Nape sasa amtaka Mbowe ajiuzulu

Nape sasa amtaka Mbowe ajiuzulu

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Shinyanga.Katibu wa Itikadi na Uendezi wa Chama Cha mapinduzi (CCM),Nape Nnauye amemtaka Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe kujiuzulu nafasi hiyo mara moja kwa sababu ameshindwa kuiongoza kambi hiyo.

Wito huo uliutoa mjini hapa Ijumaa jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana katika mkoa huo.

Nape alisema vurugu zilizotokea hivi karibuni Bungeni ni uthibitisho wa wazi kuwa,Mbowe ameshindwa kuiongoza kambi hiyo kwa kuwa kabla yake hakukuwahi kuonekana fujo na vurugu kama hizo katika chombo hicho kinachoheshimika.

Alisema udhaifu wa Mbowe katika kuiongoza kambi hiyo ndiyo unaosababisha ishindwe kufanya kile ambacho Watanzania wanakitarajia kutoka kwa wapinzani.

Alisema wanasiasa ambao wanasababisha na kushabikia fujo na vurugu hawafai kwa madai kuwa wanaipeleka nchi mahali pabaya.

Hata hivyo, alisema hilo halitafanikiwa kwa sababu Serikali, CCM na Watanzania wapo makini dhidi ya mtu yeyote anayepanga kuwachonganisha. Aliishangaa Chadema kwa kushinikiza wabunge waongezwe kwenye Bunge la Katiba huku ikitaka wengi wa hao watokane na wanasiasa.

“Chadema inataka wawakilishi wa wakulima wawe kumi tu wakati wakulima ni asilimia 80 ya Watanzania wote. Hivi kweli wana lengo la kuwatetea Watanzania au maslahi binafsi tu,?”alihoji Nape.N

nape waliwataka wananchi kufanya uamuzi wa busara wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mku
 
Very simple argument.

It leaves a lot to be desired on the credibility of most of the CCM leaders
 
Mbowe ajiuzulu kwa fujo za Bungeni.
Kikwete aachwe asijiuzulu kwa fujo za UVCCM na UWT
 
inabidi walioleta muswada mbovu wajiuzulu kwanza kabla ya kiongozi wa KUB......
 
Kama ideology ni vurugu tu,kwanini asianze kuonesha uwajibikaji Rais kikwete? Vurugu zinazotokea kwenye taas zilizo chini yake ni kipimo cha kushindwa kiuongozi
 
Mbowe ajiuzulu kwa fujo za Bungeni.
Kikwete aachwe asijiuzulu kwa fujo za UVCCM na UWT
Nafikiri Nape amepata jibu zuri. Aanze kwanza Kikwete kujiuzuru, kisha afuate spika na naibu wake kisha wengine watafuata.
 
Mwambie ajiuzuru kwanza yeye ukatibu uenezi wa CCM. Nilimsikia pia akisema kuna wabunge wengine wanapoingia bungeni wanakuwa wameshakunywa viroba, nadhani angebanwa awataje hadharani hawa wanaokunywa viroba kabla ya kuingia bungeni.
 
ukiona chama tawala kinazunguka nchi nzima kuwatukana wapinzani basi ujue kweli ccm imedhibitiwa na imekosa namna ya kujitetea.
Nape Nnauye kumuambia mh.Mbowe ajiuzulu inadhihirisha kuwa CCM wamekubali CHADEMA chini ya Kamanda Mbowe ni moto wa kuotea mbali.
 
Last edited by a moderator:
Naunga mkono hoja. Mh. Mbowe ajiuzulu haraka sana.

vp nape na vita dhidi ya mafisadi kafanikiwa asilimia ngapi? hata pale alipowaahidi wananchi na kutoa siku tisini mafisadi kujivua gamba ninani hasa aliyemsikiliza? wote waliziona hzo ni mbio za sakafuni na viongozi wengne wote walijiweka kando..kama kweli alikuwa na nia ya dhati na kwa jinsi alivyo achwa apgane mwenyewe..nadhani angejiuzulu mapema 2. watanzania wengi wapo makini na mchakato huu wa katiba...kuanzia jinsi mlivyobemenda mabaraza ya katiba na sasa ktk bunge la katiba...hebu jiulize tunataka kutengeneza katiba ya ccm au ya taifa la tzania? wananchi wanajua nani mtetezi wa kweli...hata hvyo wananchi hawaridhiki na ubemendaji wa katiba..na iwapo rais hatasain mswada ule naamini utakuwa ujumbe tosha kwa nape, kwako na kwa wote wenye mtazamo wa chama kwanza taifa baadae. tafakari...tzania kwanza vyama baadae.
 
