Eng. Y. Bihagaze
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,487
- 913
. . ?
!!!Kutokana na wimbi la wananchi kuchukizwa na mfumo wa CCM na serikali yake na kiasi cha wanachama wengi kukihama chama hiki kikongwe, vile vile kutokana na ukweli kwamba chama hiki kikongwe kimepoteza mwelekeo kwa kasi na kustawisha majungu, udini, fitina na umaskini miongoni mwa jamii ya watanzania, Ububu au ukiziwi wa viongozi wake kwenye kero wazi zinazowasumbua wananchi kama migomo ya madaktari na chochezi za ubaguzi, baadhi wa wanachama wa CCM wameguswa na matukio ya upepo yanayokiandama chama chao hiki.
Fukuto la minong'ono kwamba kuna watumishi wengi wa serikali wakiwemo wanajeshi wana vyeti feki, limesokota hisia kwa kundi la wanachama wa CCM nao kuingiwa na mawazo kwamba isitoshe ndani ya CCM kuna vidudu-mtu ambao si wana CCM, lakini wako ndani ya Chama ili Kukidhoofisha na kukiua isitoshe baadae waunde vyama vyao kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Vyama kongwe barani humu.
Vuguvugu la kishawishi hiki kiliwasukuma wanachama hawa kwa siri kuunda kikosi kazi ili kuchunguza uhalali wa uanachama kwa baaadhi ya Viongozi wa chama chao ambao waliwalenga kama wavunjaji wakuu wa Chama. Baada ya wiki chache za uchunguzi wao wameorodhesha na kugundua kwamba baadhi ya viongozi wao kimsingi si wanachama wa Chama hiki. Wana-ccm hawa wakachomoa karatasi moja ya mtuhumiwa ambayo waliipenyeza kwenye meza yangu na mimi bila kumung'unya maneno LAZIMA niweke wazi suala lao kwa manufaa ya Umma. Kwa ridhio langu mwenyewe, na kama nazusha basi ntakua nimekiuka JF rules na nastahili kupigwa BAN!!, lakini nachokitoa ni uchunguzi uliojitosheleza ..
Nasema Nape, Moses Nnauye, si MWANACHAMA HALALI wa CCM, nikiwasilisha hoja ! Viongozi wote wa CCM mjue, kamati Kuu Ijue, Sekretariat ya Chama nayo ijue HILI..
1. Nape hana KADI ya CCM. Ingawa katiba haitaji moja kwa moja kwamba mwanachama wake itampatia kadi maalum yenye namba, ni utaratibu uliozoeleka wa kila mwanachama kuwa na kadi ya Chama Chake, Nape hana kadi Yoyote labda ya CCJ, mfukoni kwake kwa sasa. Kama atakuwa nayo basi aikate LEO baada ya kuona bandiko hili..labda. Kadi inuzwa kwa Tsh 500. Nape hana. Hana na anajua kwamba anatakiwa kuwa nayo muda wote. Na kama anayo naahidi kupigwa BAN!! Hapa JF na najiunga na CCM LEO, aniambie tu namba na tawi alilokata kadi hiyo.. HANA HANA HANA.. NASISITIZA SI MWANA CCM.
2. katika sehemu ya pili, fungu la kwanza Ibara ya Tisa ya katiba ya CCM, inasema mwanachama anayeomba uanachama wa CCM, atajaza fomu maalum ya uanachama na kuipeleka kwa katibu wa tawi analoishi. Nape hana tawi, hakuna kumbukumbu Popote kwamba mweshimiwa Huyu aliwahi kujaza Form za mwanachama, wala tawi husika. Anaeleaelea tu . kama analo ataje tawi husika tuone form husika na lazima tuwajibike kama tumemnangia makosa.
2. Katiba ya CCM, kwenye Ibara ya 10, Fungu hilo hilo inasema kamati ya Siasa ya halmashauri kuu ya CCM itakaa na kutoa maamuzi ya mwisho juu ya maombi ya mwanachama husika . hakuna Miniti zozote na Popote ambapo Halmashauri kuu ya CCM ilikaa na kumpitisha Nape na wengineo kwenye orodha ya Kikosi kazi hicho kwamba ni wanachama wa CCM. Kama kipo aseme tuwajibike..
3. Na Ibara ya 11 ya Fungu hilo inaainisha kwamba
Mtu akiwa mwanachama itabidi atekeleze yafuatayo.
a). Atatoa kiingilio cha uanachama ( Nape hajawahi kulipa kliingilio popote hapa Duniani cha uanachama wa CCM, kama amelipia hata kama ni kuzimu atuonyeshe risiti husika)
b). Atalipa ada ya Kila mwezi au akipenda atalipa kwa mwaka mzima (nape hajawahi kulipa ada hii jamani. Uhai wa Chama unategemea ada kutoka kwa wanachama wake, mwanachama Huyu hajawahi kulipa ada Yoyote, ni usanii sanii tu, kama anayo atuonyeshe risiti zote, au aseme amelipia kwenye tawi gani kikosi kazi kitafuatilia leo leo yeye ni kiongozi, hakuna usiri kwenye mambo haya, ni ya wazi kabisa, sijamtaka atuonyeshe account yake ina kiasi gani?, ni uhalali wa uanachama wake tu, na hili ni jambo la wazi kabisa)
Pamoja na mapungufu mengine mengi yaliyojitokeza, kikosi kazi hicho kimebaini kwamba baadhi ya viongozi wake wakuu si wanachama wa Chama hicho. Imagine Mtu mpaka anapewa kuwa Katibu Mwenezi wa Chama, hana sifa za Uanachama, unategemea atakuwa kwa maslahi ya Chama kweli au pana agenda ya siri hapo, alihoji mjumbe mmoja.
Ni Vema wanachama wa CCM wakawa macho na baadhi ya Viongozi wao, kauli aliyoitoa mweshimiwa huyu juzi kwamba CCM haifi hata akibaki peke yake, anamaanisha kila mtu sasa aondoke CCM ili abaki peke yake. Wazee wa mji waliokuwa kwenye kikao, wakimwelezea kwanini vijana walisusia mkutano wake , na kero ambazo zinakiandama chama, mweshimiwa huyu hakujali kujibu hoja husika badala yake alizidi kutoa matamshi tata ya kubariki watu kuondoka CCM abaki peke yake, akishabaki peke yake then, akibadili jina au..
Hutakiwi kujibu hoja Ngumu kwa majibu laini, jipange, kanunue kadi, uwe na tawi, Lipa ada Zote, jenga chama chako, Kiongozi lazima uwe mfano, ukiona inakukera achana na Uongozi nenda kaendeleze NGO aliyoiacha Mzee.