Napenda sana upweke

Napenda sana upweke

utapataje ubunge na hupendi socialization? Angalia usije hisiwa ni mchawi au ni mwizi ukakosa wa kukutetea sikumoja maana hujulikani unaishi kama mwizi mwizi tu, at least uwe na marafiki wachache na ujulikane vyema kwa majirani zako kwamba wewe ni nani na umetoka wapi. Hv kweli hata jina lako hawakujui ndugu yangu sasa unaishije aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah huu uzi 90% ni mm kabsa, yan ukniona unaweza sema sio mm nnavyokoment humu ndan na real life nlivyompole. Kuna advertise nlimuonesha dem flan hakuamin, ye alikuwa mshkaj tu so siku hyo aliamua kuja geto kuntembelea... Alivyofika akagonga mlango me npo ndan nauliza nan kunijibu nkamwambia we nisubiri huko huko nakuja. Aisee hakuamin! Mpaka leo tukikutana ananiambia "yan ww sio mtu wa kawaida kabsa" me nacheka tu

Sometimes soft is strong

Sent using Jamii Forums mobile app
 
utapataje ubunge na hupendi socialization? Angalia usije hisiwa ni mchawi au ni mwizi ukakosa wa kukutetea sikumoja maana hujulikani unaishi kama mwizi mwizi tu, at least uwe na marafiki wachache na ujulikane vyema kwa majirani zako kwamba wewe ni nani na umetoka wapi. Hv kweli hata jina lako hawakujui ndugu yangu sasa unaishije aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
Haaahh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jf kila mtu introvert
Hapo hapo mnatuambia mimi hivi mimi vile wakati maisha yenu ya siri
Sio hvyo unavyofikiria princess ariana ila mtu mwenye hiyo hali akiuona huu uzi lazma apite nao sababu unamuhusu. Alafu factor ya kuja kusemea humu ni kwamba hatufahamiani ID zetu fake so mtu anakuwa free kutiririka tani yake. Si ajabu tunafahamina mm na ww sema ID zetu ndo znatuficha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio hvyo unavyofikiria princess ariana ila mtu mwenye hiyo hali akiuona huu uzi lazma apite nao sababu unamuhusu. Alafu factor ya kuja kusemea humu ni kwamba hatufahamiani ID zetu fake so mtu anakuwa free kutiririka tani yake. Si ajabu tunafahamina mm na ww sema ID zetu ndo znatuficha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
aiii mbona wengi nawafahamu 😂.. Introvert umebebwa na ubinafsi, binadamu ili uenjoy unatakiwa uwe introvert 50% extrovert 50%
 
Ni sawa na useme unapenda NJAA! Sema unapenda kuwa mwenyewe, ni tofauti na upweke. Upweke ni kukosa company huku unaitamani.
Siku hizi watu wengi ni introverts hata hawahitaji marafiki wana uwaki mwingi sana.
 
Nadhani wewe unapenda kuwa peke yako na sio upweke!
Zamani nilikuwa napenda sana kutuma message, ikafika kipindi nikaona message ni kupotezeana muda mtu akinitumia meseji mimi sijibu nampigia. Ukafika muda ata nikiwa na dakika za kupiga simu Sipigi simu. Pia nikikuta meseji na missed call isiyo na umuhimu ama namba mpya sipigi kabisa. Ikitokea nikipiga sitaki maneno mengi kabisa.

Siku zinavozidi ndio namimi nazidi kupenda upweke. Kuna muda natamani kuzima simu kwa muda mrefu nisiwasiliane na watu mpaka Mimi nitakapohitaji kufanya hivyo.

Maisha yangu ni ya ukimya kuongea kidogo sana, Nina marafiki wachache na sijawahi mkaribisha yeyote anaenijua kwangu. Ni kawaida yangu tokea nikiwa Mdogo nilikuwa naenda kucheza nyumbani kwa wenzangu lakini kwetu. Hapana na siku marafiki wakija nyumbani nawatoa nawaambia twendeni tukachezee nyumbani kwa Fulani.

