makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,219
Mjomba unapoambiwa kuwa bila ukawa katiba haiandikiki huelewi? Ama kweli sisiemu wamewafanya watu wao kama misukule. Yaani hata masuala ya kawaida mnashindwa kubaini. Sasa shughuli gani itaendelea na wakati ushasikia bila ukawa katiba haipo. Huna hata aibu?
spiritual hero;
Uko sahihi mkuu. NEPI ni chizi kama chizi yeyote. Mimi nakwambia kuna mijitu ya CCM inaudhi na inakarihisha ile mbaya. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba iko wazi kabisa kwamba ili Sura au Kifungu kiweze kupitishwa kinahitaji kuungwa mkono kwa 2/3(Theuluthi 2) kwa pande zote za Muungano kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar!
Sasa kama UKAWA wako nje na hawa ndiyo wanahitaji ndani ya BMK ili kukamilisha AKIDI ya 2/3 kwa pande zote,hiyo Katiba utaipitisha vipi bila ya UKAWA.Hivi Nepi hawezi kujiuliza kwanini Mwenyekiti wa BMK Mhe. Sitta aliamua kuwafuata UKAWA kule Zanzibar ili kuwabembeleza warudi Bungeni???
Lakini pia hata Rais wao Kiwete ameona umuhimu wa UKAWA kuwepo kwenye BMK na ndiyo maana juzi kasema kuwa Katiba ikishindikana basi! Kiwete ameshaona ugumu wa kupatikana Katiba bila UKAWA. Sasa chizi mmoja hapa anasema UKAWA hata wasiporudi Bungeni Katiba itapatikana tu...????
Labda kama anazungumzia Katiba ya CCM!!!