Nape: Watanzania kuanza kukopeshwa Smartphone

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,289
222,349
Waziri wa Habari Mh Nape Nnauye amesema , Serikali inaangalia uwezekano wa kushawishi Makampuni yanayotengeza Simu , au mawakala wao ili wawe wanawakopesha simu wananchi na kuwakata fedha kidogo kidogo .

Amesema inakuwa vigumu kwa Mtanzania Mnyonge kulipa sh. laki 3 taslimu ili kugharamia manunuzi ya smartphone , hivyo mpango huu utawawezesha wengi kumiliki simu hizo .

Bali sisi wengine tulidhani labda serikali ingekuja na Mpango wa kuwawezesha wananchi kwenye Pembejeo au mitaji ya biashara ili waweze kujikomboa kiuchumi , lakini badala yake inataka kuwawezesha kwenye Smartphone ambazo wakishakuwa nazo haijulikani ni nani atakayewanunulia vocha ili waweze kuingia mitandaoni .

Nakulilia Tanzania .
 
Hebu nchi yetu viongozi wawe serious kidogo,unawaza kukopesha smartphone kweli? Kilimo hoi, ufugaji hoi,maisha ya wananchi ni ya kubangaiza.....tumemkosea nini Mungu sisi watanzania mpaka tunakuwa na Viongozi wenye mawazo mgando?

Inachosha sana hasa kwa wale ambao tumepita vijijini huko na tumeona maisha halisi ya mtanzania yalivyo duni.
 
Huu ubunifu wa hawa viongozi wetu wakati mwingine huwa majanga tu, anataka smartphones zijae mpaka vijijini halafu bando ziendelee kupanda bei kila siku, hawa inawezekana kweli wanamiliki hisa kwenye makampuni ya simu.
 
Mwambieni huyo kuwa wakulima tunataka mikopo ya pembejeo na wanafunzi vyuoni wanataka mikopo kamili na siyo hii isiyotosheleza!
 
Waziri wa Habari Mh Nape Nnauye amesema , Serikali inaangalia uwezekano wa kushawishi Makampuni yanayotengeza Simu , au mawakala wao ili wawe wanawakopesha simu wananchi na kuwakata fedha kidogo kidogo .

Amesema inakuwa vigumu kwa Mtanzania Mnyonge kulipa sh. laki 3 taslimu ili kugharamia manunuzi ya smartphone , hivyo mpango huu utawawezesha wengi kumiliki simu hizo .

Bali sisi wengine tulidhani labda serikali ingekuja na Mpango wa kuwawezesha wananchi kwenye Pembejeo au mitaji ya biashara ili waweze kujikomboa kiuchumi , lakini badala yake inataka kuwawezesha kwenye Smartphone ambazo wakishakuwa nazo haijulikani ni nani atakayewanunulia vocha ili waweze kuingia mitandaoni .

Nakulilia Tanzania .
Nape kumbe yuko wizara ya kilimo..!! 🤔
 
'
JamiiForums470129845.jpg
 
Back
Top Bottom