Nape, usipolichukulia MwanaHALISI hatua utakuwa una chuki binafsi

jamiiyamtimkavu

JF-Expert Member
May 20, 2011
274
192
Wana jukwaa heshima kwenu.

Niende kwenye hoja.

Gazeti la leo la Mwanahalisi limeandika taarifa ya uchochezi, kudhalilisha na kuchonganisha. Nikiwa kama mkazi wa Dar es salaam imenikwaza sana.

Kuna aya nyingi zinazosema '' Daudi (Makonda kwa sasa)" huu ni udhalilishaji, Nape upo kimya kwa nini? au bado una bifu la wem#?

Daudi (Makonda Kwa sasa) alipata sifuri (division zero). Makonda amekana juzi kwenye kikao cha RC hajawahi kupata zero,unataka nini ili uchukue hatua.

Hivi ungekuwa umeandikwa wewe mh Nape ungekaa kimya?

Na usipolichukulia hatua juu ya hii habari, nitaamini unayoyafungia ni kwa sababu ya chuki.

Msijibu kwa jazba tushee mawazo

Nawasilisha
 
Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo. Haki ya nani wanamuziki wa zamani walikuwa na maono!

IMG_3845.JPG
 
Mnaoyakuza ndo wachochezi tena mnatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu, au kisa kataja Tanaka tawala ndo shida? Tafuteni hoja za msingi acheni uchochezi.

Mkitaka mwambie mweshimiwa ajitokeze na magamba mbele ya waandishi wa habari ndo tuelewe nani mkweli na nani mwongo vinginevyo mnafanya mchezo wa kuigiza. Sheria ni msumeno na hakuna aliyejuu ya sheria.

Suala la uhakiki wa vyeti si kwa ngazi za chini hata kwa hao walio juu japo wapo chini kwenye sheria. Tafuta hoja usilete ushabiki wa kitoto. We need a concrete document.
 
Gazeti limeandika vizuri na limefanya utafiti mzuri kabisa na kuweka quotations, na kuminya sources nyingine za habari. Na limesaidia kuondoa mjadala wa kweli si kweli. Sasa kama habari ya gazeti haiaminiki, ni vyema mhusika akapinga kwa kuelezea historia yake ya kielimu kinagaubaga huku akitiririsha vyeti original.
 
Back
Top Bottom