Nape, Zitto na Msigwa waungwe mkono, Changamoto na mapokeo ya TISS

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Leo nataka nishereheshe hoja ya Mh Nape Nnauye Bungeni ikiungwa mkono na wabunge Mh Msigwa na Mh Zitto Kabwe ya kupendekeza mabadiliko ya mfumo wa usalama wa Taifa nchini Tanzania. Hoja hii ni muhimu sana sana kiliko inavyofikiriwa, na nihimize wabunge waitilie mkazo bila kuathiriwa na itikadi za kisiasa. Nimesikiliza hata majibu ya hoja ya Mh Waziri Mkuchika akitetea kwamba TISS haihitaji marekebisho kwakuwa inafanya kazi kwa ufanisi.

Nijaribu kumkumbusha Waziri Mkuchika, mabadiliko ya idara au mashirika ya kiusalama duniani sio jambo geni ama jambo la siri, Tarehe 20 January 1996 Mzee Mkapa alitia saini sheria iliyounda upya chombo hiki cha ujasusi kutoka kuitwa Tawi Maalumu ndani ya Jeshi la Polisi, (SB) na kuzaliwa TISS, Mzee Mkapa alitumia Buge hilihili la Jamhuri kufanya mabadiliko haikuwa siri, hakuna mbunge asiyejua kazi na majukumu ya TISS kwakuwa yapo kisheria kwa sheria iliyotungwa na Bunge, Kifungu cha sheria ya Usalama wa Taifa (Duties and Power of TISS) kifungu cha 14-(1),(2),(3) (a) na (b), kinafafanua wazi kazi za MSINGI za TISS. Lakini haiishii hapo tu, kifungu cha 15-(1),(2),(3) (a),(b),(c) na kifungu (4).

Sasa leo Mkuchika akiwapinga wabunge kwa hoja kuwa hawajui kazi za kisheria za TISS inashangaza na huku ndio kuingiza siasa kwenye chombo hiki, kwa Mataifa yaliyoendelea Waziri alitakiwa kutulia na kujibu kwa hoja mujarabu za kimantiki au kupokea hoja za wabunge na kuzipeleka katika vyombo vya michakato kuliko kujibu tu tena kienyeji tu kwa hoja nyeti kama hii.Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi nimeleza kwa kirefu kwanini mabadiliko ya TISS ni muhimu, fuatana nami hapa chini toka kitabuni:

Idara ya TISS ambayo ndio uhai wa taifa la Tanzania imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali. Wadadisi wa masuala ya kijasusi watakubali kuwa TISS ndicho chombo pekee nchini Tanzania kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa lilipo sasa, Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayotakiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo ya Sayansi na Teknolojia na uchumi wa kijasusi, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote muhimu kuanzia uhusiano,watendaji,teknolojia na sheria. Mathalani Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996 iliyounda upya chombo hiki ina upungufu kwa sasa kulingana na mageuzi dunia ya kifikra na kiteknolojia, Sheria hii inaififisha taasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu, sheria inasema, "kazi yake kubwa ni kukusanya na kuchambua taarifa (intelligence gathering and analysis) na kuzipeleka/kushauri wahusika kuchukua hatua."

Kwa maneno hayo, TISS imenyimwa nguvu ya moja kwa moja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu. Mara nyingi utekelezwaji wa aina kama hii ya sheria hufaa kwenye mataifa ya kijamaa na kiimla, lakini kwenye mataifa ya kidemokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi ni hatari sana kuwapo kwa sheria hii. Upitishaji wa sheria hiyo lilikuwa shambulizi moja kubwa dhidi ya mamlaka ya Usalama wa Taifa lililohitimishwa kwa kutekwa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa. Wanasiasa na mafisadi walifanikiwa, na tangu hapo kuyumba na kudorora kwa taifa kila nyanja ndipo kulipoingia Tanzania. Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika kutekeleza wa ushauri wanaopewa na chombo hiki, Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hiyo ili taasisi ya Usalama wa Taifa Tanzania iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo uhuishwaji wa sheria hii ufanywe kwa umakini ili kutofungua mwanya wa idara hii kuwa na nguvu ya kumuondoa kiongozi/rais pia uende sambamba na kuifanya imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii awajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa za vyama.

Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kikanda (regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi. TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni rahisi katika kufanya ubadilishanaji wa taarifa za kijasusi (informations sharing) wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani, Uingereza, Pakistan, Israel, Afrika Kusini, China, India na Canada.

