Napendekeza: Tubadilishe Muundo wa Serikali za Mitaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza: Tubadilishe Muundo wa Serikali za Mitaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by UmkhontoweSizwe, May 15, 2011.

 1. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hoja yangu inalenga hasa kwa maeneo ya mjini ambako ndo kuna kizungumkuti katika uendeshaji wa halmashauri za miji.

  Pendekezo langu ni kwamba tupunguze maeneo ya halmashauri za miji.
  Mfano: 1. Badala ya Jiji kama Dar kuwa halmshauri za miji tatu tu (Ilala, Temeke na Kinondoni), kuwe na serikali za miji nyingi. Iwe ni miji inayojitegemea na kujiendesha yenyewe.

  Nionavyo: Dar sasa hivi ingekuwa na Serikali za miji siyo chini ya 6, (eg. Kigamboni, Mbagala, City Center, Magomeni, Ubungo/Kimara, Sinza/Mlimani/Mikocheni, Kinondoni/Mwananyamala/Msasani, Kipawa/Ukonga/Yombo, nk – wengine mnaweza kunisaidia mgawanyo). Hii inatokana na kupanuka kwa eneo la mji na ongezeko la idadi ya watu.

  2. Jiji la Mwanza (2nd largest) lingekuwa na miji km 4 hivi, city center/mabatini, Buzuruga/Nyakato/Mahina, Igoma, Pasiansi/Nyamanoro/Bwiru, Igogo/Butimba, nk.

  Faida:
  1. Itazipunguzia halmashauri za wilaya ukubwa wa maeneo ya kuhudumia na mzigo wa huduma yenyewe.

  2. Tutasogeza huduma karibu zaidi na wananchi, tofauti na ilivyo sasa ambapo halmashauri za miji zinahudumia maeneo makubwa na matokeo yake ufanisi unakuwa kiduchu sana, kama siyo hakuna kabisa.

  3. Tutasogeza kwa wananchi vikao vya maaamuzi. Wananchi watachagua viongozi wao wa miji na kufanya maamuzi yatakayoendana na mazingira na utashi wao. Viongozi wataochaguliwa watawajibika kwa wananchi moja kwa moja.

  4. Tuasogeza karibu zaidi kwa wananchi upangaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya maendeleo, tofauti na sasa hivi ambapo uamuzi unafanywa wilayani na wananchi kubaki km watazamaji tu.

  5. Tutaongeza ajira. Badala ya kuhudumiwa na kundi dogo la watu wa wilayani, kila mji utakaoanzishwa utaajiri wataalam wake, kwa hiyo watu wengi wataajiriwa.

  6. Itasaidia kuweka suala la maendeleo mikononi mwa wananchi wenyewe badala ya kutegemea serikali kuu.

  7. Kwa kuwa mwenye kisu kikali ndiye hula nyama, miji itakayoboresha huduma kwa wananchi ndo itakayovutia uwekezaji zaidi na hivyo kupata makusanyo zaidi ya kodi na hivyo kuwa na mapato zaidi.

  Hili ni wazo ghafi. Wenajamvi mnasemaje? Na wataalam wa mipango miji mnasemaje?

  Jumapili njema.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Yaani..... sijui tuna undugu!!! I second THAT! Ya kwangu ilikuwe iwe "Jiji la Dar livunjwevunjwe".. thanks. Ila mimi nilitaka kwenda mbele zaidi na kuivunja serikali kuu kwenye mambo fulani fulani. Sielewi kwa mfano kwanini tuna Jeshi Moja la Polisi utadhani utawala wa Kikoloni!
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yes!

  Wazo hili limekuja wakati muafaka. Ukweli ni kwamba sio tu utoaji wa huduma umekuwa dhaifu bali hata masuala yanayohusu ustawi wa jamii katika maeneo yao ya makazi limekuwa ni jambo la kusikitisha na kulifikisha taifa kwenywe aibu ya ajabu.

  Utaratibu wa kuzigawanya Halmashauri za miji ni suala la msingi kwa maana ya udhibiti wa rasilimali, na kushughulikia vipaumbele vya wakazi papo kwa papo "locally addressed priorities".

