Martin Maranja Masese
Member
- Apr 24, 2011
- 29
- 542
Airbus Helicopters H225 ina horsepower 1,820, inatumia mafuta ya Jet-A1. Wastani inakunywa 540 us liquid gallons/hour=2,044.122 litres/hour. Gharama za kujaza pale JNIA ni US$3.612 (Shs. 8,390.87) per Gallon in USD. Zingatia 1 us liquid gallon=3.785 litres leo. Piga hesabu zako.
Hivyo kwa saa moja tu hiyo chopa hii inaweza kutumia wastani wa Shs. 4.53 milioni kwa safari ya saa moja angani kwa mafuta yake tu. Sijaweka gharama nyingine, maana lazima irukee ikiwa na operators wawili. Sifahamu kama operators wanalipwa na JWTZ au wizara, lakini zitakuwa fedha za umma
Naona taarifa hapa inaeleza ndugu Nape Nnauye atakwenda mikoa yote kuhamasisha uwekaji anuani za makazi (postikodi). Na leo Nape Nnauye ameanza kuruka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Shilingi ngapi zitatumika katika kurusha hii chopa ya JWTZ? Nani atagharamia hizo fedha?
Kwanini watendaji huko chini wasiagizwe kusimamia zoezi la postikodi? Kuna wakuu wa mikoa, makatibu tawala mikoa, wakurugenziwa majiji, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tarafa, watendaji wa kata na vijiji. Waziri wa kazi gani na chopa?
Watasha wana msemo wao mzuri, wanasema “The bigger the helicopter, the larger its engine or engines and the more thirsty they become.”. Ndugu Nape ulipaswa kwanza kujiuliza hili swali “How much fuel does my bird burn per hour?”. Halafu ukipata jibu ndiyo uanze kuchoma fedha zetu
Helicopter ambayo inaweza kusafiri umbali mrefu kwa muda mrefu inahitaji mafuta mengi. Helicopters nyingi zina matenki yenye kubeba mafuta yatakoishi wastani wa saa 1.5 hadi saa 3 na dakika 20 za ziada. The Sikorsky S92 and the Agusta A139 zina matenki ya ziada. Pigeni hesabu.
Wakati huu wa mdororo wa uchumi na gharama za maisha kupanda, serikali ilipaswa kupunguza kuleta Supplementary Budget kusaidia wananchi, kuondoa tozo kadhaa (hata kwa miezi 6 tu) haswa katika bidhaa za mafuta yenye tozo 23 na serikali kupunguza matumizi yake ya ANASA.
Wakati nchi nyingine zinasaini Supplementary budgets (bajeti ya nyongeza) ili kuwapunguzia wananchi wao ukali wa maisha, waziri wa Tanzania anakwenda kufanya ziara (kuhamasisha uwekaji postikodi) isiyokuwa na ulazima ambayo kwa saa moja pekee itagharimu karibu Shs. 5M.
Mfano, leo wananchi wa Tarime, wanannua mafuta ya Petroli lita 1 kwa Shs. 3,000. Kwamba ukiwa na Shs. 20,000 utapata lita 6. Nape Nnauye kwa kuwa ni waziri, analipwa pesa za umma, anaamua kufanya ziara nchi kwa helicopter? Wakati kama huu? Hayo ni matumizi ya ANASA na dhihaka.
Siyo kwa ubaya, nauliza tu, Nape Nnauye mnaona hii ni sawa kutumia fedha za umma hivi? Zoezi la postikodi limefika 68%, lipo pazuri. Waziri anakwenda kumpa hamasa nani kwa gharama zote hizi? Acheni kuchezea pesa zetu. Hatujasahau upigaji wa HK kwenye urithi na HK chalenji
MMM, Martin Maranja Masese
View attachment 2183961