Mimi si mshabiki wa chama cha siasa, ila huwa ni mshabiki wa wanasiasa. Kati ya watu ninaowashabikia ni walikuwa hawa wote wawili, hata wakati ule wote wanagombea Ubunge hapo Ubungo, nilikuwa nasikitika sana maana niliona majembe yote mawili yako pamoja, na kwa vyovyote mmoja angekosa, kitu ambacho kweli kilitokea. Ushujaa aliokuwa nao Nape sijui kama ulikuwa wa kweli au alikuwa hivyo baada ya kukosa madaraka ndani ya chama. Maana nakumbuka wakati huo alimlipua Lowasa juu ya ujenzi wa jengo la Umoja wa vijana wa chama chake. Baada ya kumweka sehemu amabayo anasaini malipo ya posho mbali mbali, amejisahau na hata ushabiki wangu kwake umeisha. Mnyika yuko juu sana kwa huyu Nape. Nahisi hata maisha yake nje ya hiyo nafasi aliyonayo ni magumu sana. Awe kama wenzake walioko ndani ya chama chake ambao wanaangalia maisha yao ya baadae.