi ulivyo anatakiwa kuitisha uchaguzi mapema maana ametwaribia uchumi na maisha ya watu wengi yamekuwa chini katika kipindi chote cha utawala wake.
Sasa hivi mtu akipata laki tano matumizi yake ni sawa na hamsini elfu.
Utasema maisha bora haya kweli.
 
Back
Top Bottom