Napenda kufahamishwa kwa undani kuhusu mizinga 21

Kind

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
247
40
Kwa mara nyingi nimeshuudia ama kusikia viongozi wengi wa selikari wakipigiwa mizinga 21. Ninapenda kufahamu yafuatayo
1. Historia ya matumizi ya mizinga 21
2. Ni mizinga ya aina gani hua hutumika.
3. Ni wakati gani hua inaruhusiwa kutumika.
4. Ni askari wa cheo gani hua wanapiga ile mizinga.
5. Je kuna viongoz wengine wanaopigiwa mizinga na hua mingapi?
6. Nchi zipi zinatumia upigaji huu wa mizinga?

Ni matumaini yangu wengi wangependa pia kufahamu.
 
FB_IMG_16167892797102291~2.jpg
 
MIZINGA 21

21 Tank/Gun Salute.

Umekua utamaduni wa KIJESHI Kwa KARNE 7 sasa. Mwanzoni ulikua ukitumika na VIKOSI vya wana maji barani ULAYA kama ishara ya AMANI. Baadae ukabadilishwa na kuwa ISHARA ya HESHIMA. Kutoka ULAYA hadi AMERIKA na sasa DUNIANI kote.
 
Why 21!? Hili ndo. Swali la msingi
 
Me nitaelezea kwa ufupi namna nilivyosoma kwenye course ya Diplomatic and consular relations law...

Katika dunia ya diplomasia kuna sheria zinazoongoza diplomasia baina ya taifa moja na taifa lingine sheria hizo zimetokana na na mikataba mikuu mitatu yote ilifanyika Vienna, Austria na pia sheria nyingine zimetokana na tamaduni(customs) nitajikita sanaa na tamaduni maana ndo swali lako lilipo

Katika tamaduni za kidiplomasia kuna mambo unatakiwa kuyafanya pale kiongozi wa taifa lingine anapotembelea taifa lako au hata kwa kiongozi wako kuonesha heshima mfano kuna zuria jekundu (red carpet) mizinga 21 (21 gun salute) gwaride la heshima (guard of honor) lengo lake ni kuonesha heshima kwa kiongozi huyo

Hili la mizinga 21 Mwalimu wangu aliwai nambia kuwa wametoa kwa kuzidisha 7 mara 3 ambapo jibu huwa ni 21. 7 inasimama kumaanisha siku saba katika juma na 3 inamaanisha utatu mtakatifu kama tunaoamini wakristo. Kwa hiyo ni heshima ya hali ya juu sanaa katika diplomasia msipompigia rais mgeni anaweza akapanda Ndege kulud alipotoka..

Pia mizinga hupigiwa viongozi wa Juu kama waziri mkuu ila yeye huwa ni 19 tu

Hii ndo dunia ya diplomasia
 
Kwahyo siku za maombolezo 21 zinaendana sambamba na 21 guard salute..7*3
 
MIZINGA 21

21 Tank/Gun Salute.

Umekua utamaduni wa KIJESHI Kwa KARNE 7 sasa. Mwanzoni ulikua ukitumika na VIKOSI vya wana maji barani ULAYA kama ishara ya AMANI. Baadae ukabadilishwa na kuwa ISHARA ya HESHIMA. Kutoka ULAYA hadi AMERIKA na sasa DUNIANI kote.
📌📌📌📌📌📌🔒
 
Me nitaelezea kwa ufupi namna nilivyosoma kwenye course ya Diplomatic and consular relations law...

Katika dunia ya diplomasia kuna sheria zinazoongoza diplomasia baina ya taifa moja na taifa lingine sheria hizo zimetokana na na mikataba mikuu mitatu yote ilifanyika Vienna, Austria na pia sheria nyingine zimetokana na tamaduni(customs) nitajikita sanaa na tamaduni maana ndo swali lako lilipo

Katika tamaduni za kidiplomasia kuna mambo unatakiwa kuyafanya pale kiongozi wa taifa lingine anapotembelea taifa lako au hata kwa kiongozi wako kuonesha heshima mfano kuna zuria jekundu (red carpet) mizinga 21 (21 gun salute) gwaride la heshima (guard of honor) lengo lake ni kuonesha heshima kwa kiongozi huyo

Hili la mizinga 21 Mwalimu wangu aliwai nambia kuwa wametoa kwa kuzidisha 7 mara 3 ambapo jibu huwa ni 21. 7 inasimama kumaanisha siku saba katika juma na 3 inamaanisha utatu mtakatifu kama tunaoamini wakristo. Kwa hiyo ni heshima ya hali ya juu sanaa katika diplomasia msipompigia rais mgeni anaweza akapanda Ndege kulud alipotoka..

