Katika uongozi wa Jk kafanya yafuatayo,
1. uongozi wake wanawake wajawazito na waliojifungua kulala kitanda kimoja 4 imebaki historia, mahospitali yetu yanatoa huduma nzuri tena za kuvutia na madawa yapo ya kutosha.
2.Kapunguza deni la Taifa kiasi kwamba bado tuna uwezo wa kukopesheka.
3.Rais wetu kashinda angani akitutafutia watanzania tukimuongeza miaka ataenda nchi nyingi na Tanzania itakuwa nchi ya neema kwa misaada.
4.Rais ana uchungu na nchi ndo maana hataki kuwabugudhi wawekezaji hata kama wakituibia kwani kwa kufanya hivyo kutazuia wawekezaji kuja kuwekeza.
5. Rais wetu amesaidia kurejeshwa kwa pesa EPa zilizokuwa zimeibiwa na akatumia ubinadamu kuwasamehe wezi wale.
6.Ajira kwa vijana zimeongezeka ndo maana zikitangazwa ajira watu hawaendi wengi matokeo yake huchukuliwa watoto wa wakubwa na kuwekwa kwenye nafasi zile maana watoto wa walalahoi hupata ajira pindi wamalizapo masomo.
7.Kila kijana achaguliwaye kwenda elimu ya juu hupata mkopo hata wale 23000 waliokuwa wanasemwa ni chuki za wapinzani kuichafua serikali.
8.Kipindi cha utawala wake kila mtanzania amekuwa na maisha bora na hii hudhihirishwa na foleni za magari Dar.
9.Mikataba yote kipindi cha imekuwa ya wazi isiyokuwa na chembe ya ubadhirifu hata kidogo.
10.Ukisikia Escrow hizo ni chuki za watu wenye kutaka vitalu vya gesi kwani pesa zile si umma lakini amemsimamisha Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini ili kuridhisha bunge
Kwa haya mazuri napendekeza tumuongezee miaka 5 ili amalizie viporo vya kazi yake vilivyobaki.