Rafiki! nadhani avator yako hapo inahusika.
Naomba nikushauri kwa Mujibu Biblia ambayo ninaamini ndio unayoiamini, ndoa na harusi ni vitu viwili ambavyo wala havina uhusiano kabisa..
1.Ndoa ni makubaliano ya kuishi kama mume na mke kati ya jinsia mbili tofauti, ili kuwawezesha kutekeleza amri ya Mungu, mkazae na kuijaza nchi,Kasome kitabu cha Musa, Mwanzo.
Pili ni kuweza upambana na tamaa za mwili, Kasome Waraka wa Paulo kwa Wakorinto..
2. Harusi ni sherehe ambayo walioona wanaandaa chakula wanakula na ndugu na marfiki kufurahia na kufahamiana na hayo sio maagizo ya Mungu. Tatizo lililopo sasa hivi ni kwamba harusi inapewa kipaumbele kuliko ndoa, na kwa sababu tumezoea kuchangisha wachangishwaji wana nafasi ya kukontroll ndoa yako. ndio wakijua hakuna pombe wanachanga 10,000.
Nakushauri kama uwezo wa kufanya sherehe wewe huna kafunge ndoa yako, ukimaliza rudi nyumbani andaa chakula cha mchana mle na mwenzako, kama una uweza waalike majirani yako...ila achana kufuata mapokeo ambayo hayana faida yoyote ktk maisha yako,
Nimefunga ndoa 10 years ago na nilifanya harusi ila sikupenda headache ya kukumbizana na michango wala kupoteza muda, niliandaa bajeti niliyoimudu na nikatumia pesa yangu wenyewe almost 90% nikamaliza mchezo na tunafuraha hakuna kudhalilika mtaani eti unaringa wakati mke tumekuozesha sie na harusi tumekuanyia..
ondo woga askari