Napendekeza Baraza lijalo la Mawaziri, Sanaa na Michezo zingekuwa Wizara 2 tofauti

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu Joseph

Leo Juni 16, 2020 Rais Magufuli alizungumza Bungeni jijini Dodoma, kulivunja Bunge kama wanavyosema Wataalam, amezungunza mambo mengi sana, Ikiwemo Uchaguzi, Siasa, Uchumi, Sanaa, Elimu, natamani sana kuandika kuhusu vyote hivyo, lkn Leo nianze kwa kimoja cha Sanaa.

Katika Hotuba Rais Magufuli amezungunza juu ya kukua kwa Kasi Kwa sekta ya Sanaa nchini ambapo alisema ni Moja ya sekta 3 zinazokua kwa Kasi ipo.

Katika Hotuba Mh. Rais ameijumuisha Sanaa, Michezo kama kitu kimoja na kueleza imekua Kwa zaidi ya asilimia 11 means kama imekua kwa kasi hata kwenye Uchangiaji wa Pato la Taifa umeongezeka Safi sana

So tuje kwenye hoja yangu Nakubaliana na Rais Magufuli kuwa Sanaa inakua Kwa haraka lakini Kwa nidhaniavyo Mimi wanaoikuza Sekta ya Sanaa na Michezo ni Mashabiki wa Sanaa na Michezo ila si Wasanii na Wanamichezo husika.

Ukiangalia kwa kuanzia 2018/2019 - 2019/2020 unaweza kujiuliza ni Wasanii wangapi wapya walioingia kwenye game ya Sanaa ( BongoFleva), Wasanii wangapi wamepata Endorsement, na je uzalishaji wa Wasanii wapya kwenye Industry upoje utakuja kugundua wanaoifanya Sekta ya Sanaa ikue Kwa kasi ni Wasanii wachache ambao wanahesabika na wanamakundi makubwa ya mashabiki, kwa maana hiyo kwenye Sanaa ni rahisi kupata shabiki mpya kuliko Msanii mpya.

Kwenye Michezo Kwa kiasi Fulani inafanana na Sanaa (BongoFleva) ni Mashabiki wanaoikuza Sekta ni rahisi kupata Shabiki mpya wa Azam, Mtibwa, Ruvu Shooting kuliko kupata Mchezaji wa anayefanya vizuri zaidi kwenye hizo Timu kuliko Mchezaji wa Simba au Yanga hapa pia tatizo ni Nani mashabiki au Wachezaji.?

Mwisho kabisa namuomba na kupendekeza kwa Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi, kwenye Baraza lijalo la Mawaziri Sanaa na Michezo vingekua Wizara 2 tofauti kama ambavyo tuligawanya Nishati na Madini na Leo hii tunafurahia matunda ya kutokatika kwa Umeme, na ongezeko la Makusanyo ya mapato yanayotokana Madini

Instagram : FB : Twitt : SanguJoseph

#KijanaMzalendo
 
Back
Top Bottom