TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,673
- 1,571
Hali kwa redio stations nyingi ni mbaya watangazaji walio wengi hawana maadili kabisa ya kiuandishi.
Wakati mwingine wanazungumza maneno ambayo siyo utamaduni wetu kuzungumzwa hadharani hasa nyakati za mchana.
Mfano leo 05/04/2016 saa tano mchana kuna redio station moja (siwezi taja jina) watangazaji wanajadili juu ya usafi kwa mwanamke. Wanaeleza bila hata ya tafsida ya lugha maeneo ambayo mwanamke anatakiwa kujisafisha, pia walizungumzia masuala ya mapenzi na mahusiano kwa kushahabiana na usafi wa mwili. Mada haikuwa mbaya, ila muda ambao kipindi hiki kilikuwa kikirushwa ndiyo tatizo hasa.
Wito serikali kupitia kwa wizara husika tuondoleeni makanjanja wa habari katika vituo vya redio karibu vyote hapa nchini. Siku hizi mwanamke akijua kuropoka tu tayari anapewa kipindi katika redio station au mshereheshaji mzuri wa kitchen party naye anakuwa mtangazaji wa kipindi fulani katika redio station.