Ingawa mikakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekuwa ikibadilika kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima ianze na kanda ya Maziwa makuu, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii ni kwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa lenye utajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI ya kutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma. Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na mpinzani wetu hapa Afrika Mashariki ni Kenya.
Hatujaweza vya kutosha kwenye ujasusi wa kiuchumi (Economic intelligence) kule Kenya ingawa wao wamewekeza hapa kwetu. Leo hii Kenya inasafirisha madini ya TANZANITE, wanasafirisha dhahabu na kadhalika. Uwiano wa kibiashara (Balance of trade) kati ya Tanzania na Kenya ni somo la ujasusi wa kiuchumi kwa nchi ya Tanzania (Economic intelligence). Tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiintelijensia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie masuala tata yanayoweza kuibuka na mwenendo wa washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi wa Tanzania hapa Afrika mashariki kupitia Kenya?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu ya Tanzania, Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekuwa zikinunuliwa kwa wingi na kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi na kuvuruga sera za uchumi Tanzania? Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe ya kisasa zaidi. Malengo ya TISS kulingana na hali ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri (si utabiri wa majini/tunguri) bali ule wa kisayansi, kupenya, na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu, na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye nyanja za kimataifa(jamii nyingine).

Ili kujenga nguvu ya propaganda ya kijasusi, mageuzi muhimu yawe kwenye uhamilishaji wa habari. Lazima ziwepo habari za kijasusi ambazo zitakuwa hadharani, hasa zile ambazo TISS itaamua umma ujue ikilenga kanda ama Afrika zifahamu kwa manufaa ya Tanzania. Ni zile habari tu ambazo zinatolewa na kudhibitiwa na vitengo vya "disinformation and misinformation". Kwa hiyo hapo ni kwamba TISS hawajafanikiwa kwenye hivyo vitengo kama ambavyo wanashindwa kufanya kwenye ujasusi wa kiuchumi na upandikizi kiuchumi.

Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi, hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe na Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI). Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe. Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.

Siku moja Luten Kanali Likvol Shekvov mkufunzi wa tabia na hisia za kibinadamu katika chuo cha majasusi cha Russian Federal Security Service (RFSS), alibainisha kuwa hulka za kibinadamu huathiriwa na unafiki, lakini unafiki usio na bughudha "unaolipa zaidi" ni ule ufanywao na wazee. Chuo hiki ni maarufu ulimwenguni kwakufundisha majasusi, na hasa ufundishaji wa somo maarufu liitwalo ujasusi wa kisaikolojia (Forensic psychology). Ndani ya kozi hii ndimo huzaliwa ama hupatikana majasusi wabobevu wa saikolojia ya binadamu na mazingira ambao kwa lugha ya kijasusi huitwa Profiler.

Pengine kama ilivyokuwa kwa Rais Boris Yeltsin wa Urusi kuibadili KGB kwenda FSB, hata hapa Tanzania kwa sasa kuna viashiria dhahiri hatuna mfumo imara wa kijasusi na kimsingi, tunahitaji marekebisho makubwa ambayo kimsingi ni sawa na kuweka mfumo mpya. Ni dhahiri kuna udhaifu wa mfumo wetu huo. Udhaifu huu unadhihirika katika baadhi ya michakato ya kitaifa, hasa masuala ya uchumi. Mfumo wetu wa utafutaji taarifa nyeti hauna tija na kimsingi una mianya inayoruhusu nchi kudanganywa au kutapeliwa kirahisi mno hata na kampuni kubwa za kimataifa. Baadhi wanaamini mfumo wetu bado ni imara isipokuwa taarifa hizo nyeti, mara kwa mara hazitumiki ipasavyo au hupuuzwa kabisa. Hoja hii ni nyepesi mno na binafsi siamini hivyo. Mfumo wa kiusalama ambao una mianya inayotoa fursa kwa taarifa zake nyeti zilizokusanywa kwa njia hatari na gharama kubwa kutotumika hata kama zinabeba maslahi ya nchi, huo ni mfumo dhaifu.