  Hivi sasa kwa mfano watu wanakaa ofisi ya Kinindoni Manispaa kule Magomeni, na kutoa maagizo ya utekelezaji kwa wakazi wa maeneo yaliyo mbali nao, kupitia uwakilishi hafifu na taarifa zinazochujwa ili kukidhi maslahi ya watu fulani!

  Najaribu kuchangia machache kwa sasa kwa uelewa nilio nao wa Halmashauri zetu.
  Tatizo la mfumo tulilo nalo linatokana na mambo mawili makubwa:

  1. linaendana na dhana ya ukiritimba uliokuwa ndio mfumo kwa miaka mingi: maamuzi- vikao vya juu; maagizo - vikao vya juu; maelekezo - vikao vya juu; Kwa hiyo hii centralised system inafanya kazi kulinda maslahi ya kisiasa ya watu ambao kwao utawala ni muhimu kuliko kutumikia watu waliowapa kura. This is typical one party system hangover!

  2. Rasilimali: Halamashauri zetu zinakusanya mapato yake nayo si haba. Lakini ukusanyaji huu umewekewa ukiritimba wa ajabu na matumizi yake yana urasimu unaotia kichefu chefu kwani pamoja na viongozi wa Halmashauri zetu kuimba kwenye majukwaa na vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya ukusanyaji mapato haingii akilini mafanikio hayo yanamgusaje mlipa kodi na mwananchi mwenye haki ya kupata huduma bora.

  Hawa watu hawtaki kuachia rasilimali zisimamiwe na ngazi zilizo karibu na wananchi! Ingawa ukweli ni muwa utaratibu mzuri ukiwepo zitasimamiwa vema kwa mujibu wa sheria na kanuni wakiwepo watekelezji wenye uelewa na usmamizi thabiti wa serikali mitaa

  Pendekezo: Hoja hii ni ya msingi na ingefaa sana kuivalia njuga tuondokane na ubwanyenye wa ukiritimba.

  Njia mojawapo ni kupata ushirikiano wa Wah. Wabunge na kama kweli wapo wanaoitakia mema nchi hii naamini itapewa kipaumbele stahili.

  Thanks for this opener, na ni tumaini la wengi kuwa litafanyiwa kazi kupitia maoni na michango ya wanajamvi

   
 4. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ndugu umetoa wazo zuri sana.

  Ila wazo langu lilikuwa ni kuzipa nguvu kubwa serikali za mitaa (maana zipo jirani na wananchi) badala ya halmashauri za jiji na manispaa na mawizara kwa kufanya yafuatayo

  1. kuwepo na viongozi watendaji wengi katika ngazi ya kata na mtaa (mf. afisa ardhi, afya, kilimo, ustawi wa jamii nk) kushughulikia kero za wananchi. sasa hivi kuna mtendaji ambaye hawezi kushughulikia shida zote mtaani

  2. kuchagua viongozi wenye uwezo mkubwa katika level ya mtaa na kata (shule & experience katika kutatua matatizo mbalimbali) na walipwe vizuri badala ya sasa kuwajaza mawizarani na kwenye halmashauri

  Hii itasaidia kupunguza usumbufu wa kufuata masuluhisho ya kero katika halmashauri na wizara
   
 5. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Weka basi na details ili tuunganishe nguvu. Thanks
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kibunango, Gaijin et al... where you at??!
   
 7. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi sikubaliani na hoja hiyo, kwa kuwa hiyo itakuwa ni vurugu kubwa, kwa kuwa mpaka sasa hata hizo halmashauri zilizopo tena hata zile ndogo ndogo tu hazijaonyesha faida yoyote zaidi ya kuwa shimo la kutupia fedha zetu.

