Napenda kuoa ila sina kipato

Napenda kuoa ila sina kipato

Mbona mimi nina "demu" na akaunti zangu zote zinasomeka hivi;
..M-Pesa: 5000Tsh;
..Tigo Pesa: 5000Tsh
..Airtel Money: 0.000Tsh
..NMB: 10000Tsh
..CRDB: 20000Tsh
..TPB: 10000Tsh
Jumla ya pesa katika accounts zangu; 50, 000tsh na mamito ananipendaje...we oa tu maisha ndo haya haya..
 
usidanganywe waweza oa bila kipato
jipange kwanza kuoa ni majukumu na lazima uwajibike kama baba kutunza mke si lele mama ati
 
Tafuta jimama lenye mshiko mnasaidiana majukumu kama kweli wewe muoaji
 
Mimi huwa nashindwa kuelewa kitu kimoja, samahani (sio wanawake wote) na hata wanaume baadhi tuna upungufu wetu, naomba kuingiza swali la kizushi

Inakuaje mwanamke anagharamiwa kila kitu na mumewe, uwezo wa kila kitu upo, mapenzi anapewa ya kutosha, na hata kwenye mtanange hapunjwi, sasa inakuaje tena mwanamke huyo huyo anaepewa/anaepata kila kitu bado anadiriki kutoka nje ya ndoa? mbaya zaidi anatoka na mtu ambae hajielewi kimaisha yaani hana mbele wala nyuma?


Wakati kwa mumewe mambo yote ya maana yapo !
 
Hata vitabu vya dini vinasema mwanaume atatunza familia mwanamke atajaza dunia means kazi yake ni kuzaa tu na kutunzwa na mwanaume
 
Majani yenyewe ya bure atayapata wapi! Hata ya mwarobaini atachuma kwa nani!

Kijana, tafuta hela kwanza. Ukizidiwa unashitua na one night stand!

Atawaolea watu we mwache adhani kuoa ni kama kujiunga na kifurushi cha jero afu unachat siku nzima....
 
Mbona mimi nina "demu" na akaunti zangu zote zinasomeka hivi;
..M-Pesa: 5000Tsh;
..Tigo Pesa: 5000Tsh
..Airtel Money: 0.000Tsh
..NMB: 10000Tsh
..CRDB: 20000Tsh
..TPB: 10000Tsh
Jumla ya pesa katika accounts zangu; 50, 000tsh na mamito ananipendaje...we oa tu maisha ndo haya haya..

Kwa hizo account zote lazima una cash flow inayoeleweka sema tu sasa hiv kuna mahali zimekwama.
 
Mimi huwa nashindwa kuelewa kitu kimoja, samahani (sio wanawake wote) na hata wanaume baadhi tuna upungufu wetu, naomba kuingiza swali la kizushi

Inakuaje mwanamke anagharamiwa kila kitu na mumewe, uwezo wa kila kitu upo, mapenzi anapewa ya kutosha, na hata kwenye mtanange hapunjwi, sasa inakuaje tena mwanamke huyo huyo anaepewa/anaepata kila kitu bado anadiriki kutoka nje ya ndoa? mbaya zaidi anatoka na mtu ambae hajielewi kimaisha yaani hana mbele wala nyuma?


Wakati kwa mumewe mambo yote ya maana yapo !

Unajua ktk ndoa mwanaume unatakiwa kuwa mtundu ktk mapenzi kuwa pesa,gari na nyumba siyo tija sasa cha ajabu yule ambaye hana pesa lkn ni mtundu kwenye mapenzi
 
Eh mkuu siku hz kuna fursa nyng,kama huna hela na hujui pia kutafta hela fanya hvi,tangaza hapahapa nia ya kutaka kulelewa na sugar mam! Utapata haja na moyo wako,kumbuka No MONEY No HONEY!
 
oa kijana itafahamika tu kwan ww hauli,huvai,hulali
 
Mkuu tatizo mimi naona sio kipato ila ni nani una muoa?ukipata mke muelewa basi mtashirikiana kukabili changamoto na hatimae kukuza kipato.ila siku hizi wanawake walio wengi wanaangalia kipato chako, hawataki waje wateseke kwako.sio kama zamani babu na bibi zetu wengi walioana na kulala kwenye jamvi ,wakakabiliana na changamoto mpaka wakayatoa maisha.ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO...kila la heri
 
Nadhani mleta uzi unajichanganya, mbona kuna wanawake wengi tu nao wanatafuta wanaume wa kuwaowa.

Sema ishu ya kipato inaingia pale wewe (mwanaume) unapohitaji mwanamke fulani, wa hadhi fulani, wa familia fulani, wa elimu fulani n.k.

Kuna stori za ZALI LA MENTALI lakini hizi ni sehemu moja ya elfu moja ya hali halisi.

Kama kweli unahitaji mke wapo tele, ila kama unataka totoz za geti kali.....zichange kwanza braza, ushindani ni mkubwa na mwenye kisu kikali ndio mla nyama.
 
Back
Top Bottom