fabinyo
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 3,043
- 2,245
"....mke wangu wa ndoa anajua sana kupika bro,hilo sipingi hata kidogo ila ajabu nafurahia zaidi msosi wa kwenye misiba,ambao kikawaida hauna kiwango,chukuchuku na huandaliwa katika mazingira sio salama sana hasa misiba ya uswazini kwetu,mara nyingi ni wali/ugali na harage/nyama lakini ndio naupenda balaa,nimejaribu kujikausha kama hili sio tatizo lakini imebidi niseme tu kwani nathani hali hii sio ya kawaida,ukizingatia nina heshima zangu,kazi nzuri na familia yangu iko safii kwani kipato si haba,msiba ukitokea popote nimo na kabla hata ya kufika nawaza msosi wa huko tu....."
Maelezo ya rafiki yangu,Baba Cornel wakati tukipata kinywaji jana usiku,Forodhani.Tanga!Tusaidiane wadau,hili ni tatizo gani?hataki hali hii kabisa
Maelezo ya rafiki yangu,Baba Cornel wakati tukipata kinywaji jana usiku,Forodhani.Tanga!Tusaidiane wadau,hili ni tatizo gani?hataki hali hii kabisa