Nape Nnauye: CCM imeshinda katika vijiji 2,708, Mitaa 644, na Vitongoji zaidi ya 26,300.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa.

Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.

Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.

Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009.

Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi.

"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema

Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.

"Nasema bila kificho, vijana wa CCM kama mtamuona mtu yeyote anajaribu kufanya fujo wakati wa upigaji kura mshughulikieni kidogo kabla ya kumpeleka polisi, maana watu wa aina hii wanabaka demokrasia, lazima waadabishwe". alisema Nape na kuongeza.

"Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge, unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi kufanya fujo, na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa natoa msisitizo tu".

Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.

Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.

Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.

Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu Tambaza.
=====================================================================================
baada%2Bya%2Bkuwasili.jpg

Nape Nnauye akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
mashabiki%2Bwa%2Bccm.jpg

mashabiki%2Bwa%2Bccm%2B2.jpg

shamrashamra.jpg

Wananchi wakimshangilia Nape Nnauye alipowasili kwenye kwenye mkutano huo
Azan%2BZungu.jpg

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Azani Zungu akisisita jambo jukwaani, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwataka watendaji wa serikali kuacha kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo katika biashara zao kwa kuwa ni eneo wanalofanyia biashara ni eneo la biashara badala yake watendaji hao watengeneze mazingira mazuri ya Mamalishe kufanya biashara zao badala ya timua timua ya mara kwa mara.
11.jpg

Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo
nape%2Bna%2Bmgombea.jpg

Nape Nnauye akimkaribisha jukwaani Gungu Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo
21.jpg

mkotya%2B4.jpg

Kada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape Nnauye baada ya hotuba.
Nape%2Bakimpongeza%2BHaji%2BManara.jpg

Nape Nnauye akimpongeza Haji Manara Mkotya baada ya kutoa hotuba fupi.
 
Nilidhani huyo Madabida yuko jela kwa ile kesi ya dawa feki za kupunguza makali ya ukimwi :confused2:
 
msitumie polisi katka siasa nendeni kwa wanach mtoe hoja by Mwenyekiti neno la kiongozi lichujwe
 
CCM wameshinda zaidi ya vijiji 2700 lkn mitaa 600 tu?Probability gani hii?

MwanaDiwani hamna probability kama hii duniani yaani ushinde kitu kikubwa zaidi(vijiji 2700) lkn kitu kidogo(mitaa iwe 600)tu!Acheni propaganda za zamani!

Kumbuka uchaguzi uliopita CCM walishinda zaidi ya 90% ya kura zote
 
MWANADIWANI,nakupa hongera tena kwa ushindi mlioupata baada ya mamia ya pingamizi.
Hongereni sana!!!!!
 
Imeshindaje wakati uchaguzi bado haujafanyika, nyie mnachezea demokrasia.
Ndugu,
Unaweza kuwa wewe ndiyo hufahamu demokrasia katika misingi ya utaratibu na sheria achilia mbali kinachotoa baada ya mchakato wa demokrasia!.
 
msitumie polisi katka siasa nendeni kwa wanach mtoe hoja by Mwenyekiti neno la kiongozi lichujwe
Ndugu,
Umeona polisi kwenye huo mkutano?

By the way, Kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zake ndani ya nchi.
 
Huyu Haji Manara ni tapeli wa magari mjini Dar-es-salaam,lakini leo chamapindu kinamuona ni hazina.
 
Nilidhani huyo Madabida yuko jela kwa ile kesi ya dawa feki za kupunguza makali ya ukimwi :confused2:

ndugu chama cha mapinduzi ni mawakili wa wezi na majambazi.wanalindwa kwa garama yoyote.ukiona mtu anaishabikia ccm umtilie shaka.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa.

Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.

Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.

Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009.

Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi.

"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema

Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.

"Nasema bila kificho, vijana wa CCM kama mtamuona mtu yeyote anajaribu kufanya fujo wakati wa upigaji kura mshughulikieni kidogo kabla ya kumpeleka polisi, maana watu wa aina hii wanabaka demokrasia, lazima waadabishwe". alisema Nape na kuongeza.

"Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge, unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi kufanya fujo, na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa natoa msisitizo tu".

Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.

Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.

Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.

Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu Tambaza.
=====================================================================================
baada%2Bya%2Bkuwasili.jpg

Nape Nnauye akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
mashabiki%2Bwa%2Bccm.jpg

mashabiki%2Bwa%2Bccm%2B2.jpg

shamrashamra.jpg

Wananchi wakimshangilia Nape Nnauye alipowasili kwenye kwenye mkutano huo
Azan%2BZungu.jpg

Mbunge wa Jimbo la Ilala, Azani Zungu akisisita jambo jukwaani, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwataka watendaji wa serikali kuacha kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo katika biashara zao kwa kuwa ni eneo wanalofanyia biashara ni eneo la biashara badala yake watendaji hao watengeneze mazingira mazuri ya Mamalishe kufanya biashara zao badala ya timua timua ya mara kwa mara.
11.jpg

Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo
nape%2Bna%2Bmgombea.jpg

Nape Nnauye akimkaribisha jukwaani Gungu Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo wa kufunga kampeni za serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo
21.jpg

mkotya%2B4.jpg

Kada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape Nnauye baada ya hotuba.
Nape%2Bakimpongeza%2BHaji%2BManara.jpg

Nape Nnauye akimpongeza Haji Manara Mkotya baada ya kutoa hotuba fupi.

Ninavyomchukia huyu ----, basi tu...angevunjika tu huo mkono na viungo vingine

Wana proud kushinda kwa pingamizi kumbe ni uoga tu washenzi wakubwa hao
 
mkuu ccm ni kichaka.ukitaka kupiga dili vizuri na kulindwa nenda ccm.

Hata huyo Madabida aliwauzia watu ARV's feki,lakini hadi leo yupo uraiani tena high table kwenye mikutano ya chamapindu,na ndiyo mwenyekiti wa chama mkoa wa Dar.Inauma Sana.
 
Only in Tanzania huyo mzee wa kutengeneza ARV feki anasimama kabisa mbele ya Wananchi kwa raha zake,aiseee ni shedaaaa
 
Back
Top Bottom