Sasa nimekua mtu mzima najishangaa muda mwingine ata ukiniambia upo karibu na kwangu nitakuelekeza nisubiri sehemu Fulani imenifanya niishi maisha ya siri sana sipendagi kutoa ABC zangu.

Kuna muda naweza kutofautiana na wife akinilaumu kwa nini usimkaribishe tu huyo rafiki yako nyumbani namkatalia, akiniambia rafiki zake wanakuja lazima nitoke home nakuwa sitaki tu wanione shemeji yao japo wananijua napenda tu kuwa scarcity.

Ukinidadisi sana nitakudanganya kulingana na unavyoweza nizania wewe. Nafurahi sana kuishi maisha ya watu kutonifahamu nafanya biashara lakini sipendi kufanya na majirani sijui ata kwanini lakini napenda tu iwe ivo. Napenda sana kujua mambo ya wengine ila mambo yangu ni Siri sana ata mtaa ninaoishi hawanifahamu kwa jina langu halisi zaidi ya Balozi na M/Kit wangu, sipendi mtu wa mtaa ajue ndugu zangu kwa namna yeyote ile.

Sipendi kabisa kukaa na watu wanaonifahamu kwa namna yeyote ile mimi ukinijua tu wazazi, nilikokulia na mambo mengine ya nyuma urafiki na wewe unakuwa mashakani sana.

Hata watoto wangu nawalea kama agents wa CIA ama KGB, kusoma vitabu sana, mafunzo ya karate na kazi pamoja na study za maisha. Michezo ni shuleni tu wakirudi home ratiba inaanza SAA 9:30 usiku wanalala

Jirani akinizoea sana sipendi kabisa mzoea huwa sijisifu kwa chochote napenda kupita njia tofauti tofauti, Mara zote huwa naishi kama vile Nina RB. Lakini sina tatizo kabisa na mtu . Ni mazoea tu.

Sipendi kuzoeeleka popote iwe bar ama club's. Sipendi kukaa eneo moja muda mrefu mfano bar lazima nibadili ata sehemu tatu kwa muda machache APA nazani sababu napenda kutembea.

Napenda sana kuelimisha watu kuhusu maisha na mengineyo angalau waweze kubadili mboga ila sio jambo rahisi kwani kuna muda ata Mimi nashindwa kubadili mboga na kadhalika.

Kuna muda I wish ningekuwa OCD / CID ila sijui kama wanatakaga loneness creature kama Mimi. Sipendi kabisa usumbufu naweza kukubali yes yes yes tu ili uondoke, sipendi kuongea sana na nikinywa pombe naongea kiasi ila vyote nitakavosema ni propaganda tu, stories, fictions ambazo haziusiani na Mimi kabisa na hufanya hivyo tu kusudi wasinitenge na kuniona mimi ni mkimya sana hapo nakuwa najilazimisha kuongea kuchangansha Genge.

I do enjoying being alone and in state of unknown for no reason hii imepelekea kuzaniwa Mimi labda nipo usalama wa taifa kwangu sioni kama ni sifa mbaya sana.

Mbaya sasa napenda sana siasa nafuatiliaga kila tukio la habari kwa kina za ndani na nje ya nchi. Kwa sasa natafuta pesa nikipata nyingi nitagombea ubunge mwaka 2035 Niwagawiapo na wananchi wangu kidogo wafurahi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimekuzidi.....
mm maongezi yangu ni humu tu na wana jf...
mtaani hata sauti yangu hawaijui...
 
Nikipanda staff bus to job, nikiingia naenda kukaa siti ya peke yangu, au nakaa na mtu mbae najua hawezi niongelesha.

Tukifika kituon ambacho anapanda mtu naihisi kuna mazoea atakuja kunifata na kunipa story zake, bas najifanya nmesinzia.

Kantini job nachukua msosi mwisho, ili nkakae meza ya peke yangu. Maana nikitangulia kukaa mtu anaenijua akiniona anakuna tukae wote. Me simaindishi.

Mara nyingi kifurush najiunga cha wiki ili nipate mb. Sasa zile dakika 150 ckumbuki km nmewah zitumia zaid ya dak 50. Nazo hizi dak 50 labda nmpigie maza.. most of the time zinaexpire.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom