Nape Nnauye ni tegemeo la CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye ni tegemeo la CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Deus F Mallya, Aug 25, 2012.

 1. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana Siasa za Tanzania tangu mwaka 2004 hadi sasa. Kwa kawaida kwenye vyama vya Siasa kuna watu 'Potential' ambao huwa kwenye 'Big five'. Leo nimelazimika kuuliza kama Nape Moses Nnauye anategemewa na CCM kwa kiasi gani? Yupo kwenye 'Big five' au hata 'Top ten'??.. Kwa wanaowafahamu na kufuatilia kwa karibu siasa za CCM (Political Obsevers) naomba tushirikiane hapa.

  NAPE NNAUYE ni Mwanasiasa Kijana ambaye awali alijipambanua kuwa anaweza kukinyoosha chama na kurejesha Imani za Watanzania. Huyu kwa sasa ni Katibu wa Itikadi na Wenezi CCM. Tangu alipopata nafasi hiyo amekuwa akifanya kinyume na pengine akimeza maneno yake mara kadhaa. Tujikumbushe: Utekelezaji wa Azimio la Kujivua gamba,hoja ambayo alizunguka nayo sehemu kadhaa akiwaambia wananchi kuwa mafisadi watafukuzwa ndani ya siku 90. Baadaye akameza maneno yake mbele ya waandishi wa habari. Nape amekuwa akiitolea serikali majibu ya hoja mbalimbali (Hoja ambazo zilitakiwa kujibiwa ama na BoT,Wizara na Ikulu).

  Nape ni kama amezidiwa na nguvu ya watu anaowaongoza ndani ya chama. Nape amekuwa akisubiri Viongozi wakuu wa CHADEMA waituhumu Serikali ya CCM ndo ajibu tena kwa ujasiri wa ajabu. Pengine ndiyo kazi ya Itikadi na uenezi CCM??.. Huku akiwekeza nguvu zote na za bosi wake kuiangalia CHADEMA kwa jicho la kengeza,CCM imekuwa ikiendelea kushindwa kwenye Chaguzi ndogo na pale inapowezekana wanacheza rafu kama Igunga... Pia Wanachama zaidi ya 800,000 wamejiunga na CHADEMA kwa kipindi kifupi sana.. Pamoja na kuwa nilijua CCM itakufa kabla ya mwaka 2015 lakini sikutegemea ife kifo cha gafla kiasi hiki.

  Nawasilisha!
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Nape ni kumuuwa kama yule Ras alivyouliwa ili mpumue.
   
 3. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Ndiye tegemeo lao mkuu kwa sasa ambaye anahangaika kujibu hoja zinazoibuliwa kila mara toka kwa wapinzani wao.
   
 4. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee babaangu nepi hana chochote anangoja akosolewe ndio ajibu mapigo,,

  ngoja niamke na kata ya mbege
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Acheni utani wandugu, CCM ndiyo tegemeo la Nape!
  Nape kuwa tegemeo la CCM itakuwa kichekesho!

  We Deus F Mallya ndiyo yule aliyepoteza roho ya Chacha?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. M

  Makupa JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa Nape ndio kijana pekee kwa sasa wa ccm anaetuwakilisha vizuri sana kwenye duru za kisiasa, ila akipunguza uharaka wa kujibu hoja dhaifu zinazotolewa na cdm hakika atajijengea jina kubwa.Kwa mfano swala la kutaka silaa achunguzwe wakati katibu wetu mzee mukama alishawahi kusema alichosema slaa.
   
 7. m

  mnduoeye Senior Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya Nape kupambana na EL kuhusu mradi wa ujenzi UVCCM na baadae kupigwa chini UVCCM na baadae kupewa ukuu wa wilaya kundi ndani ya ccm waliamini kuwa Nape ni jasiri kupambana na kundi la EL lakini matokeo yake yamekuwa tofauti kwani si Nape au kundi lililomweka uenuzi lilikuwa linajua upande wa pili una nguvu kiasi gani. ndio maana amebaki kujibu mapigo ya CDM na kuijibia serikali kazi ambayo sio yake.Hana nguvu tena kwani upande wa pili umemzidi maarifa na hata katibu wake mkuu amemwacha njiani akiwa kimya akimwacha aendelee kuyakoroga.Na vijana waloomtegemea Nape aokoe jahazi wamekata tamaa.Tuseme tu kwa kifupi kamati tendaji ya ccm hawako tena pamoja.
   