Mfumo wa namna hiyo unapaswa kuvunjwa au kufanyiwa marekebisho makubwa. Mfumo wa kiusalama lazima si uwe na uwezo mkubwa wa kusaka taarifa nyeti kwa njia yoyote (halali au kinyume chake), lakini pia unapaswa kujijengea mazingira ya kuhakikisha matumizi bora ya taarifa hizo kwa maslahi ya nchi. Kwa mfano, mapungufu ya ujasusi wa kiuchumi pamoja nakuwa na mfumo ambao si imara kwa sasa wa kukusanya taarifa, yameibuka madudu mengi kwenye mchakato wa ubinafsishaji. Hata ukiangalia michakato mingine muhimu kwa taifa mikono ya kitapeli imeshindwa kudhibitiwa, kwa nini? Ni dhahiri mfumo wetu ni dhaifu isipokuwa swali la kujiuliza; je, udhaifu huo uko kwenye eneo gani mahsusi? Je, ni eneo la ukusanyaji taarifa au ni matumizi ya taarifa husika? Au vyote viwili? Ndani ya maswali haya, ufumbuzi muhimu unaojitokeza ni kwamba; tunahitaji mfumo imara zaidi wa kiusalama nchini na hasa kwenye eneo la uchumi na siasa kama ilivyo kwa Urusi ya Yeltsin kwa wakati ule.

Mfumo ambao si tu utakusanya taarifa kwa mujibu wa mahitaji lakini pia taarifa hizo zitajengewa mazingira ya lazima ili kutumika kwa manufaa ya nchi. Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na mfumo ambao utekelezaji wa taarifa zake unategemea upeo wa kiongozi mkuu pekee, ingawa pia Rais ni taasisi. Tujenge mfumo ambao ingawa utahitaji wanasiasa, wachumi, wahandisi, wanasheria na wanataaluma wengine lakini kamwe usiwe na maslahi ya moja kwa moja na makundi hayo wakati wote. Kwa sasa, inawezekana mfumo wetu umefungamana zaidi na utashi wa baadhi ya wanasiasa kuliko utaifa. Tunahitaji kujenga mfumo mpya imara wa kiusalama ambao utakuwa karibu na taaluma zote nyeti lakini hautafungamana na maslahi ya taaluma hizo wala wanataaluma husika.Hii itasaidia kujenga mwelekeo wa taifa katika mazingira halisi ya mwelekeo wa dunia na si mazingira ya utashi wa wanataaluma au wanasiasa husika.

Kwa bahati mbaya, mfumo wetu wa sasa umejenga hisia kwa umma umetekwa na wanasiasa na zaidi, ni mfumo uliowekezwa katika siasa kuliko eneo la uchumi. Chombo chetu hiki lazima kicheze vilivyo na kwa ustadi disko la dunia kuhusu uchumi zaidi na si siasa pekee. Hisia kwamba mfumo wetu wa kiusalama ni dhaifu zina ushahidi. Pale tulipopaswa kudhibiti au kuchukua hatua kabla, tumeshindwa kufanya hivyo na hatimaye kufikwa na madhara yasiyo ya lazima. Matapeli wasiojaa hata mkononi wanaingia popote na kufanya wizi wa mali za umma. Wengine wanafanya hivyo wakijiita wawekezaji wa kimataifa ambao baadhi ya makuwadi wao ni wanasiasa au wataalamu wetu mashuhuri nchini.Kama tunafeli kudhibiti masuala yaliyoko ndani ya uwezo wetu tutawezaje kupanga na kutekeleza mipango ya kupata taarifa nyeti kutoka kwa mataifa mengine ili tujenga taifa bora zaidi katika ushindani wa kidunia? Kwa nini hata wale wanaojifunza au kuchipukia kwenye utapeli wa kimataifa (wawekezaji), Tanzania iwe sehemu yao ya mazoezi?

Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.......

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni 80,000/= tu.

Piga simu 0715865544 au 0755865544 popote ulipo utaletewa...

Na Yericko Nyerere
 
Sijaona sababu ya kubadilisha mwenendo,muundo na sheria inayosimamia TISS kwa hoja eti watu wanapotea.

Namshangaa mbunge anayesema eti TISS haifuatili maswala ya uchumi wakati haijapita hata mwaka tumeshuhudia kazi muhimu ya TISS kwenye sekta na sakata la madini.

Tusipende kuwa parrots au kasuku kwa kuigaiga mambo bali tuwe na hoja zinazojengwa kutoka kwenye tafiti.

Mfano kati ya watanzania milioni zaidi ya 58 ni wangapi wamepotea au kupigwa risasi?
 
Utaonane na we jingalao?
 
Nyakati zingine uwe unaweka mahaba ya kisiasa pembeni
 
Sijaona sababu ya kubadilisha mwenendo,muundo na sheria inayosimamia TISS kwa hoja eti watu wanapotea.

Namshangaa mbunge anayesema eti TISS haifuatili maswala ya uchumi wakati haijapita hata mwaka tumeshuhudia kazi muhimu ya TISS kwenye sekta na sakata la madini.

Tusipende kuwa parrots au kasuku kwa kuigaiga mambo bali tuwe na hoja zinazojengwa kutoka kwenye tafiti.

Mfano kati ya watanzania milioni zaidi ya 58 ni wangapi wamepotea au kupigwa risasi?
Sasa hivi hamtaona siku haya mapigo yakiwarudi mtaona bila kuambiwa
 
Damu ya Mtanzania mmoja ina thamani kubwa sana. Najua watanzania tunafurahia kumwaga damu ndiyo maana ukiitwa mwizi mitaani hakuna anayesubiri ushahidi - unashughulikiwa papo hapo!
 
Leo nataka nishereheshe hoja ya Mh Nape Nnauye Bungeni ikiungwa mkono na wabunge Mh Msigwa na Mh Zitto Kabwe ya kupendekeza mabadiliko ya mfumo wa usalama wa Taifa nchini Tanzania.

Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.......

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni 80,000/= tu.

Piga simu 0715865544 au 0755865544 popote ulipo utaletewa...

Na Yericko Nyerere
Naunga mkono hoja, baada ya tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lisu, nilishauri, hawa Jamaa wafumuliwe!.
TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali Wachunguzwe, Wafumuliwe!

P.
 
Waungwe mkono hata pale tutakaposikia wametekwa na kupotezwa kama akina Ben na tutakaposikia wamefanyiwa pyuupyuu
 
Leo nataka nishereheshe hoja ya Mh Nape Nnauye Bungeni ikiungwa mkono na wabunge Mh Msigwa na Mh Zitto Kabwe ya kupendekeza mabadiliko ya mfumo wa usalama wa Taifa nchini Tanzania. Hoja hii ni muhimu sana sana kiliko inavyofikiriwa, na nihimize wabunge waitilie mkazo bila kuathiriwa na itikadi za kisiasa. Nimesikiliza hata majibu ya hoja ya Mh Waziri Mkuchika akitetea kwamba TISS haihitaji marekebisho kwakuwa inafanya kazi kwa ufanisi.

Nijaribu kumkumbusha Waziri Mkuchika, mabadiliko ya idara au mashirika ya kiusalama duniani sio jambo geni ama jambo la siri, Tarehe 20 January 1996 Mzee Mkapa alitia saini sheria iliyounda upya chombo hiki cha ujasusi kutoka kuitwa Tawi Maalumu ndani ya Jeshi la Polisi, (SB) na kuzaliwa TISS, Mzee Mkapa alitumia Buge hilihili la Jamhuri kufanya mabadiliko haikuwa siri, hakuna mbunge asiyejua kazi na majukumu ya TISS kwakuwa yapo kisheria kwa sheria iliyotungwa na Bunge, Kifungu cha sheria ya Usalama wa Taifa (Duties and Power of TISS) kifungu cha 14-(1),(2),(3) (a) na (b), kinafafanua wazi kazi za MSINGI za TISS. Lakini haiishii hapo tu, kifungu cha 15-(1),(2),(3) (a),(b),(c) na kifungu (4).

Sasa leo Mkuchika akiwapinga wabunge kwa hoja kuwa hawajui kazi za kisheria za TISS inashangaza na huku ndio kuingiza siasa kwenye chombo hiki, kwa Mataifa yaliyoendelea Waziri alitakiwa kutulia na kujibu kwa hoja mujarabu za kimantiki au kupokea hoja za wabunge na kuzipeleka katika vyombo vya michakato kuliko kujibu tu tena kienyeji tu kwa hoja nyeti kama hii.Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi nimeleza kwa kirefu kwanini mabadiliko ya TISS ni muhimu, fuatana nami hapa chini toka kitabuni:

Idara ya TISS ambayo ndio uhai wa taifa la Tanzania imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali. Wadadisi wa masuala ya kijasusi watakubali kuwa TISS ndicho chombo pekee nchini Tanzania kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa lilipo sasa, Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayotakiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo ya Sayansi na Teknolojia na uchumi wa kijasusi, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote muhimu kuanzia uhusiano,watendaji,teknolojia na sheria. Mathalani Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996 iliyounda upya chombo hiki ina upungufu kwa sasa kulingana na mageuzi dunia ya kifikra na kiteknolojia, Sheria hii inaififisha taasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu, sheria inasema, "kazi yake kubwa ni kukusanya na kuchambua taarifa (intelligence gathering and analysis) na kuzipeleka/kushauri wahusika kuchukua hatua."

