Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #21
He might be a ccm but SIKILIZA hoja
Kwanza nakushukuru kaka Mchambuzi, hili ni jamboambalo ni la msingi sana, kuliongelea maana kwa sasa mimi naona ilivyo ni kama vile, pamoja na serikali kuongozwa na ilani ya chama tawala, lakini ukweli ni kuwa sehemu kubwa inaongozwa na priority za aliyeko madarakani, i mena raisi, ina maana regardless ni nani atakuwa raisi, ila akishika nchi vipaumbele vyake ndivyo vitakavyofanya kazi, that is why leo tumefika point nchi hii haieleweki ni ya kijamaa au ya kibepari ama ni mixed economy??!! (kama unajua unisaidie).
Nashukuru sana kwa mchango wako kwani unazidi kuhalalisha hoja yangu kwamba tuna tatizo kubwa la ki-tikadi, jambo ambalo linachangia sana umaskini wa walio wengi. Umeniuliza swali la msingi sana kwamba, Je Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa aina gani? Kijamaa? Kibepari? Mixed economy? Hili ni swali gumu, yet muhimu sana. Ugumu na umuhimu unatokana na ukweli kwamba, kwanza, ubepari katika jamii kubwa ya watanzania (vijijini), ni one way i.e. kuzalisha for exports to feed the global capitalist system; vilevile watanzania wengi (ambao ni vijijini) hawana uhusiano wa karibu sana na public sector, badala yake wana ukaribu karibu zaidi na NGO sector, na pia kwa mbali sana private sector. Pia vijijini suala la market ni kama no- existence kutokana na uwepo wa subsistence economu, hivyo market forces dont exist; na hata kungekuwepo na market, ingekuwa ni market failure.Ni kutokana an mvurugano huu ndio maana sitaweza kujibu swali lako, na badala yake kulijadili tu randomly (niwie radhi kwa hilo),kwani hakuna jibu rahisi. Hivyo naomba tusaidiane mawazo ili tupate jibu zuri.
Kwanza, Tanzania kama taifa, inafuata soko huria ambapo wananchi wanaathirika nalo either directly au indirectly, kutegemeana wanaishi wapi baina ya modern and subsistence sector. Na katika hili, tusisahau kwamba soko ni kitu kilichokuwepo kwa karne nyingi hata kabla ya kuzaliwa ubepari. Kilichobadilishwa na ujio wa ubepari duniani ni aina tu ya soko, ambalo kwa sasa, tofauti na zamani, linaitwa soko huria.
Pili, kwa vile Tanzania ni nchi inayotegemea mataifa makubwa kwa misaada, sera zetu ni mchanganyiko wa zile za kihafidhiana, kiliberali, na Ujamaa wa demokrasia, kutegemeana na vyanzo vya misaada hiyo. Kwa mfano, misaada kutoka nchi kama Sweden,Norway ina leftist agenda na inaenda kwenye huduma za kijamii zaidi, while misaada inayotoka Marekani, Japan, na hata WorldBank au IMF, kwa kawaida inaenda kwenye maeneo ambayo wana amini yataleta economic growth (hata kama such a growth is not pro poor). Vilevile, mchanganyiko wa sera hutokana na chama gani/itikadi ipi imekamata DOLA katika nchi kama UK, USA, na Ujerumani, ambao ni wahisani wakubwa sana wa Tanzania. Na mchanganyiko unazidi kushika kasi pale tunapobaini kwamba wakati CCM ni rafiki mkubwa wa vyama kama Labour (UK) na Democrats (US), Chadema ni rafiki mkubwa wa vyama kama Conservatives (UK) na Republicans (US, ingawa vyama hivi sio vya mrengo wa kati kama Chadema bali mrengo wa kulia. Vilevile CCM ni rafiki mkubwa wa Chama Cha Kikomunisti, China.
Kwa mtazamo wangu, njia nyingine ya kutusaidia ubaini mfumo gani Tanzania inaufuata ni kwa kuangalia vitu viwili:
Moja, Je wananchi walio wengi wanaishi katika mfumo upi? Maoni yangu ni kwamba, wapo katikati, na kote ni kubaya. Kwa upande mmoja, wanaumizwa na mfumo ule ule wa kikoloni wa kuwazalisha mazao ya mataifa matajiri (kahawa, chai, n.k), na pia kuwazalishia elites wa mjini (DSM etc) vyakula (mahindi, viazi, mchele), bila ya faida yoyote ya maana in return. Na kwa upande mwingine, hawafaidiki na mfumo wowote uliopo Tanzania (whether ni ubepari, mixed, n.k) kwa sababu ambazo nimezitaja kwa mfano, huduma za sekta binafsi na sekta ya umma kule vijijini ni kama hakuna, zaidi ya zile zinazotolewa na NGO sector, au zitokanazo na juhudi binafsi za wananchi wenyewe kama vile kujijengea nyumba, na madaraja ya ovyo ovyo, kuishi kwa kutegemea tiba za kienyeji, kujilisha chakula kwa kulima nyuma ya nyumba/uani, badala ya kutegemea exchange in the market, n.k.
Pili ni kuangalia, Je wananchi wengi wanaamini katika itikadi ipi. Kwa mtazamo wangu, wengi vijijini (ni muhimu tuangalie zaidi wa vijijini kwani ndio walio wengi Tanzania), watavutiwa zaidi na itikadi za mrengo wa kushoto kuliko wenzao wa mijini kutokana na ukweli kwamba kwa hali zao duni, wanahitaji msaada wa serikali/sekta ya umma katika kila hali. Hili linachangiwa pia na ukweli kwamba viijiji havivutii sekta binafsi kuwekeza/kuendesha shughuli kibiashara. Isitoshe dhana ya efficient allocation of resources chini ya soko huru inahimiza uwekezaji/mitaji kwenda kule tu panapozaa faida, na ni bayana kwamba vijijini suala la faida kwa mwekezaji halipo.
Kwa upande watanzania wanaoishi mijini, hawa kuna uwezekano wa kugawanyika kati ya wanao unga mrengo wa kushoto, mrengo wa kati na mrengo wa kulia. Lakini wengi wa wakazi wa mijini pia wana hali duni sana, Kwahiyo wao pia watavutiwa zaidi na itikadi na sera mrengo wa kushoto. Sakata la ongezeko la nauli za Kivuko cha kigamboni ni mfano mmoja wapo.
Niwie radhi kwa majibu yasiyokuwa na mpangilio wa maana, lakini natumai angalau inaweza kuweka msingi tuanzie wapi juu ya mjadala huu wa mfumo gani Tanzania inafuata n.k .