  Halmashauri nyingi kama sio zote ni wezi wakubwa wa fedha za umma, sasa tukifanya hivyo tutakuwa tunazidi kuongeza walaji wa fedha zetu. Kinachotakiwa sasa hivi ni kubuni mbinu za kuwadhibiti hawa halmashauri waliopo kuacha wizi na kuhakikisha kwamba miradi mingi ya maendeleo iwe inabuniwa na kusimamiwa na watu kutoka maeneo husika, halmashauri wawe wawezeshaji tu (ku-finance).

  Hii inatokana na ukweli kwamba halmashauri zimekuwa zinabuni miradi mingi ambayo haendani na mahitaji ya watu kwa lengo la kuiba fedha tu, unakuta halmashauri inaamua kuchonga barabara sehemu bila kuweka kifusi, na kama ikiweka kifusi wanarashia tu, na kama wasiporashia hawaweki mifereji ya kutolea maji ya mvua hivyo barabara inaharibika kwa muda mfupi, lengo lao ni kuendelea kupeana tenda kila siku kwenye barabara moja tu, hapo maendeleo yatapatikana vipi?
   
 8. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mwanakatwe,
  Nadhani hujaona kwamba hizi ulizoziita vurugu tulizonzo zinzsababishwa na mfumo mbovu tulionao. Tatizo lililopo kwenye mfumo wa halmashauri kwa sasa ni kukosa accountability. Hizo halmashauri ziko accountable kwa nani? Huwezi kusema kuwa ziko accountable kwa wananchi maana wananchi hawana say yoyote kwenye maamuzi ya halmashauri. Kama ulivyosema kuwa halmashauri nyingi zinabuni miradi mingi ambayo haiendani na mahitaji wala matakwa ya watu, matokeo yake ndo haya tunayoyashuhudia - vurugu mechi. Muundo wa sasa unawapa hao walio kwenye halmashauri kujiamulia vyovyote watakavyo bila mtu wa kuwawajibisha.
  Naomba usome tena faida #3. Tukipunguza maeneo tutasogeza vikao vya maamuzi kwa wananchi na itazifanya serikali za miji itakayoundwa kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Nafikiri wengi wetu wananchi kwanza hatujui mipaka ya majukumu ya ngazi mbali mbali kwenye mfumo huo uliopo sasa.

  Nini kazi, majukumu, mipaka ya

  Serikali za mitaa
  Manispaa
  Halmashauri ya jiji
  Wilaya
  Mkoa

  Kimsingi mfumo uliopo sasa hauonekani kushirikisha wananchi vya kutosha kwenye masuala yanayohusiana na jamii yao. Manispaa zilizopo ni kubwa na inaonekana wananchi wanashindwa kushiriki kwenye masuala yanayohusu mazingira na ujenzi labda iwapo yanatokea eneo la mbali na wanapoishi.

  Lakini ziadi ya hapa kuna tatizo la uwajibikaji. Hata tukiunda manispaa ndogo ndogo zaidi, hazitakuwa na manufaa iwapo uwajibikaji wake utaendelea kuwa kama huu ulipo au wananchi tutashindwa kuwa aware na wajibu na haki zetu kwa manispaa hizo
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi nasikitishwa sana na viongozi wetu wa kuchaguliwa maana nao akili yao iko zaidi kwenye pesa kuliko hata kutoa mwongozo kwa wananchi.

  Mathalani mitaa yetu ni michafu na barabara nyingi za mitaa ni mashimo ntu na watu wanaoishi maeneo hayo siyo kwamba hawawezi kufanya huo usafi au kurekebisha hizo barabara, bali hakuna mtu wa kuwa organise kufanya hivyo vitu.

  Kuna sehemu kama Tegeta ambayo ni chafu kupindukia, haina utaratibu wa kuzoa takataka mpaka leo watu wanaishi na taka zao nyumbani ili hali ni uswahilini. Hapa watu wako tayari kulipia uzoaji wa taka majumbani kwao lakini hakuna kiongozi wa kulifatilia jambo hili.

  Mbunge wetu Mdee anajua kabisa serikali haiwezi kumpa hela ya kuindeleza Kawe,ila anashindwa kujua kuwa anaweza kutumia nguvu ya wanannchi wake kufanya mambo mengi tu pasipo hata kuhitaji hiyo hela ya serikali.