Pia mizinga hupigiwa viongozi wa Juu kama waziri mkuu ila yeye huwa ni 19 tu

Hii ndo dunia ya diplomasia
Noted
 
1.ASILI

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao, Saluti ya Mizinga 21 asili yake ni katika enzi za karne ya 14 na ni utaratibu ulioanzishwa na Jeshi la wanamaji la Uingereza kipindi hiko.

Meli za kijeshi za Jeshi la wanamaji la Uingereza zilipokuwa zinawasili katika bandari ngeni kwao, zilikuwa na utaratibu wa kupiga mizinga kwa umbali ambao hauwezi kuathiri au kulipua katika uelekeo ambao ndipo bandari ya wenyeji wao ipo.

Hii ilikuwa ni ishara ya kuwaonesha wale wenyeji wao kuwa wana "empty" au wanaifanya Mizinga yao kuwa mitupu kipindi wanakaribia katika eneo la bandari.. Kwa kipindi hiko mizinga ndo ilikuwa kama silaha hatari kwa mashambulizi inayotumika katika mapambano ya kivita majini.

Kitendo cha meli ya kijeshi inayopiga mizinga isiyokuwa na madhara ilikuwa inatafsiriwa na wenyeji kama ishara ya wageni kutotaka mapambano na wamekuja kwa nia nzuri.

2. KWANINI MIZINGA 21??

Kwa wakati huo ina aminika, meli nyingi za kivita za Uingereza zilikuwa na uwezo wa kuchukua MIZINGA 7 katika meli moja. Na ndo maana mizinga yote saba ilikuwa inaandaliwa na kupigwa kwa kipindi ambacho meli inajiandaa kuwasili katika bandari ya nchi ngeni.

Pia ilikuwa ni shughuli kuandaa mzinga kwaajili ya kupigwa tena kulingana na teknolojia ilivyokuwa kipindi hicho. Hii pia ilikuwa inawapa amani wenyeji kwa kuamini meli inayokuja bandarini kwao haina muda wa kutosha kujiandaa na shambulizi lolote lile ambalo wanaweza kutumia mizinga yao.

Baada ya utaratibu huu wa Meli ya kigeni inayowasili bandarini kuhakikisha ina empty mizinga yake kabla ya kutia nanga, Ikaonekana pia wenyeji nao wanatakiwa kuonesha ishara ya amani kama wageni wao pia.

Hapa ndipo ukaja utaratibu wa wenyeji nao kuhakikisha mizinga yao iliyoko bandarini inakuwa mitupu kama vile wageni wao wanaotaka kutia nanga katika bandari yao.

Hapa WENYEJI WALIPIGA MIZINGA 3 kwa kila MZINGA 1 ambao ULIPIGWA NA MELI YA KIGENI. Kumbuka meli ya kigeni ilikuwa na MIZINGA 7 kwahiyo wenyeji walitakiwa kupiga MIZINGA 21 ili kwenda sawa na wageni wao.
(7 x 3 = 21)

Utaratibu huu uliendelea mpaka karne ya 18 ukaingizwa rasmi katika jeshi la Uingereza ambapo ikawa ni utaratibu kwa ugeni wowote ule wa kimataifa ukija nchini kwao au katika makoloni yao basi watapiga mizinga 21 kama ishara ya heshima kwa ugeni huo kwa taifa lao.

Pia kupiga mizinga 21 ikawa ni utaratibu rasmi wa kutoa salamu kwa familia ya kifalme. Baadaye wamarekani waka adapt huu mfumo kwa kutoa salamu kwa viongozi wao wa kitaifa.

Kutokea hapo ndo kuna mtiririko wa mabadiliko na utaratibu wa kidiplomasia ambao uliendelea mpaka kuwa adapted na nchi zingine duniani.

View attachment 1735524
images%20(3).jpg
 
Kwa mara nyingi nimeshuudia ama kusikia viongozi wengi wa selikari wakipigiwa mizinga 21. Ninapenda kufahamu yafuatayo
1. Historia ya matumizi ya mizinga 21
2. Ni mizinga ya aina gani hua hutumika.
3. Ni wakati gani hua inaruhusiwa kutumika.
4. Ni askari wa cheo gani hua wanapiga ile mizinga.
5. Je kuna viongoz wengine wanaopigiwa mizinga na hua mingapi?
6. Nchi zipi zinatumia upigaji huu wa mizinga?

Ni matumaini yangu wengi wangependa pia kufahamu.
Pia la kujua Sio viongozi wote wanaopigiwa mizinga 21, wapo wanaopigiwa 19, wapo wanaopigiwa 17...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom