Nape Nnauye aapa kufia CCM

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,556
21,483
nape.jpg

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amesema kuwa hana mpango wa kuhamia chama chochote cha upinzani na ataendelea kubaki ndani ya CCM.

Alisema hawezi kufanya uamuzi wa kuhamia katika vyama vya upinzani , huku akidai magari ya upinzani kwa sasa yanazidi kuzama na haijulikani yataibuka lini.

Kauli hiyo aliitoa mjini Songea wakati akimnadi mgombea Ubunge wa Songea kupitia CCM, DK. Damas Ndumbaro katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Bombambili mjini hapa.

Nape ambaye pia aliwahi kuwa katibu Mwnezi wa CCM, alisema kama kuna watu walidhani atakihama chama tawala CCM na kujiunga na upinzani wasahau.

Alisema matatizo ya chama humalizwa ndani ya chama na si kukihama kama walivyofanya wanachama wengine waliokimbia ndani ya CCM.

“Naikubali serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari DK. John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa. Ni serikali yenye viongozi imara na mimi naapa kufia CCM na sivinginevyo.

“Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo,” alisema Nape.


Muungwana
 
Hana tofouti na luwasa hata akija atakuja kuvuruga then atakimbia mwishowe.yeyote yule aliyekulia ccm hawezi upinzani hata apewe uongozi hawezi....ndani ya ccm kuna fursa nyng sna ya ulajiulaji na usanii mwingi tofouti na upizani hakuna fursa unapambana na police.mwishowe hata sumaye atatimkia ccm.
 
Awaulize Lowassa, Sumaye na Kingunge kama kuna siku katika maisha yao walifikiri watakuja kuishi nje ya ccm!

Akijiuliza hivyo kisha aweke akiba ya maneno maana kwenye siasa hakuna linaloshindikana
 
Nape kahuzunika Lowassa kurejea Nyumbani Sijui alitaka aishi 'guest ' Maisha yote?
 
Hakuna mwana CCM WA kuondoka labda afukuzwe. Nyalandu mwenyewe sahz anafikiria decision aliyofanya kama ipo sawa.
Chadema wajipange upyaa .
 
Nape CCM hutaiweza!! kuhoji ukiukwaji wa katiba yenu ni sawa na kutumwa mabati ya simba-Dumu wewe ukanunua mengine....
 
Back
Top Bottom