  Watu wanahitaji uongozi tu watatoa fedha zao kufanya vitu ambavyo vinafaida kwao.

  Kama Mdee yuko JF afike Tegeta afanye mkutano na wananchi ili kuangalia namana ya kuondokana na kero ya uchafu iliyopo sasa. Tunahitaji uongozi zaidi kuliko pesa na wala Mbunge asiumize kichwa kutafuta pesa akapoteza muda mwingi badala ya kukaa karibu zaidi na wananchi na kuwapa mwelekeo wa kujiletea maendeleo kwa kutumia kidogo walichonancho.

  Mdee asipofanya hivyo hatakuwa na kitu chochote cha kujivunia katika jimbo lake maana anajua fika serikali haiwezi kumpa fedha za kuleta maendeleo na hilo wananchi tunalijua ila tunamtaka yeye kutumia uongozi zaidi kuwaelekeza wananchi wafanye nini ili kuondokana na kero zao.
   
 11. k

  katitu JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  \Ni vizuri labda ungetuambia katika kugawa maeneo kama hayo kwa kupunguza majiji na kuongeza miji labda mwenzetu umeangalia swala la kiuchumi yaani hiyo miji itaweza kujimudu kimapato,yaani (viability),swala la ukusanyaji mapato litakuwaje pamoja na mambo mengine.
   
 12. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu nadhani ungetupa data zaidi!
  Binafsi, kuna vitu vimekuwa vinanitatiza na huwa najiuliza kama kwa mfano kuna Mhandisi wa wilaya kwanini asiwepo Mhandisi wa mtaa?
  Nadhani kwa hoja iliyopo mezani inawazo kama langu, kupeleka mamlaka mtaani kwa WATU!
  Hii itakuwa ina maana kubwa sana kwenye maendeleo na nadhani WATU watasimamia maendeleo yao wenyewe na kwa dhati.
  MMM natamani utupe zaidi hapo kwenye jeshi la polisi umenifurahisha sana, na natamani nisikie muundo mbadala.
  Nadhani tunapozungumzia Tanzania mpya tunazungumzia mfumo unaoendana na huu, bila aina ya namna hi ya mfumo ambapo WATU wataamua maendeleo yao wenyewe basi tutakuwa hatujabadili kitu.
  Binafsi siasa za hii nchi nilianza kuziangalia kwa jicho mvuto zaidi pale mwaka 2005, ambapo kuna mgombea urais alikuja na hoja za kujenga aina hizi za serikali za UMMA.
  Hahahaha sikuwa kwenye mkumbo wa wale 80%, so kumbe sikushindwa sababu naona bado hiyo ndio njia pekee kuelekea TANZANIA MPYA TUNAYOITAKA.
  SERIKALI ZA UMMA (MTAA/VIJIJI)
  Ila plz Mwanakijiji fafanua zaidi.
   
 13. k

  katitu JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Sioni kama tatizo ni mfumo sababu wananchi wanawakilishwa na madiwani ambao huchaguliwa na wananchi wenyewe.Mimi naona tatizo ni elimu ya uraia kwa wananchi hao.Je wanajua wanaowachagua kama ni wawakilishi wao.Je wanaowachagua wana sifa za kuwawakilisha?Wanafahamu kuwa wao ndio wanaopaswa kuwaadibisha wanapoenda kinyume na matakwa yao,Na je wanapowachagua wanaangalia sifa za viongozi hao au wanafuata ushabiki wa kisiasa tu bila kujali kama watalinda maslahi yao?Si tanzania pekee inayofuata mfumo huo.Je umefanya tafiti kuwa nchi nyingine zinazofuata mfumo huu zina matatizo kama yetu ya Tanzania?
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Kama alivyosema katitu suala la vyanzo vya mapato litaleta shida sana na sijui kama baadhi ya miji itaweza kujiendesha.
  Kwa upande mwingine kitendo cha madiwani kukaa kikao na kuanza kujadili mambo ya mitaa isiyowahusu pia kinatia shaka.
  Mimi nadhani tatizo lilipo ni kutokuwepo kwa mgawanyo mzuri unaofahamika wa madaraka. Kazi za kiwilaya chini ya mkuu wa wilaya zinaingiliana na za halmashauri za manispaa na hii ina polarize shughuli. Kama hakuna ulaji ni kutupiana mpira tu.

