Napendekeza route mpya Mbezi Luis - Bunju

Napendekeza route mpya Mbezi Luis - Bunju

Ruti ndefu zaid zipo sema huku kwetu bunju tume kosa wawekezaji,,
K,koo via buguruni + chanika 750
Chanika via g ,mboto +kinyerezi +mbezi 750
Mbagala via vikindu + mkulanga 1000
Bagamoyo via magereza,miembe saba,matimbwa+mlandizi 2000

Wenye magari iwe dala dala
Au private car vipi hii ruti ya bunju -+ mbezi luiis
 
Wadau natumaini kuwa ni wazima wa afya.

Kituo cha daladala Mbezi-Luis ni katika vituo vikubwa vinavyounganisha maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam.

Cha kushangaza hakuna daladala za moja kwa moja Mbezi Luis-Bunju, hali inayowapa ugumu wakazi wa Kunduchi, Mbezi Beach, Tegeta na Bunju kuwafanya waunganishe magari hivyo nauli kuwa kubwa na usumbufu kuongezeka.

Napendekeza kuanzishwa kwa route hii mpya.
Hii inatokana na kukosekana ushirikishwaji wa wananchi kwenye kutoa mapendekezo, wengi wa watoa maamuzi hawatumii public transport, wana magari yao binafsi, kwahiyo hawaoni hizo adha, niliwahi kumsikia kigogo mmoja akishupalia kujengwa kwa shule karibu na eneo analoishi, kumbe mkewe ni Mwl anafundisha mbali.
 
Hata kama iko sawa kwa umbali na Mbezi - Mlandizi?
Ruti yoyote inayolipa mabasi yenyewe yanaenda omba,
Sema utata unakujaga bei elekezi ya nauli.

Kwa jiji dsm nauli kubwa kwa ruti ni 750 ndogo 400
So sidhani kama urefu ukiwa sawa nauli itakuwa sawa! ( kwa fact ya wale wa mlandizi wanatoka kwenda mkoa mwingine).
 
Ruti yoyote inayolipa mabasi yenyewe yanaenda omba,
Sema utata unakujaga bei elekezi ya nauli.

Kwa jiji dsm nauli kubwa kwa ruti ni 750 ndogo 400
So sidhani kama urefu ukiwa sawa nauli itakuwa sawa! ( kwa fact ya wale wa mlandizi wanatoka kwenda mkoa mwingine).

Kuna tofauti gani kwa ruti ya Mbeziluis-Makumbusho via goba na Mbeziluis-Tegeta via goba
 
Ndani ya Dar haitakiwi kufika 900 ndo maana wanazikacha hizi route. Fikiria jamaa waliomba Mbagala Rangi Tatu to Tegeta Kwa 1300 mamlaka ikakataa na ilipendekeza sh 900.
 
Mbunge yupo kinyume na baadhi ya maelekezo ya m/kiti wa chama: hela za lami zinaeza chelewa
Hapa najaribu kuwaza kwa sauti
 
Pia route ya pugu mnadani kwenye mbezi kupitia malamba mawili pasipo kulazimika upitie majumba sita.
 
Ikikamilika stend ya Mwenge nadhani magari mengi yanayotokea bunju yataishia hapo,
Ndipo yataanzia hapo Mwenge kwenda mjini, kwenda Luis nk.

Lakini Kama Jambo la maana ambalo mamlaka ingelifanya Ni Bunju b kupitia mabwepande hi ingekua rahisi hata kwa Basi zinazoenda kaskazini na pia bagamoyo na mbezi Luis, kwa urahisi wa wanatoka mikoani kuja bagamoyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tegeta nyuki to Mbezi luis ni route ya muhimu sana.
Wahusika wafanye hima barabara iko na lami tayari watoe maelekezo haraka.
 
Back
Top Bottom