Kwa maneno hayo, TISS imenyimwa nguvu ya moja kwa moja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu. Mara nyingi utekelezwaji wa aina kama hii ya sheria hufaa kwenye mataifa ya kijamaa na kiimla, lakini kwenye mataifa ya kidemokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi ni hatari sana kuwapo kwa sheria hii. Upitishaji wa sheria hiyo lilikuwa shambulizi moja kubwa dhidi ya mamlaka ya Usalama wa Taifa lililohitimishwa kwa kutekwa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa. Wanasiasa na mafisadi walifanikiwa, na tangu hapo kuyumba na kudorora kwa taifa kila nyanja ndipo kulipoingia Tanzania. Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika kutekeleza wa ushauri wanaopewa na chombo hiki, Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hiyo ili taasisi ya Usalama wa Taifa Tanzania iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo uhuishwaji wa sheria hii ufanywe kwa umakini ili kutofungua mwanya wa idara hii kuwa na nguvu ya kumuondoa kiongozi/rais pia uende sambamba na kuifanya imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii awajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa za vyama.

Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kikanda (regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi. TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni rahisi katika kufanya ubadilishanaji wa taarifa za kijasusi (informations sharing) wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani, Uingereza, Pakistan, Israel, Afrika Kusini, China, India na Canada.

Ingawa mikakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekuwa ikibadilika kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima ianze na kanda ya Maziwa makuu, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii ni kwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa lenye utajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI ya kutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma. Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na mpinzani wetu hapa Afrika Mashariki ni Kenya.
Hatujaweza vya kutosha kwenye ujasusi wa kiuchumi (Economic intelligence) kule Kenya ingawa wao wamewekeza hapa kwetu. Leo hii Kenya inasafirisha madini ya TANZANITE, wanasafirisha dhahabu na kadhalika. Uwiano wa kibiashara (Balance of trade) kati ya Tanzania na Kenya ni somo la ujasusi wa kiuchumi kwa nchi ya Tanzania (Economic intelligence). Tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiintelijensia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie masuala tata yanayoweza kuibuka na mwenendo wa washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi wa Tanzania hapa Afrika mashariki kupitia Kenya?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu ya Tanzania, Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekuwa zikinunuliwa kwa wingi na kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi na kuvuruga sera za uchumi Tanzania? Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe ya kisasa zaidi. Malengo ya TISS kulingana na hali ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri (si utabiri wa majini/tunguri) bali ule wa kisayansi, kupenya, na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu, na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye nyanja za kimataifa(jamii nyingine).

Ili kujenga nguvu ya propaganda ya kijasusi, mageuzi muhimu yawe kwenye uhamilishaji wa habari. Lazima ziwepo habari za kijasusi ambazo zitakuwa hadharani, hasa zile ambazo TISS itaamua umma ujue ikilenga kanda ama Afrika zifahamu kwa manufaa ya Tanzania. Ni zile habari tu ambazo zinatolewa na kudhibitiwa na vitengo vya "disinformation and misinformation". Kwa hiyo hapo ni kwamba TISS hawajafanikiwa kwenye hivyo vitengo kama ambavyo wanashindwa kufanya kwenye ujasusi wa kiuchumi na upandikizi kiuchumi.

Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi, hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe na Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI). Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe. Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.

Siku moja Luten Kanali Likvol Shekvov mkufunzi wa tabia na hisia za kibinadamu katika chuo cha majasusi cha Russian Federal Security Service (RFSS), alibainisha kuwa hulka za kibinadamu huathiriwa na unafiki, lakini unafiki usio na bughudha "unaolipa zaidi" ni ule ufanywao na wazee. Chuo hiki ni maarufu ulimwenguni kwakufundisha majasusi, na hasa ufundishaji wa somo maarufu liitwalo ujasusi wa kisaikolojia (Forensic psychology). Ndani ya kozi hii ndimo huzaliwa ama hupatikana majasusi wabobevu wa saikolojia ya binadamu na mazingira ambao kwa lugha ya kijasusi huitwa Profiler.

