TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Chama Cha Mapinduzi kila mwaka huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Februari 05, 1977. Mwaka huu kitakuwa kinatimiza miaka 39.
- UZINDUZI
- KILELE CHA SHEREHE
Viongozi wa kitaifa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria watapangiwa shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa kwa ujumla katika wilaya zote za mkoa wa Singida siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho hayo.
Mikoa yote iandae shughuli mahsusi kwa wiki nzima ya maadhimisho hayo, mkazo ukiwa ni kufanya shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa katika maeneo yao, Mambo ya kuzingatia katika wiki hiyo ni kama ifuatavyo:-
i. Kuingiza wanachama wapya wa CCM na Jumuiya zake na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama.
ii. Kufanya mikutano ya kuwashukuru wana CCM na wananchi kwa kuiamini CCM kuendelea kuongoza Nchi yetu kwa kushiriki na kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CCM ilipata ushindi wa kishindo wa Rais, Wabunge na Madiwani.
iii. Kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
iv. Kushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, upandaji miti, uchimbaji wa mitaro ya maji, kufanya usafi wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za kijamii.
- KAULIMBIU
Nape Moses Nnauye (Mb.),
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
13/01/2016
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
13/01/2016