Nape Nnauye na Hekima za mfalme Suleimani

Nape Nnauye na Hekima za mfalme Suleimani

Uko sahihi kaka
Nape ni fungu la kukosa..alisimama kidete kufungia bunge live..Nape amekuwa ni mpinzani kila anaponyimwa fursa, kwa wanaojua siasa nadhani mnakumbuka alivyotoswa uvccm na mzee makamba alivyoendesha upinzani mpaka wakamtimua. Uwaziri unamuuma sana, gari la bure, nyumba bure, kila k2 bure.. Nape apambana na hali yake..kwenye furaha anatufanyia nyodo..goli la mkono..leo katoswa bashite yupo juu yake anataka tuumie wote hapana. Wapo wanasiasa naweza ku sympathy nao km Lisu siyo Mnape Mnauye..
 
Hilo neno DOMO naomba ulibadilishe maana hajatumia vibaya mdomo wake. Ila alichokuwa anakifanya ni sahihi kuunda tume ile ambayo haijampendeza aliyemuweka pale.
Nape na ile tume yake ilikuwa ni batili..
 
Kiburi chake huyo jamaa ndio kilifanya akomalie sheria za habari,BUNGE LIVE,kutukana wale wasiokua na mtazamo kama yeye kwakujiona alikua karibu na wafalme

Ujumbe huo amejilenga mwenyewe maana Mungu amemchapa fimbo
 
Kwenu,

"Kiburi cha mtu kitamshusha bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa"
Haya ni maneno ya Nape Nnauye, akinukuu Biblia toka kitabu cha Mithali sura 29:23,bila shaka yalielekezwa kwa fulani!
Alikuwa anajilenga mwenyewe baada ya kufuta "bunge live".
 
Nape anajifariji tu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nape ni fungu la kukosa..alisimama kidete kufungia bunge live..Nape amekuwa ni mpinzani kila anaponyimwa fursa, kwa wanaojua siasa nadhani mnakumbuka alivyotoswa uvccm na mzee makamba alivyoendesha upinzani mpaka wakamtimua. Uwaziri unamuuma sana, gari la bure, nyumba bure, kila k2 bure.. Nape apambana na hali yake..kwenye furaha anatufanyia nyodo..goli la mkono..leo katoswa bashite yupo juu yake anataka tuumie wote hapana. Wapo wanasiasa naweza ku sympathy nao km Lisu siyo Mnape Mnauye..
Vijana wanapopata nafasi za uongozi wapiganie haki na siyo ghilba za kipumbavu.
Mfumo walioutengeneza kina lowassa na sumaye for 20 years+ ndiyo uliotumika kuwatandika 2015 kwenye uchaguzi mpaka Leo ni majuto matupu.

Nape alitoa assist kwenye goli la mkono yanayotokea hata yeye anajiuliza kwanini hata hakufanyiwa faulo tu goli lisifungwe.

Kaingia bungeni kafungia Bunge ambalo sasa hivi lingempa fursa ya kusikika badala yake anafanya siasa twitter upumbavu tu.

Akapeleka sheria ya kuvifunga mdomo vyombo vya habari akitaka kumfurahisha baba yake wa kambo ( soma jiwe) madhara yake yanamrudia na yeye hakuna chombo cha habari kiko huru hata kumwita azungumzie utawala huu.

Vijana mnapopata nafasi piganieni haki.
 
Hayo mawaidha ya mfalme Suleiman yanamuhusu kila mwanadamu hata Nape pia. Zile kauli za Nape kuwa lazima tutashinda hata kwa bao la mkono au tutatawala kwa miaka 100 ijayo zilijengwa kwenye kiburi.
 
Huyu Jamaa Mnafiki Sana, Magufuli Anatakiwa Amkamue Haswa Hadi Unafiki Uishe
Sikubaliani na hili.
Nchi ama kiongozi yreyote yule hata kama ni RAIS ama nani HAHITAJIKI kuwa na moyo wa KISASI maana anaweza kuumiza wengi.
Huo ni USHAURI wa Hovyo sana kuwahi kuusikia.
 
the best comment...Ndiyo maana nasema Nape apambane na hali yake..
Mara nyingi nawambia vijana wenzangu wanapopata nafasi wapiganie haki watajenga Jamii iliyostaarabika kuliko kujikomba kwa wakubwa kutafuta mkate.

Kwa vyovyote vile vijana wana muda mrefu wa kuishi kuliko walioko juu yao kwahiyo mfumo wowote wanaoutengeneza Leo una madhara ya moja kwa moja kwao.
 
hyo c ndo alihimiza sana kuminywa kwa uhuru wa kuongea leo kawa na hekima tena duh
 
Alifanya kiburi wakati wa uchaguzi mkuu, akatukana na kukebehi alivyoweza.

Alifanya kiburi wakati wa kusitisha matangazo ya bunge live

Alifanya kiburi na jeuri wakati wa kupitisha muswada dhalimu wa sheria ya Huduma za habari mwaka 2016/

Hivyo kiburi na jeuri vimemshusha.

Nape ni mfano thabiti wa ule usemi Kuwa "malipo ni duniani"
Na big G ikiisha utamu hutupwa. Apambane na hali yake nje ya mfumo wa serikali
 
Vijana wanapopata nafasi za uongozi wapiganie haki na siyo ghilba za kipumbavu.
Mfumo walioutengeneza kina lowassa na sumaye for 20 years+ ndiyo uliotumika kuwatandika 2015 kwenye uchaguzi mpaka Leo ni majuto matupu.

Nape alitoa assist kwenye goli la mkono yanayotokea hata yeye anajiuliza kwanini hata hakufanyiwa faulo tu goli lisifungwe.

Kaingia bungeni kafungia Bunge ambalo sasa hivi lingempa fursa ya kusikika badala yake anafanya siasa twitter upumbavu tu.

Akapeleka sheria ya kuvifunga mdomo vyombo vya habari akitaka kumfurahisha baba yake wa kambo ( soma jiwe) madhara yake yanamrudia na yeye hakuna chombo cha habari kiko huru hata kumwita azungumzie utawala huu.

Vijana mnapopata nafasi piganieni haki.
Umenena vema mkuu
 
Ngoja nitafakari Tena ...

Anasema ....

''Kiburi Cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa''

Mh! Mbona ubongo wangu unanipa tafsiri ya mbali Sana ...

Eti ubongo wangu unaniambia eti kua amesema hivyo kumaanisha kua Eti ... huenda yeye ndie akawa raisi wa inji hii 2020 ...

Eti inawezekana kuwa kweli jamani mh!!!!

Mi mbona siuamini ubongo wangu ... LABDA!!!!!
 
Ila msisahau kuwa huyu mnafiki ali play part kubwa sana kufanya magu ashinde.
Na alizima bunge live
Na alihusika moja kwa moja kukanyaga katiba ya warioba.
Kwa hio inabidi apewe sonyo
 
Back
Top Bottom