Nape: Sijayapata matokeo ya Serikali za Mitaa ya Sumbawanga

Nape: Sijayapata matokeo ya Serikali za Mitaa ya Sumbawanga

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
1,488
Reaction score
2,762
akiulizwa nape na mwaandishi kwanini mmepoteza viti vingi huko sumbawanga katika hali ya kushangaza nape alisema bado hajapata matokeo ya huko.je ni kweli nape hajapata matokeo au alikuwa anakwepa swali?
=====================

UKAWA wailiza CCM Sumbawanga
mt2-300x275.jpg

Sumbawanga,

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeigaragaza vibaya CCM katika uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana katika kata tatu za Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Chadema ni miongoni mwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na vyama vya CUF na NCCR Mageuzi.
Vyama hivyo viliweka makubaliano ya kushirikiana kwenye uchaguzi kwa kuachiana maeneo ambayo kuna chama kati yao kina nguvu.
Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, CCM iliongoza kwa kupata jumla ya mitaa na vijiji 9,406, huku vyama vya upinzani vikigawana nafasi 3,211.

Uchaguzi huo wilayani Sumbawanga ulirudiwa baada ya kuahirishwa kutokana na kasoro zilizojitokeza.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana na msimamizi wa uchaguzi huo, Hamid Njovu, Chadema wameshinda viti 37 na CCM wakiambulia vitano tu kati ya mitaa 43 ambayo uchaguzi wake ulikuwa ukirudiwa katika kata za Msua, Chanji na Kizwite na mitaa miwili ambayo pia uchaguzi wake ulivurugika awali.

Njovu alisema uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti katika mtaa mmoja wa Nankasi, Kata ya Chanji, utarudiwa Jumapili baada ya kura kugongana.

Alisema katika Kata ya Kizwite mitaa iliyofanya uchaguzi ilikuwa 15, ambapo Chadema ilishinda mitaa 13, huku CCM wakiambulia miwili.

Katika Kata ya Msua, mitaa iliyofanya uchaguzi ilikuwa 13 ambapo yote ilikwenda Chadema na CCM kuambulia patupu.

Njovu alisema kwa upande wa Kata ya Chanji yenye mitaa 14, Chadema imeshinda 10, wakati CCM imepata mitatu. Mtaa mmoja uchaguzi utarudiwa.

Aliongeza pia uchaguzi wa marudio kwenye mitaa miwili, kila chama kiliibuka na ushindi katika mtaa mmoja, ambapo CCM ilipata ushindi Mtaa wa Bangwe, Kata ya Izia na Chadema ikishinda Mtaa wa Tambazi katika Kata ya Sumbawanga.

Uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa tofauti na ilivyokuwa awali Desemba 14 mwaka jana ambapo ulivurugika katika kata hizo kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza, ikiwa pamoja na vituo kuchelewa kufunguliwa.

Hali hiyo ilisababisha wananchi waliokaa vituoni kwa muda mrefu wa zaidi ya saa nane wakisubiri kupiga kura kuhamaki na kujichukulia sheria mkononi kwa kuchoma moto ofisi ya mtendaji wa Kata ya Kizwite na Kata ya Chanji na kuteketeza nyaraka zote muhimu za kupigia kura.

Hivyo kufanya mchakato mzima wa uchaguzi huo kurudiwa upya kuanzia kujiandikisha hadi upigaji wa kura.

Akizungumza baada ya matokeo hayo, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Sumbawanga, Zeno Nkoswe, aliwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wingi kupiga kura na kufanya chama chao kuibuka na ushindi wa kimbunga kiasi hicho na kudai huo ni mwanzo wa kuelekea ukombozi wa taifa hili kutoka mikononi mwa CCM ambayo inatumia vibaya rasilimali na maliasili za nchi kwa kunufaisha mafisadi.

Naye Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya hiyo, Clement Bakuli, alisema wameyapokea matokeo hayo kwa masikitiko makubwa, lakini katika mpambano wowote lazima mshindi apatikane, hivyo chama kitakaa kufanya tathmini kuona wamekosea eneo gani ili waweze kujirekebisha kwa uchaguzi ujao.

Timu nzima ya CCM ngazi ya wilaya ikiongozwa na mwenyekiti wake, Emmanuel Kilindu na Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly, walipiga kambi na kufanya kampeni za nguvu katika kata hizo.

Akizungumzia matokeo hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, alisema ushindi huo ni mwelekeo wa anguko la CCM nchini.

"Ushindi huu mkubwa ni mwendelezo wa anguko la CCM na ni motisha kuelekea hatua ya Ukawa ya kutoshiriki kura ya maoni na badala yake kuelekeza nguvu katika kuhamasisha wananchi kuiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu mwaka huu," alisema Mnyika.

Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza ratiba ya uandikishaji wapigakura ukiwamo Mkoa wa Rukwa, huku akiwataka pia wananchi kuiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Kwa upande wake, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema hana taarifa na matokeo hayo, hivyo hawezi kusema chochote.

Chanzo:Mtanzania
 
Mkuu ilikuwa unatagemea Nape aseme ameyapata matokeo ya Sumbawanga wakati zile asilimia alizowahi kubwabwaja alikuwa amezikokotoa akiwa kwenye kiwanda cha ukokotozi cha Lumumba?!

Hivi kuna mtu Amesha wahi kumuuliza Nape Wamepata asilimia ngapi za ushindi wa magumashi wa kupita bila kupingwa na ushindi wa kushindina na vyama vingine ilikuwa asilimia ngapi?
 
2.jpg


Nape na Kinana wamekuwa na safari nyingi za kuzurura vijijini wakiwa na imani kuwa wanaimarisha chama, kwa matokeo haya wanatakiwa watoe maelezo ya kutosha kwa nini wasiwajibike.


 
Achana na ----- huyo kama anaweza aende kwao jimbo la Tandahimba akagombee kama atapita, mpumbafu huyo
 
Mbaya zaidi asilimia 80 ya waliopiga KURA walikuwa wamepewa kipaumbele na CCM cha kukipigia kura Chama Chao CCM bila kujua binadamu anabadilika na binadamu akielimika ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.Mjinga akielimika Muerevu kaa chonjo hii hawakuifikira kabisaaaaaaaaaa.Poor CCM
 
Ni Kweli Nape huenda hajapata Matokeo kamili ya uchaguzi wa marudio SM mkoa wa Rukwa. Tusimlaumu kwa kuwa amekiri hayuko informed.

Ni busara pia kumpatia matokeo kwa kuwa hawajapata.

Mwambieni matokeo yako hivi, Kati ya mitaa 44 Rukwa mjini, Chadema tumeshinda mitaa 39 sawa na asilimia [89%] na CCM mitaa 5 sawa na asilimia [11%]

Matokeo ya kushangaza, Kata ya Msua kulikuwa na Mitaa 13, CHADEMA wameshinda mitaa yote 13 na CCM hawajapata hata mtaa mmoja. Kabla mitaa yote ilikuwa ya ccm.

Kata ya Chanji kulikuwa na Mitaa 14, CHADEMA wameshinda mitaa 11 wakati CCM wakiibuka na ushindi wa Mitaa 3 tu. Mitaa yote 14 ilikuwa ya ccm.

Mpeni matokeo hata kwa sms aache visingizio vya kijuha.
 
hata dada
Lizabon hajapata matokeo
 
Last edited by a moderator:
Hahahaha kweli ukitaka kuwa kiongozi CCM ni lazima ujitoe ufahamu kama Nape, sasa hivi huyu Nape inamana hata mitandaoni haingi hadi asijue matokeo, au na yeye ni mhanga wa MB 8?
 
Nape na Kinana wamekuwa na safari nyingi za kuzurura vijijini wakiwa na imani kuwa wanaimarisha chama, kwa matokeo haya wanatakiwa watoe maelezo ya kutosha kwa nini wasiwajibike.
CCM haina kitengo cha watu weledi cha kupima matokeo ya ziara za viongozi wao, wanadhani ziara ni kuzurura mitaani na kushangiliwa na watu bila kuwa na lengo maalumu.

Ziara anazofanya Kinana vijijini haina faida yeyote kwa chama zaidi ya kuwanufaisha wapinzani wao, kazi anayofanya Kinana na Nape ni kuamusha waliolala waifahamu siasa zaidi hasa vijana, na wengi wa vijana wanaohamasishwa huishia kujiunga na upinzani.
 
akiulizwa nape na mwaandishi kwanini mmepoteza viti vingi huko sumbawanga katika hali ya kushangaza nape alisema bado hajapata matokeo ya huko.je ni kweli nape hajapata matokeo au alikuwa anakwepa swali?

source.gazeti la Mtanzania
Jinga sana kwaiyo unataka uletewe mezani kwako badala ya kufatilia au kazi yako ni nini?
 
Matokeo rasmi bado hayajatangazwa, hayo mnayoyasema ni matokeo ya kwenye vilabu vya gongo na viroba
 
SASA MLITAKA ASEME UONGO,!!?,NAPE HAJAPATA BADO MATOKEO,ana,mambo mengi ya kufanta,akiyapata atatueleza kinachoendelea NA MIKAKATI YA CCM KURUDISHA HESHIMA YAKE,UONGO HAUFAI,NAPE NI MTU MAKINI .
 
Nape sijui anafanya kazi gani amesababisha chadema wanapotosha jamii kwa matokeo yao ya vilabu vya gongo na viroba
 
Nape yuko sahihi coz bado hawajachakachua ili wapate matokeo yao Ikiwemo kuwaapisha wenyeviti wanawataka wao
 
Back
Top Bottom