Nape Nnauye na Ugoro wa Babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye na Ugoro wa Babu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Apr 14, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni mwa miaka ya tisini, nikiwa kijana mdogo kabisa kambini kwetu akaja mgeni. Mosses Nnawie. Kulikua na shuhuli fulani ya kijeshi.

  Mosses Nnawie alikuwa mhamasishaji wa chama ndani ya jeshi. Alikuja na kinanda chake na mtoto wake. Mtoto wake alikuwa mdogo lakini akacheza kinanda, akajitahidi kutufurahisha. It was not the best but kwa umri wake alituburudisha. Nape Mosses Nnawie leo hii anafanya kazi aliyoifanya baba yake ndani ya chama hicho hicho, lakini siyo jeshini.

  Wakati huo alimsindikiza baba yake kila mahali (akasahau kusoma). Leo ameteuliwa kuwasindikiza babu zake, Msekwa, Wassira, Chiligati, na Mukama. Wakati huo alibeba kinanda cha baba yake, leo hii itabidi abebe ugoro wa babu zake ndani ya chama. Wakati huo alicheza kinanda, leo hii anacheza rumba la nguvu ya umma na JF.

  Ni kutokana na uzoefu wake wa kuwa anabeba mikoba ya baba yake tangu akiwa mdogo, ndiyo maana akafuzu vigezo vya kuteuliwa kufanya kazi na hao babu wa ccm. Ilikuwa ni jukumu la kifahari wakati huo, lakini kwa kazi hii mpya ni fedheha.

  Vuta hisia, kama uliwahi kuishi nyumba moja na babu yako. Jiulize ni kwa namna nyingi kiasi gani asivyokubaliana na mawazo yako. Jiulize kuhusu babu kutokupenda kuonekana kwamba hajui. Jiulize kuhusu babu kutokubaliana na namna za kisasa za kufanya jambo. Babu anapenda kusikilizwa na kuheshimiwa.

  Kuna mfano tayari. Msekwa anasema watapambana na JF (siyo Chadema!). Sijui kama anajua hasa anasema nini, natumani Nape anaelewa babu yake karopoka tu. Lakini by default and protocal ni Nape ndiye anatakiwa ahamasishe mapambano dhidi ya JF!

  Jaribu kujiuliza ni vipi inawezekana kupambana na JF. Watafanyaje kupigana na kitu ambacho hakishikiki. Kitu ambacho siyo taasisi. Kitu ambacho kinaweze kuendeshwa kutokea mahali popote duniani, kinakuwa managed kutokea kwenye computer yoyote au simu. Ukifunga huku wanafungua kule. Ukimkamata huyu, wale wanaendeleza.

  Kwamba Msekwa anamwagiza Nape apambane na keyboard? Ipi? Wapi? Hao mababu wana uwezo na nguvu ya kupambana na ufisadi ndani ya ccm na pia kudhoofisha Chadema na JF?

  Well, Nape atafanikiwa tu kuwabebea hao wazee ugoro na siyo kupambana na nguvu ya umma wala JF.

  Should I say, for ccm, it is as good as a doomsday conspiracy?
   
 2. T

  Taso JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Gurudumu, kwani Nape hakusoma? Jamiiforums tusiwe jamvi la waongo na wakuda.

  ``Nape alizaliwa Novemba 7, 1977 na kusoma Shule ya Msingi Mwanga, Nduguti, Iramba, Singida aliko babu yake kwa upande wa mama. Anasema Nape kuhusu kijiji alikozaliwa: "Ni kijiji ambacho kwa muda wote hakikuwa na umeme na nakumbuka hapa ndipo nilipoanza kusikia uchungu juu ya shida za Watanzania. Hiyo ilikuwa mwaka 1987 hadi mwaka 1989.

  "Kisha nilihamia Shule ya Msingi Bukumbi ambako mama alikuwa akifundisha toka mwaka 1989-1993. Mwaka 1994-1995 nilisoma Shule ya Sekondari Ngudu, Kwimba, Mwanza kama mwanafunzi wa Kutwa na baadaye nikajiunga na Shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza kati ya mwaka 1995-1997.

  "Kati ya mwaka 1998-2000 nilisoma masomo ya kidato cha tano na sita ya uchumi, jiografia na hesabu na kisha mwaka 2001-2003 nilijiunga na Chuo cha Sayansi Jamii Kivukoni, Dar es Salaam, sasa kikiitwa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere Kivukoni nikapata stashahada ya sayansi ya jamii," anasema.

  "Kivukoni nilisoma siasa, uchumi, saikolojia na uhusiano wa kimataifa. Mwaka 2003-2004 nikajiunga na Chuo cha Diplomasia cha Dar es Salaam kwa stashahada ya pili ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa. Baada ya hapo nikaajiriwa kwa mara ya kwanza mwaka 2004 Makao Makuu ya CCM, Lumumba Ofisi Ndogo kama Katibu Msaidizi, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa chini ya Omar Mapuri, baadaye chini ya Dk Asha Rose Migiro na sasa chini ya Bernard Membe".

  Anasema alikuwa masomoni Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, kwa shahada ya kwanza ya saikolojia, habari na lugha (Kiingereza na Kifaransa) na matumizi ya kompyuta na ushauri nasaha kati ya mwaka 2005 na mapema mwaka huu.``

  www.raiamwema.co.tz/news.php?d=225
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkuu wangu ee, angesoma angefaulu. Kuna watu wengi wamepita kivukoni enzi hizo lakini pia hawakusahau kusoma! Kivukoni lilikuwa ni jando la ccm siyo accredited higher learning college. Anayefaulu form six alichaguliwa kwenda chuo kikuu. Watoto wa vigogo kama yeye waliofaulu wakati huo walipelekwa urusi, china, ujerumani kusoma

  Hivyo nakubaliana na wewe kwamba amekalia madawati muda mrefu
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Thanks first for the nice work of art..............maelezo ya hapa pia yanajitosheleza

  Nina rafiki ambae alisoma kivukoni sio kwa kuwa aliingia kama ambavyo wewe utaingia UDSM au CBE au IFM lakini kwa lengo maalum la kujimezea siasa na uchumi kama sehemu ya mkakati wa CCM kujenga watu watakaokuwa wamejaa damu ya chama tayari kwa majukumu ya kuwa wapiga propaganda (nasikia zamani walikuwa wanpelekwa sijui nchi gani nje huko, wa kale mnaweza kutusaidia)......na ndio maana amekabidhiwa jukumu la propaganda kwa kuwa alipita wakati wakitoa elimu ya propaganda

  All in all, ugoro wa babu ndilo jukumu lake kubwa, akiwa amepewa kipoozeo baada ya machungu marefu ya wakati wa kura za maoni
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Vyovyote iwavyo, tunamkaribisha huku JF aje kupambana na wana jamii
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbona hiyo kazi walifanya wakati wa Uchaguzi mkuu wakasalimu amri? Hakuna mtu anadanganyika hapa
   
 7. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nnape achana na mawazo ya watumiaji ugoro kwamba eti adui mkubwa wa ccm ni JF. Waambie hao mababu kwamba adui yao ni watanzania wote waliofukarishwa na sera mbovu. Njoo humu JF tupambane kwa hoja.
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huyo "gamba junior" ajiandae kujivua maana kuingia mlango wa kutokea pole sana!
   
 9. e

  emrema JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  EEEEHE Kumbe Nape kama TUMBO HIZA,Kivukoni , 2003-2004 Chuo cha Diplomasia ,nilikuwa nangoja kuona BA,BSc,MSc kumbe YALE YALE. Naanza kunyong'onyea. Nape kwa nini hukusoma na Baba alikuwa na nafasi? Form 6 ulipata Division ngapi? MH Anza evening classes upate hata kabachelor.
   