Nafikiri Nape amepata jibu zuri. Aanze kwanza Kikwete kujiuzuru, kisha afuate spika na naibu wake kisha wengine watafuata.

Mkuu Tanganyika TANU huwa nasema siku zote kuwa Nape Nnauye ni mlevi. Akina Sofia Simba wameporomosheana matusi ya nguoni na kina Anne Kilango utadhani sio akina mama tena wasomi. Wametamkiana hata mambo wanayoyafanya na hao vigogo wanaowawezesha ku-achieve political goals zao. Mambo ya sirini pamoja na tupu za binadamu zimetamkwa na kina mama hawa kisa UWT Shyrose bhanji na Sofia Simba waliporomosheana matusi hadharani. Huo umoja wao wa mizoga wanaouita UVCCM watu wametoana ngeu, wametukanana na wametaka kutoana roho. Hata sasa hawaaminiani. Nape Nnauye hakuona haja ya kumwambia Mwenyekiti wake ajiuzulu?
 
Last edited by a moderator:
Bila kutumia mabavu mbowe hana hoja nyingine ya kutumia kwenye uongozi wake.
 
Lakini siku anaondoka mbowe madarakani labda cdm ife kwamba kile chama ni chake hakuna mtu wa kumwambia kitu ndani na nje ya chadema ,jamani cdm ni ya mbowe.
 
Huyu nape amekosa cha kuongea sasa kati ya mbowe ambae anatetea wanyonge watanzania na kikwete ambaye ameshidwa kudhibiti matukio ya tindikali na milipuko ya mabomu ni nani anatakiwa ajihuzulu? Huko ni kukurupuka kama nguruwe pori mmeeneza mambo ya udini mnasafirisha madawa ya kulevya kila uchao hamjiuzulu
kweli nyani haoni kundule
 
vp nape na vita dhidi ya mafisadi kafanikiwa asilimia ngapi? hata pale alipowaahidi wananchi na kutoa siku tisini mafisadi kujivua gamba ninani hasa aliyemsikiliza? wote waliziona hzo ni mbio za sakafuni na viongozi wengne wote walijiweka kando..kama kweli alikuwa na nia ya dhati na kwa jinsi alivyo achwa apgane mwenyewe..nadhani angejiuzulu mapema 2. watanzania wengi wapo makini na mchakato huu wa katiba...kuanzia jinsi mlivyobemenda mabaraza ya katiba na sasa ktk bunge la katiba...hebu jiulize tunataka kutengeneza katiba ya ccm au ya taifa la tzania? wananchi wanajua nani mtetezi wa kweli...hata hvyo wananchi hawaridhiki na ubemendaji wa katiba..na iwapo rais hatasain mswada ule naamini utakuwa ujumbe tosha kwa nape, kwako na kwa wote wenye mtazamo wa chama kwanza taifa baadae. tafakari...tzania kwanza vyama baadae.
Zingine unaleta porojo sasa mkuu hakuna hoja ndani yake nikuhangaika tu.
 
Nape is a jackass let him continue with his idiot. Why should him threat Ndugai to resign and let freedom to reign in the legislative organ of tanzania? This is nonsense arguement from narrow minded man.
 
Hapa umekurupuka. Hii tabia ya kuandika utadhani unawahi maliwatoni misukule ya Lumumba mtaacha lini?
Tumia kichwa kujibu au kuchangia usitumie kile kiungo kingine unatia aibu kwani mbowe alishawahi kuwa na hoja lini zaidi ya kelele na matusi.
 
Naunga mkono hoja. Mh. Mbowe ajiuzulu haraka sana.

Huyu nape amekosa cha kuongea sasa kati ya mbowe ambae anatetea wanyonge watanzania na kikwete ambaye ameshidwa kudhibiti matukio ya tindikali na milipuko ya mabomu ni nani anatakiwa ajihuzulu? Huko ni kukurupuka kama nguruwe pori mmeeneza mambo ya udini mnasafirisha madawa ya kulevya kila uchao hamjiuzulu
kweli nyani haoni kundule
 
Zingine unaleta porojo sasa mkuu hakuna hoja ndani yake nikuhangaika tu.

Pole sana mtumwa wa magamba kwa kutetea vitu visivyofaa kutetewa.hizo buku 7 hazikusaidii kitu..kazi povu linakutoka na kuita kila mtu mkuu..ama kweli kichaa sio mpaka uvue nguo ,wewe utakuwa na ugonjwa wa akili.
 
Back
Top Bottom