Pengine kama ilivyokuwa kwa Rais Boris Yeltsin wa Urusi kuibadili KGB kwenda FSB, hata hapa Tanzania kwa sasa kuna viashiria dhahiri hatuna mfumo imara wa kijasusi na kimsingi, tunahitaji marekebisho makubwa ambayo kimsingi ni sawa na kuweka mfumo mpya. Ni dhahiri kuna udhaifu wa mfumo wetu huo. Udhaifu huu unadhihirika katika baadhi ya michakato ya kitaifa, hasa masuala ya uchumi. Mfumo wetu wa utafutaji taarifa nyeti hauna tija na kimsingi una mianya inayoruhusu nchi kudanganywa au kutapeliwa kirahisi mno hata na kampuni kubwa za kimataifa. Baadhi wanaamini mfumo wetu bado ni imara isipokuwa taarifa hizo nyeti, mara kwa mara hazitumiki ipasavyo au hupuuzwa kabisa. Hoja hii ni nyepesi mno na binafsi siamini hivyo. Mfumo wa kiusalama ambao una mianya inayotoa fursa kwa taarifa zake nyeti zilizokusanywa kwa njia hatari na gharama kubwa kutotumika hata kama zinabeba maslahi ya nchi, huo ni mfumo dhaifu.

Mfumo wa namna hiyo unapaswa kuvunjwa au kufanyiwa marekebisho makubwa. Mfumo wa kiusalama lazima si uwe na uwezo mkubwa wa kusaka taarifa nyeti kwa njia yoyote (halali au kinyume chake), lakini pia unapaswa kujijengea mazingira ya kuhakikisha matumizi bora ya taarifa hizo kwa maslahi ya nchi. Kwa mfano, mapungufu ya ujasusi wa kiuchumi pamoja nakuwa na mfumo ambao si imara kwa sasa wa kukusanya taarifa, yameibuka madudu mengi kwenye mchakato wa ubinafsishaji. Hata ukiangalia michakato mingine muhimu kwa taifa mikono ya kitapeli imeshindwa kudhibitiwa, kwa nini? Ni dhahiri mfumo wetu ni dhaifu isipokuwa swali la kujiuliza; je, udhaifu huo uko kwenye eneo gani mahsusi? Je, ni eneo la ukusanyaji taarifa au ni matumizi ya taarifa husika? Au vyote viwili? Ndani ya maswali haya, ufumbuzi muhimu unaojitokeza ni kwamba; tunahitaji mfumo imara zaidi wa kiusalama nchini na hasa kwenye eneo la uchumi na siasa kama ilivyo kwa Urusi ya Yeltsin kwa wakati ule.

Mfumo ambao si tu utakusanya taarifa kwa mujibu wa mahitaji lakini pia taarifa hizo zitajengewa mazingira ya lazima ili kutumika kwa manufaa ya nchi. Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na mfumo ambao utekelezaji wa taarifa zake unategemea upeo wa kiongozi mkuu pekee, ingawa pia Rais ni taasisi. Tujenge mfumo ambao ingawa utahitaji wanasiasa, wachumi, wahandisi, wanasheria na wanataaluma wengine lakini kamwe usiwe na maslahi ya moja kwa moja na makundi hayo wakati wote. Kwa sasa, inawezekana mfumo wetu umefungamana zaidi na utashi wa baadhi ya wanasiasa kuliko utaifa. Tunahitaji kujenga mfumo mpya imara wa kiusalama ambao utakuwa karibu na taaluma zote nyeti lakini hautafungamana na maslahi ya taaluma hizo wala wanataaluma husika.Hii itasaidia kujenga mwelekeo wa taifa katika mazingira halisi ya mwelekeo wa dunia na si mazingira ya utashi wa wanataaluma au wanasiasa husika.