 8. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mantiki ya nafasi yake hasa ni ipi? Manake naona kama anakurupushwa sana na CHADEMA!. Mara kadhaa ukifuatilia kauli na hoja zake ni za kukurupuka!. Hapati muda wa kujipanga/Kufikiria. Hakai kwenye nafasi ya msikilizaji na kujisikiliza kabla hajasema. Kama kweli ni Tegemeo kwa CCM basi yeye atakuwa ugonjwa mkubwa sana wa kuiua CCM kwa haraka kiasi hiki.
   
 9. m

  mnduoeye Senior Member

  #9
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafasi ya uenezi ni kukijenga chama na kuhamasishi ujio wa wanachama wapya kwa maana ya kufanya mikutano ya uhamasishaji lakini afanyacho sasa ni kukurupuka bila kutafakari na kujibia sirikali
   
 10. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #10
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu kuna kundi linalojiita CCM Reform ambalo lina vijana wachache waliokuwa waamini wa Nape siku za nyuma. Nape si tu amepoteza nguvu ya Chama bali amepoteza marafiki wa karibu na kubaki na wanafiki wa karibu. Pia amechangia kuondoka kwa wanachama wanaohama kila kukicha kila sehemu ya kona ya nchi. Kifo hiki cha CCM ni kibaya kuwahi kutokea kwenye chama cha siasa kwa mujibu wa duru za kisiasa barani Afrika.
   
 11. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #11
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naam!. Nape anaendesha CCM kama chama cha Upinzani (Tena kichanga kabisa kama NLD au UMD). Kama alisoma Political Science atakuwa hakufanya vizuri darasani kwa kweli. Nafasi aliyo nayo ndiyo moyo wa Chama lakini yeye anaridhika tu wanachama wanavyohama kila kukicha huku akiwasindikiza kwa ngoma na matambo ya kejeli.
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ze Komedi
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yaani Watu Wazima na akili yenu Mnapoteza Muda wenu Kumjadili Nape? Nape My Foot
   
 14. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hayo ndiyo majibu yenu. Very good! Mnachekelea wakati damu zinawatoka puani mnajitia upofu. Shauri yenu!.
   
 15. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #15
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu hujasikia kuwa "Hata Dhaifu hujadiliwa"?

  By,Malcom Max
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Hivi hatuwezi kujadili bila kutaja damu? Jina lako+Damu= Mwili unasisimka.
   
 17. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Mwacheni nape jamani sasa hivi anajipanga kwenda kufukia mashimo ya m4c moro
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Nape kweli ndio tegemeo la Ccm akitoka Nape ni lusinde na Burn.

  Nape amekuwa mtu wa kuongea tu, najua kuna wana ccm wanakerwa natabia ya Nape lakini wanashindwa lakufanya!

  Nape huyu huyu anae waogopa watuhumiwa wa ufisadi hasa Jemedali E. Lowasa ndio apambane na ufisadi?
   
 19. M

  Makupa JF-Expert Member

  #19
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa Nape ndio kijana pekee kwa sasa wa ccm anaetuwakilisha vizuri sana kwenye duru za kisiasa, ila akipunguza uharaka wa kujibu hoja dhaifu zinazotolewa na cdm hakika atajijengea jina kubwa.Kwa mfano swala la kutaka silaa achunguzwe wakati katibu wetu mzee mukama alishawahi kusema alichosema slaa.
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ninavyoelewa mimi katibu wa halmashauri kuu ya Taifa wa itikadi na uenezi anafanya kazi zifuatazo
  1.anashughurikia masuala ya msingi ya itikadi na sera za CCM
  2.Ndiye msimamizi mkuu wa shughuri za uenezi wa itikadi,siasa na sera za CCM
   
Loading...