 10. B

  Blessing JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa Kabisa Mkuu unaongea kabisa ukweli. Huyo Nanuye pia atuonyeshe cheti ya darasa. Sio cheti ya mlango ya nyuma. Hawa na lolote wa Chochote. WAMVUA GAMBA ----- Gamba Gani ??? Wakati nyoka ni hiyo hiyo na atapaki kwa nyoka tuu. Kuvua magamba sio hoja. The poison is within not on the surface. Hata wafanyeje ---- CCM ina smell BIG TIME there is no way Watanzania watakuwabali.

  Watanzania wa mia 47 sio waleo --- Walie tuu
   
 11. B

  Blessing JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anambavu gani ??? Aje kujaribu tumolize elimu yake imefikia wapi mkuu.... Aje tuu tutamvua wuchi
   
 12. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ni ngumu kupambana na tecknolojia ya habari,adui wa ccm yupo ndani ya ccm na sio social network,wajipange upya but first wanatakiwa wamjue abui wao kwanza na sio jf,facebok na twitter kama alivyosema pius,wataangukia pua kama 2010
   
 13. l

  lyimoc Senior Member

  #13
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  adui namba moja wa ccm ni hali ya kukatatamaa ya maisha ya watanzania .nawala wasijidanye kwamba jf ni adui wa ccm.
   
 14. maritanga

  maritanga Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu namshauri huyo aje kulingana na elimu na kigezo cha uelewa bado utakuwa mdogo sana inaonyesha zairi muda aliokalia madawati ni mrefu hali tu asiropoke ,angalizo kwake aende kwanza kuapa shahada tofaut na hiyo ya damu ya ccm
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kama mwenyekiti wao wa Taifa alikuwa anamkimbia Dr Slaa kwenye midahalo, ndio zije kuwa hizi takataka zake? ni nani mwenye uwezo ndani ya ccm wa kujenga hoja na kuisimamia na kupanguo hoja? siongelei propaganda hapa, namaanisha facts. siku moja humu nilimuuliza swali mbunge wa ccm wa jimbo la nzega ndugu Kigwangallah ( maana binafsi siwezi kumuita binadamu mwenzangu mheshimiwa ) basi ameingia mitini mpaka leo hajarudi humu na hakunijibu swali langu.
   
 16. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hoja ya kupambana na JF ingekuja kutoka kwa mtu mwingine ningeweza kuitafakari, lkn kama inatoka kwa Pius Msekwa? Sijui hata kama anaelewa anachoongea. Naona wanataka hata kumzeesha tuu huyu mtoto Nape afanane nao japo kifikra (za kizee)
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Labda watafute wanachama wa kukodi mkuu, siyo hao walio nao. Angalia waliokuwa wanapambana humu wakati wa uchaguzi walivyozidiwa nguvu. Angalia Jeykey na kundi lake walivyoishiwa nguvu na hasa baada ya magamba kuvuliwa sijawasikia tena kwa nguvu kama ilivyokuwa awali.
   
 18. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo Nape anatakiwa alione mkuu, kwamba yuko kwenye timu ambayo wachezaji wenzake wanatumia kanuni za mchezo za zamani sana halafu wanajidanganya kwamba watashinda. Yeye ndiye atakaye badilika na kuwa na fikra ma matendo ya kizee
   
 19. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  They have a wrong understanding of the problem and therefore a wrong strategy to solve the problem
   
 20. A

  Anold JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Ni historia nzuri ila kitu ambacho kinanishangaza ni kuwa ni sababu zipi ambazo zilifanya ccm imnyime kugombea jimbo la ubungo na sasa wanamfanya almasi? Nyota ya Nape ilikuwa inawaka toka siku nyingi lakini inavyooelekea viongozi hawahawa wa ccm walihakikisha kuwa wanampotezea, sasa hivi ccm imegundua dili ni serengeti boys ndiyo inajifanya kumfagilia Nape. Hivi nape analijua hili kuwa ni baada ya ccm kushikwa pabaya na CHADEMA ndiyo wanakumbuka damu changa? sasa huu mchanganyiko wa makande na maharage yaliopitwa na muda wake vitalika kweli?
   
Loading...