Serikali yasisitiza kuedeleza sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na mchango wake kitaifa na kimataifa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SERIKALI YASISITIZA KUEDELEZA SEKTA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUTOKANA NA MCHANGO WAKE KITAIFA NA KIMATAIFA.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia na kuendeleza sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na umuhimu na mchango wake katika maendeleo ya nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja.

Amesema sekta hizo zina nguvu kubwa ya ushawishi, uhamasishaji na ustawishaji wa jamii na maendeleo ya nchi kupitia ajira, utalii, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, mtangamano baina ya nchi na nchi kupitia diplomasia.

Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika leo Machi, 30, 2023 jijini Dar es Salaam.

“Kipekee kabisa namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Sekta za Wizara. Katika uongozi wake kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo” Amesema.

Amesema Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zinajulikana kama nguvu laini hapa nchini na zimekuwa na mvuto mkubwa kwa makundi mbalimbali ya jamii hususan vijana ambao ndio wanaunda sehemu kubwa ya nguvu kazi ya nchi.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeelza kuwa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa ya mwaka 2021 inaonesha kuwa Sekta ya Sanaa na burudani iliongoza kwa ukuaji wa wastani wa asilimia 19.4 na mchango wake katika uchumi wa asilimia 0.3.

Amesisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandaa Mkakati wa Maendeleo ya Michezo na kuendelea kufanya mapitio ya Sera, Sheria zinazosimamia Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo pia inaendelea na ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya michezo.

Aidha, amesema Sekta Binafsi imekua na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya michezo, ufadhili wa Timu za mpira wa miguu kwa upande wa wanawake na wanaume, ufadhili wa Ligi Kuu ya Tanzania, ujenzi wa miundombinu na uendelezaji wa vipaji vya Sanaa na Utamaduni.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Othman Yakubu akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imekua na mchango mkubwa katika kukuza ajira na Pato la Taifa hapa nchini kwa kuwa ni Sekta inayoshughulika na Watanzania wote.

Ameeleza kuwa baadhi ya nchi Sekta hizo ndizo zinazopewa kipaumbele kutokana na mchango wake katika uchumi akibainisha kuwa baadhi ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini zimetoa kipaumbele kikubwa kwenye eneo la Ubunifu.

IMG-20230330-WA0874.jpg
IMG-20230330-WA0872.jpg
 
Attachments

  • IMG-20230330-WA0867.jpg
    IMG-20230330-WA0867.jpg
    164.5 KB · Views: 1
  • IMG-20230330-WA0871.jpg
    IMG-20230330-WA0871.jpg
    196.2 KB · Views: 1
  • IMG-20230330-WA0870.jpg
    IMG-20230330-WA0870.jpg
    202.1 KB · Views: 1
  • IMG-20230330-WA0868.jpg
    IMG-20230330-WA0868.jpg
    176.3 KB · Views: 1
  • IMG-20230330-WA0869.jpg
    IMG-20230330-WA0869.jpg
    164.4 KB · Views: 1
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia na kuendeleza sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na umuhimu na mchango wake katika maendeleo ya nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja.

Amesema sekta hizo zina nguvu kubwa ya ushawishi, uhamasishaji na ustawishaji wa jamii na maendeleo ya nchi kupitia ajira, utalii, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, mtangamano baina ya nchi na nchi kupitia diplomasia.

Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika leo Machi, 30, 2023 jijini Dar es Salaam.

“Kipekee kabisa namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Sekta za Wizara. Katika uongozi wake kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo” Amesema.

Amesema Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zinajulikana kama nguvu laini hapa nchini na zimekuwa na mvuto mkubwa kwa makundi mbalimbali ya jamii hususan vijana ambao ndio wanaunda sehemu kubwa ya nguvu kazi ya nchi.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeelza kuwa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa ya mwaka 2021 inaonesha kuwa Sekta ya Sanaa na burudani iliongoza kwa ukuaji wa wastani wa asilimia 19.4 na mchango wake katika uchumi wa asilimia 0.3.

Amesisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandaa Mkakati wa Maendeleo ya Michezo na kuendelea kufanya mapitio ya Sera, Sheria zinazosimamia Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo pia inaendelea na ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya michezo.

Aidha, amesema Sekta Binafsi imekua na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya michezo, ufadhili wa Timu za mpira wa miguu kwa upande wa wanawake na wanaume, ufadhili wa Ligi Kuu ya Tanzania, ujenzi wa miundombinu na uendelezaji wa vipaji vya Sanaa na Utamaduni.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Othman Yakubu akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imekua na mchango mkubwa katika kukuza ajira na Pato la Taifa hapa nchini kwa kuwa ni Sekta inayoshughulika na Watanzania wote.

Ameeleza kuwa baadhi ya nchi Sekta hizo ndizo zinazopewa kipaumbele kutokana na mchango wake katika uchumi akibainisha kuwa baadhi ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini zimetoa kipaumbele kikubwa kwenye eneo la Ubunifu.View attachment 2571413View attachment 2571415View attachment 2571414View attachment 2571416View attachment 2571418View attachment 2571417View attachment 2571419View attachment 2571420
1680199989738.jpg
1680199983425.jpg
1680199986403.jpg

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huwa sielewi katika watanzania wanaume milioni 30 hivi; milioni 10 hivi walio between 18 na 35 tunakosa watanzania 11 wa kuiheshimisha timu yetu ya taifa hadi tufungwe na Uganda. Ni fedheha.
 
Back
Top Bottom