Nape: Tofauti ya kipato inahatarisha amani

Shenkalwa

JF-Expert Member
May 3, 2011
580
132
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) itikadi na uenezi ya chama cha mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema ipo haja sasa kujadili kwa kina namna ya kupunguza tofauti kubwa ya kipato iliyopo kati ya maskini na matajiri kwani ni hatari kwa amani ya nchi.

Alisema hayo kwenye viwanja vya Sokoni Igoma jijini Mwanza wakati akihutubia mkutano ulioandaliwa na ccm katika ziara ya baadhi ya viongozi wa chama hicho mkoani hapa.

Nape alisema nchi nyingi duniani zimekuwa zikikumbwa na machafuko kutokana na kuachiwa kukua kwa tofauti kubwa ya kipato kati ya maskini ambao ndio wengi na matajiri wachache.

"ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji...Heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Ni muhimu leo wapenda amani wa nchi hii tujadili kwa kina namna bora ya kupunguza tofauti kubwa ya kipato nchini kwani ikiachwa hivi baada ya muda nchi hii itachafuka," alisema Nape.................."

Source: NIPASHE October 20, 2011.

Huyu jamaa sijui kama anaelewa anachokiongea naona mimi nashindwa kumpata kabisa. Sio katika mkutano huo tu lakini maneno anayoyaongea katika mikutano yake mingi simuelewi analenga nini.

Ukichukulia kwa mfano watu aliokuwa anaongea nao huko Igoma, Mwanza kwenye viwanja vya sokoni ni hao maskini na walala hoi ambao kwa namna yeyote maneno hayo ya nape hayawasaidii zaidi ya kupoteza muda wao kumsikiliza.

Mimi kwa mawazo yangu niliona bora angeliongea maneno hayo kwenye mikutano ya viongozi wenzake wa magamba kwa sababu wao ndio wanaoipeleka nchi hii kubaya, ndio mafisadi, ndio waliosababisha hilo pengo kati ya matajiri/mafisadi na masikini walalahoi. Hao ndio wanaotakiwa watafute namna ya kurekebisha mambo, kuinua uchumi wa wananchi na kuwafunga mafisadi na wezi wa mali ya umma wote.

Yeye na chama chao ndiyo walioifilisi nchi hii kwa kujilimbikizia mali ndani na nje ya nchi hii pamoja na kujijali wenyewe na familia zao na kuwaacha walio wengi wakitaabika kwa mlo mmoja kwa siku.

Sasa leo anakwenda kuwaambia walalahoi wa igoma Mwanza maneno hayo ambayo hayawasaidii. Tena naona kwao ni kama kejeli. Sijui kama huyu bwana mdogo ana uwezo kweli wa nafasi aliyopewa na magamba wenzake.
 
Aache unafiki kama ana anaimanisha anachoongea basi aache kutumia gari la kifahari analotumia kwa sasa
 
Anayajuwa leo? Magamba bwana usanii tu kila siku. Tulipokuwa tunasema gap baina ya maskini na matajiri linakuwa haraka kuliko inflation na ni hatari kwa nchi walikuwa wanaona watu wanalalamika tu. Leo ndio anaona umuhimu.
 
nadhani alikua anapoteza muda wake.....maana mm navyowafahamu wakazi wa igoma ni watu ambao kwa sasa wameshabadilika sana...ndio maana wakaamua kumpa udiwani kijana wa chadema miaka 25 na kumwacha mzee wa magamba miaka 50.....igoma ni mji ambao unakua kwa kasi sana na unahitaji viongozi makini.....hili la nape kuhutubia mkutano pale ni kazi bure......peeeeeeeeeeelz..............power
 
Kama yuko serious aifanye agenda kwenye CC na aisimamie ipite mpaka NEC ikisubiri mkutano mkuu. La sivyo ni porojo tu.
 
Anaimba wimbo na kucheza mziki uleule anaoukataa kila siku. Wananchi wakielezea kutoridhishwa na namna serikali ya ccm inavyowahudumia wananchi, yeye anapinga na kudai serikali imefanya mengi makubwa katika miaka 50 ya uhuru. Ni huyuhuyu Nape aliyeandika katika facebook wall yake na anaendelea kuhubiri: "Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele", upuuzi mtupu.

Nilimsikia gamba kuu jana, EL, akilalama eti uchumi umeporomoka na vijana hawana ajira na kwamba hilo la ajira kwa vijana ni bomu. Upuuzi mwingine! Ni huyu huyu Lowasa aliyewahi kusema uchumi unapaa na serikali ya ccm 'inatekeleza ilani' kwa makini. Leo anataka madaraka anajifanya kuwajali vijana, Kikwete alijifanya kijana mwenzetu 2005 leo ndo huyu kaitumbukiza nchi kaburini. Wote hawa hawana nia njema kwa taifa letu, tuwaambie bila kificho wala kuwaonea haya kwamba HATUDANGANYIKIIIIIII........
 
Nape anaimba nyimbo kwa lugha asiyoifahamu. Ni kama mbongo anavyokomaa kuimba na kucheza wimbo wa lingara bila kujua maana yake.

Kama anafahamu hicho anachokiongea kwa wananchi wa igoma, anatakiwa aongee na mwenyekiti wake afanye jitihada za kudhibiti inflation ili maisha ya wananchi yasizidi kuwa magumu.
 
Nape anaimba nyimbo kwa lugha asiyoifahamu. Ni kama mbongo anavyokomaa kuimba na kucheza wimbo wa lingara bila kujua maana yake.

Kama anafahamu hicho anachokiongea kwa wananchi wa igoma, anatakiwa aongee na mwenyekiti wake afanye jitihada za kudhibiti inflation ili maisha ya wananchi yasizidi kuwa magumu.



Mkuu,
Ungemsikia mkulo jana ungepatwa na kichefuchefu kama nilichopata mimi! Eti inflation imeongezeka kutoka 14 hadi 16pc lakini Tz ndio nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa sana ndani ya EAC kwa 7pc mfululizo!!? Nilijiuliza uchumi unakuaje sambamba na inflation, nikajikuta nabanwa na haja nikaishia toilet!
 
Back
Top Bottom