MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Wanasiasa wa CCM wanaojiunga kwenye upinzani hunikumbusha watu ambao husilimu au kuokoka. Hawa huwa wanavamia dini kuwashinda wale ambao wamekuwa kwenye dini hiyo kwa muda mrefu. Hudhani wao ndio wanajua ukweli wa kiimani zaidi ya waumini waliokulia ndani ya dini.
Lowassa alipoingia ndani ya upinzani alisikika akisema yeye ni safari ya matumaini kwa wapinzani huku akirudia rudia maneno ya Mwl. Nyerere yanayosema ‘’Wananchi wakiyakosa mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM’’.
Lowassa akawaaminisha mashabiki wake kuwa kwa uwezo wake CCM itaondoka madarakani saa mbili asubuhi tu siku ya kupiga kura za Ubunge na Urais. Now, two years down the line, hata nguvu zake za kisiasa zimeanza kupotea huku washabiki wake wakitaka apumuzike na aache kufikiria kugombea Urais. Kwa sasa macho, masikio na matumaini yako kwa Lissu!
Sumaye alipoingia ndani ya CHADEMA tarehe 22 August 2015 alisikika akisema ameenda kuwafundisha wapinzani jinsi ya kuendesha siasa na serikali kwa sababu hawana uwezo na uzoefu. Kwa sasa badala ya kuwafundisha wapinzani jinsi ya kuendesha siasa na serikali, hao hao wapinzani kwa sasa wanamfundisha jinsi ya kuwa mvumilivu katika siasa za upinzani wakati chama tawala kinakumamua! Kutoka Waziri Mkuu ndani ya serikali kwa miaka 10 mpaka kuwa mwenyekiti wa Mkoa/kanda sio kazi ya kubezwa!
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru baada ya kuondoka CCM na kupanda kwenye jukwaa la UKAWA aliibuka na kauli inayosema CCM imechoka na kuishiwa pumzi na kwamba haina uwezo wa kuleta mabadiliko yanayohitajika kuiokoa nchi. Miaka miwili imepita, kinachotokea ni yeye kuchoka mpaka hata kupanda kwenye jukwaa la upinzani hawezi.
Lazaro Nyalandu imeibuka kwenye upinzani na gia ya hoja ya Katiba Mpya. Jana nimemsikia wakati akiwa Mwanza akitoa hotuba ndefu lakini dhima yake ni kuonyesha kuwa yeye ndiye atahakikisha mchakato wa kuandika Katiba mpya unafanyika. Anaongea kama vile hakuna katika upinzani wenye uwezo au waliokuwa na uwezo wa kushinikiza serikali ili iweze kurejesha mchakato wa Katiba.
Kwa sasa kila baada ya saa moja anaposti andiko kwenye facebook na twitter kuonyesha uwezo na nguvu alizonazo katika kuleta ''ukombozi'' nchini.
Huyu naye siyo siku nyingi atapotea kisiasa kama ambavyo wengine kutoka CCM wanapotea mpaka wanaamua kujiondoa upinzani au kurudi CCM.
Wakati akihojiwa na TBC tarehe 19 January 2012, Nape Nnauye aliwahi kusema, CCM na wanasiasa wake ni sawa kama maji na samaki.
"Samaki ukimtoa majini hana nguvu, CCM ni taasisi na kina nguvu, ukitaka kuwa na nguvu inabidi uwe ndani ya CCM, bila CCM mwanasiasa huwezi kuwa na nguvu’’ alisema.
Kwa haya yanayojitokeza kwa wanasiasa kutoka CCM kwenda upinzani siwezi kudharau maneno ya Nape Nnauye!
Hata kwa Lazaro Nyalandu muda utatoa jibu sahihi.