Kwa bahati mbaya, mfumo wetu wa sasa umejenga hisia kwa umma umetekwa na wanasiasa na zaidi, ni mfumo uliowekezwa katika siasa kuliko eneo la uchumi. Chombo chetu hiki lazima kicheze vilivyo na kwa ustadi disko la dunia kuhusu uchumi zaidi na si siasa pekee. Hisia kwamba mfumo wetu wa kiusalama ni dhaifu zina ushahidi. Pale tulipopaswa kudhibiti au kuchukua hatua kabla, tumeshindwa kufanya hivyo na hatimaye kufikwa na madhara yasiyo ya lazima. Matapeli wasiojaa hata mkononi wanaingia popote na kufanya wizi wa mali za umma. Wengine wanafanya hivyo wakijiita wawekezaji wa kimataifa ambao baadhi ya makuwadi wao ni wanasiasa au wataalamu wetu mashuhuri nchini.Kama tunafeli kudhibiti masuala yaliyoko ndani ya uwezo wetu tutawezaje kupanga na kutekeleza mipango ya kupata taarifa nyeti kutoka kwa mataifa mengine ili tujenga taifa bora zaidi katika ushindani wa kidunia? Kwa nini hata wale wanaojifunza au kuchipukia kwenye utapeli wa kimataifa (wawekezaji), Tanzania iwe sehemu yao ya mazoezi?

Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.......

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni 80,000/= tu.

Piga simu 0715865544 au 0755865544 popote ulipo utaletewa...

Na Yericko Nyerere

HABARI,
"Yericko Nyerere,
Asante kwa uchambuzi wako mzuri Juu ya swala hili umetoa hoja nzuri iliyotulia na inayoeleweka pia kwa Kitabu chako sijakisoma ila nilishakisikia sifa zake na sasa ndio wakati wakekusomwa nawatu nitakupigia nitume pesa nitumiwe nikisome.
Ila nina swali moja tu kwa hizi kazi za Idara Hiyo ulizozitaja kukusanya na kuchambua taarifa (intelligence gathering and analysis) na kuzipeleka/kushauri wahusika kuchukua hatua."
Kwani ni mambo gani hayo je ya uchumi hayapo na kama yapo niya ndani tu sio na nje kama Rais anavyosimamia Mambo ya Madini umetaja Tanzanite Mh.Rais ametaja kabisa haiwezekani India waongoze wakati sisi ndio Chanzo ina maana Hata kenya anajua sasa ndio anafanyia kazi je hiyo siyo Ujasusi wa Uchumi.?
Kwa maelezo yako
Asante,

LUMUMBA
 
Nakushukuru Mkuu wangu,

Mambo hayo ukiisoma sheria yote hakuna panapoonyesha Idara itafanya shughuli za kiuchumi, vifungu vyote vya majukumu ya TISS vinaeleza katika mambo ya jinai na usalama tu, hakuna diplomasia ya uchumi wala popote panapoeleza juu ya uchumi...

Kwa sehemu kubwa ya matokeo yanayotokea leo nikwenye madini au kwenye miradi kama ya bomba la mafuta toka Uganda ni suala ambalo ni msimamo tu wa sponsor (rais), sio suala la kisheria.... Hoja yetu na ama msimamo wangu katika kitabu nikuwa hili lisiwe hisani bali liwe sheria, na litengenezewa ulazima wa kisheria wa kutumika kwa ripoti ya TISS katika Uchumi wa nchi wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
 
Nimekuelewa hoja yako tayari ngoja nikisome kitabuchako nitarudi tena kwako kwa maswali juu ya kitabu chako tena tegemea mengi kwakuwa hapa ni wigo wa kuelimishana kuna mtu tayari ananisaidia kukipata toka kwenu.
Ila nina swali lingine kwa mfano marekani kuna idara za usalama ninavyojua mimi tatu CIA,NSA na FBI na hiyo kazi ya ujasusi wa kiuchumi hasa wanafanya CIA sina hofu kwa hilo wewe unajua sasa mimi nauliza kwako je hufikirii isianzishwe idara nyingine iwe ni kwa kazi hiyo tu duniani vita vya uchumi ni vikubwa sana hata MH.RAIS alisisitiza hilo.Ili kazi ya jinai na usalama vibaki kwa TISS.

Ni moja ya wazo zuri ulilolipendekeza...nakubaliana nawe, kama ndani vilivyo anzishwa vitengo vya kupambana na uhalifu wa mitandao, basi ni wakati wa kuanzisha idara mpya ya mambo ya uchumi
 
Sasa hivi hamtaona siku haya mapigo yakiwarudi mtaona bila kuambiwa
Hapa tatizo lipo kwa anaye pendekeza mabadiliko hayo, kichwani ana perception ya kwamba serekali inapingwa/inashurutishwa,.........Amini nakwambia kama serekali itaanzisha mabadiliko hayo huyo jamaa ataiunga mkono.
 
Back
Top Bottom