  Inawezekana kama makusanyo yatafanywa na halmashauri lakini mafungu yapelekwe kwa hiyo miji ili madiwani na viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wananchi waamue nini wanataka. Kama 'mji wa sinza' utaamua kujenga barabara hiyo iwe juu yao, kama 'mji wa magomeni' wataamua kujenga mifereji ya maji machafu hiyo iwe juu yao. Kazi ya madiwani katika halmashauri ziwe kuwakilisha mipango, kugawa mapato, lakini mipango na matumizi ya fedha hizo yatoke kwa wananchi wa sehemu husika.
  Nadhani hii itasaidia wananchi kupanga mipango yao badala ya kuwasubiri madiwani waende kusinzia ndani ya vikao vya halmashauri na kushindwa hata kutoa majina ya mitaa. Kwa maneno mengine itamfanya diwani awajibike kwa watu wake moja kwa moja bila kisingizio.

  Ni mtazamo tu.
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145

  Mkuu GJ.
  Nadhani wazo la serikali za watu anazozizungumzia UmkhontoweSizwe hujazielewa tu.
  Kadiri tunavyoendelea na huu mjadala utapata picha.
  Kwa njia hii, huo ubadhirifu hautakuwa na nafasi kabisa sababu kubwa ni kwamba watendaji wakuu wa hizo "halmashauri" watachaguliwa na watu na watawajibika kwa watu wa huo mji/mtaa/kijiji.
  Hapo kutakuwa na utolewaji wa ripoti wa mapato na matumizi kwenye vikao rasmi ambapo wakazi wote ni wajumbe (mf mkutano mkuu wa kijiji unaofanyika mara 4 kwa mwaka)
  Pia sababu hizi halmashauri zitakuwa zitumikia eneo dogo sana ukilinganisha na mfumo wa sasa. Naamini kila kitu kina mapungufu yake lakini huwezi linganisha na hali ya sasa.
  Kikubwa kwenye wazo hili ni kwamba kila mwananchi anakuwa na taarifa za maendeleo ya eneo lake, afu hii itaondoa watu kumtegemea Rais na ahadi zake "bajaji", sababu maisha ya watu na shughuri zao za kila siku ni suala la wao na serikali yao ya mtaa/mji/kijiji, serikali kuu ni kusimamia mamlaka kuu ya nchi na mambo makuu kama uhusiano wa kimataifa, jeshi nk.
  Kwa mfumo huu ni rahisi kusimami matokeo.
   
 16. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hii direction! Nadhani pamoja na kuendeleza harakati katika mtindo wa kijukwaa kama ambavyo imezoeleka katika jamvi la siasa,harakati za mrengo huu zinaweza kututoa sana! Asante wakuu!
  Mie mtizamo wangu upo namna hii: Hivi tujiulize kwanza je inefficiency ya muundo uliopo sasa unatokana na TU kwamba maeneo ya halmashauri yamekua makubwa sana? Nadhani pamoja na hilo kuna jingine. Serikali hizi zipo MBALI sana na wanachi. Si umbali physical,hapana! Lakini ni umbali wa kimaamuzi unaotokana na uwakilishi hafifu unaofanya mwananchi aone halmshauri ya manispaa au wilaya haina tofauti na makao makuu ya wizara fulani. Haoni kuhusika kwake moja kwa moja na barabara inayopita hapo mtaani kwake wala dampo lililoanzishwa nyuma ya nyumba yake. Hamjui anaekusanya kodi hapo sokoni na baa ya jirani zaidi ya kelele usiku kucha. Na hata akijua,hawezi kufahamu makusanyo yanapelekwa wapi,ili iweje!
  Serikali zipo mbali sana! Lakini je,tukiwa na halmashauri ya Sinza,Ubungo n.k, itazifanya ziwe jirani? Tuvunje kwanza halmashauri ya manispaa ya Kinondoni au tuangalie kwanza ni kwa vipi,mkazi wa tandale atajiskia kuhusika zaidi na halmashauri ya sinza kuliko hii ya kinondoni ambayo makao yake yapo hapo magomeni,a walking distance perharps.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  May 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mchango mzuri Mshindo na maswali mazito yenye kufikirisha.
  Wananchi wapo tayari kuchangia maendeleo yao, tatizo ni utaratibu wa nchi ambapo sekta ya utumishi haina mpangilio. Haijulikani mipaka na majukumu ya viongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa. Ukiangalia vizuri wakuu wa wilaya wamekuwa ni kikwazo kwani utendaji wao ni wa urasimu sana. Kwa upande mwingine viongozi wa kuchaguliwa kama wabunge/madiwani/serikali za mitaa hawajui majukumu yao hasa kuwashirikisha wananchi,wanadhani wapo kwa vikao vya halmashauri na maamuzi hata kama hayahusu maeneo yao. Shughuli au mipango ya maendeleo, haijulikani ni nani anahusika na wala mapato au matumizi yanakwenda wapi.

