Nape TBC: Anawajua samaki walioko majini vema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape TBC: Anawajua samaki walioko majini vema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jan 19, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  "Samaki ukimtoa majini hana nguvu, chama ni taasisi na kina nguvu, ukitaka kuwa na nguvu inabidi uwe ndani ya chama, bila chama mwanasiasa huwezi kuwa na nguvu, tutawatoa majini hawa" Nabe Mnauye, Jambo Tanzania, TBC 19 January 2012.

  Ni muda sasa tangu Magamba mpaka sasa Samaki. Sijui nini kilichotokea Magamba yakawa shida kuyatoa ssa sijui wamegunduaje kuwa magamba ya samaki hayatolewi akiwa anaogelea majini lile lilikuwa wazo la kitotot, sasa wanataka kuwatoa majibi wanawafahamu samaki wenyewe vema ili wajue jinsi ya kuwatoa majini? maana wasije wakaishia pabaya wao...

  Kama kijana nampongeza kwa nguvu ya kauli anazozitoa ila ninamtaka aongeze nguvu ya kupata support ya wazee waadilifu maana shida ni tumeshuhudia akitoa kauli zenye nia njema tu kuboresha chama lakini samaki haohao wamekuwa wakimbeza na kumfanya wakati mwingine aonekane kituko
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Ama hakika nguvu ya Mamba iko Kumayi kumchanga anaburuta!!
   
 3. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nape watakutowa uhai uwe makini kitumbuwa cha watu
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kijana angalia papa havuliwi na ndoano.
   
 5. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,203
  Trophy Points: 280
  Nimemsikiliza vizuri sana leo. kweli alikua anaongea pointi nzuri sana. Lakini hofu yangu tu ni kwamba hawa samaki wanaotaka kutolewa baharini je uwezo wa kuwatoa wanao?.
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  I've once said this, and am saying it again. Ukitaka kutupa mtu nje ya ghorofa kuwa makini, mkaenda wote au balaa zaidi utupwe wewe uwaache wenzio.
   
 7. d

  davidie JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape anashindwa kuelewa kuwa yeye katika hao samaki ni dagaa tu je anaweza kuwatupa nje ya maji hao papa? aangalia mfano wa dhana ya kujivua gamba kule dodoma alikuaje mpole? asitake kuleta hadithi ya mwanga wa mshumaa ambao unawaka kwa kiburi cha kuondoa giza mwisho wa siku unaangamia na ukizimika tu giza linaendelea
   
 8. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Nape akae akijua kuwa kwenye maji si samaki pekee, hata nyangumi wapo, asifikiri technics za kuvua samaki ndo zile zile za kuvua papa na nyangumi.


  By the way Nape he is good boy.
   
 9. S

  Sakaja Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape acha kudanganya watanzania,ww mwenyewe ni mmoja wa vijana ndani ya ccm ambao unasumbuliwa na tamaa ya kutafuta umaarufu,mawazo unayotoa si zakwako ni la kundilinalotafuta madaraka.Nani asie jua kuwa tatizo la kwanza la ccm ni uwezo mdogo wa mwenyekiti wake,kila kukucha jina lingine mara magamba na leo hi samaki,wafukuzeni kama kweli mna uwezo.Nikueleze kama CCM ni maji yanayotunza samaki wa namna hiyo basi dawa ni kukausha hayo maji ili wafe na sio kuwa dimbwi pembeni(ccj),ww ndani ya hayo maji nimdudu tu na hujawa hata dagaa.NAPE NAUYE tumekuchoka sana na danganya toto zako.
   
 10. naninibaraka

  naninibaraka JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  huyu anaongea utumbo,hajui wajibu wake ndani ya chama,si alisema ataweka hadharani sms zote alizokuwa anatumiwa na jk kumtukana lowassa,mbona mpaka leo hajafnya hivyo? sijaona hata agenda moja waliofanikisha,kapewa vx new model na driver kazi sifur anabaki kuvaa cheni kama bwabwa....tumechoka kusikia upuuzi wao>....
   
 11. F

  Fahari MJ JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 425
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kma unawajua samaki wa sangara za ziwa victoria miaka ile ya zamani walikuwepo wakubwa sana wengine kama size ya mtu mzima....... mpaka kilo 30.

  asa Nape kama anategema Kuwatoa hao samaki "sangara" kwa kutumiamia Ndoano asahau. Asije aauta anazidiwa nguvu nasangara ananvuta majini. Ndano itawachomoa Sato tu . Wale sangara wanahitaji nyavuboti za uvuvu zlizojipanga vema.

  Tena hata sangara nimekosoea huyo wanyetakaiwa kumtoa ili "baharini" yaani CCM iwe safi ni "Nyangumi
   
 12. chizi1

  chizi1 Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape hana sera, notin new.. Samaki, magamba, kuwakomesha story tu. Anajazwa ujinga ikulu, anakurupuka. Hafikirii,hana strategy, hana agenda wala targets.

  Kwangu mimi naona he is a failure in life, he is a failure in his position and he is failing the party and killing it.. Akiguswa kdogo anakurupuka. Hana vision ya aina yoyote.
   
 13. J

  Jalem JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kijana mwenzetu Nnauye, sikwasababu baba yako alikuwa one of mafisadi wa chichini enzi hizo, napenda kukwambia kuwa ukisikia mbwa anapiga kelele saaaaaaana ujuwe ni muoga anajihami adui asifike karibu, kama unauwezo wakuwatoa samaki majini je, ni samaki wapi? labda wakuwafuga sebuleni lkn siyo wale ambao ushahidi unao au huna lakini uwezo huna wakufanya lolote, na pia nakuhakikishia kuwa one day utachukiwa na kundi kubwa sn kwa kubwabwaja maneno badala ya kutekeleza ki intelegensia, kama unaushahidi kuw avijisent ni mali ya wa Danganyika umeshindwa kumtoa kafara? kama ELnae unaushahidi fanya wacha poroja za kila siku au unataka kuwa Mwakiembelise nini? wacha fanya tuone siyo kuwa shekhe yahaya kutabiri tu na mwisho utabiri usitokee, juu yako, unajikusanyia maadui kwa wingi kuliko mrafiki.
  be watchfull with ur lips.
   
 14. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Haya tusikie Propaganda Mpya "Kuvua Samaki" nimependa hiyo ya ukivua samaki lazima uwe na mbinu na umjue samaki unaemvua, usije ukaenda na ndoana ya papa, Nyangumi akaidaka ukadhani umevua papa mkubwa ukang'angana nae mwisho unatumbukia wewe baharini, afu kuogelea umeanza juzi tu wenzako wameishi humo maisha yao yote
   
Loading...