  Mpango wa kuwa na vimiji inawezekana kuleta ukaribu na wananchi. Viongozi kama madiwani na watendaji wengine ni lazima kwanza wawajibike katika maeneo yao kwa vitendo. Njia ya kuwabana ni kuhakikisha wanajua eneo lao la uwakilishi, watu wanaowawakilisha na vyanzo vya mapato. Hii itawalazimisha wapewe fungu kutokana na jinsi wanavochangia. Mathalani, kama sinza ina watu milioni moja na makusanyo ni milioni 5 basi wapewe 1/3 ya makusanyo. Kama magomeni ni watu laki 5 na makusanyo ni milioni 10 wapewe 1/3. Mfano huu ni wa kuwawajibisha viongozi na kuleta tija kwa wanaojishughulisha.

  Lakini pia lazima twende mbali na kufikiria huduma za jamii, kwamba itakapotokea kuna uzembe iwe ardhi, elimu au afya basi viongozi husika wa vimiji wawajibishwe na watu wao bila kuingiliwa. Nitoe mfano, kama kuna mitaro haifanyi kazi wahusika wabanwe na wananchi papo hapo, lakini pia wahusika wawabane wananchi kutokana na uzembe huo, ikitegmea nani atawahi mwingine(tit for tat).

  Kule kwetu kuna kitu kinaitwa msaragambo(volunteerism). Kijiji kikiamua kujenga shule basi watu wote watashirikishwa,lakini balozi wa nyumba kumi aliogopwa sana. Yeye alipewa privelege fulani siku za kazi, lakini wajibu wake ulikuwa ni kuwafahamisha 'nyumba kumi' mipango iliyoamuliwa utekelezaji na ushiriki, hii ilimgusa pia mtendaji kata na kiongozi wa mtaa hadi juu.
  Viongozi hawa tuliwabana na walitubana hata sisi watoto wao kwa vile ujenzi ulipangwa kwa nyumba kumi,mtaa n.k
  Kwa mwendo huo tumepiga hatua sana katika nyanja za elimu,afya na huduma za jamii kuliko mikoa mingi licha ya rasilimali zetu chache sana na uhaba mkubwa wa ardhi.

  Kuleta uongozi na maamuzi karibu na wananchi ni kitu kinaitwa 'quid pro quo' yaani kiongozi anachukua nini na analeta nini. Siamini kujenga ofisi karibu na wananchi ndio kusogeza huduma na ushirikishaji. Nina amini tatizo letu ni kutokuwa na mgawanyo mzuri wa madaraka na majukumu, pili kutokuwa na mechanism ya kuwawajisha viongozi kwa wananchi. Tukifanikiwa kuwabana viongozi waelewe wapo kwa ajili yetu kuanzia ngazi za chini na vimiji vidogo tunaweza piga hatua.
   
Loading...