Chaimaharage
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 211
- 78
Mbona mara zote umekuwa mwepesi kushobokea mambo yasiyo yamsingi wala tija kwa chama chako? mfano unapo komalia suala la Shibuda suala ambalo lina shughulikiwa na chama husika. Hakuna kiongozi hata mmoja wa CDM amepoteza muda wake kumjadili Shibuda sababu wanajua "it's not a big deal" Hivi unadhania mzozo wa Shibuda utawapatia credits magamba? Hebu jaribuni kubuni mbinu mbadala za kukiokoa chama chenu. Yaani wewe dogo hujui mpaka sasa kuwa unakiua chama.
Safari hii mnalo..na imekula kwenu..Tatizo hamjui kuwa chama kinakufa. Watu wanataka maji, barabara, huduma bora za afya n.k. Muda huu siyo wa propaganda wala ahadi kama mlivyozoea. Uchaguzi wa 2015 wenye nafasi ya kutoa ahadi ni vyama vingine na siyo CCM. Ninyi tunataka mtatueleza kwa miaka 50 mmefanya nini ili mpimwe kwa hilo. Propaganda chafu na fitina hazito wasaidia. Bahati mbaya kwenu bado muna amini katika hayo kama silaha ya kisiasa. Kwa taarifa yenu CCM ina chukiwa kuliko mnavyo dhania. Vijijini ambako palikuwa ngome yenu ya kujizolea ushindi wa bwerere baada ya kuwahonga pesa, vyakula, pombe za kienyeji, t-shirt, khanga, kofia na ahadi kemkem zisizo tekelezeka hivi sasa wana mwamko wa ajabu kufanya mageuzi.
Sasa basi 2015 pelekeni mbinu zenu hizo muone kazi. Kimsingi kuna kila dalili za kushindwa. mfano maswahiba wenu katika kufanikisha mbinu chafu kwenye chaguzi wenyeviti wa vijiji na mabalozi kitendo cha kukataa kugombea uongozi ni pigo kubwa na kiashiria nini kitatokea siku zijazo. Nani atafanikisha mikakati yenu? mfano mwingine ni kwamba zaidi ya 70% ya population ya nchi hii ni vijana ambao wengi wamefikisha umri wa kupiga kura na hawa ndiyo wanaongoza kuichukia CCM na wanaihama. Je, mnatarajia nani atawapatia ushindi, wazee?
Ushauri wangu jiandaeni kuwa kambi rasmi ya upinzani, mkichelea nafasi hiyo itachukuliwa na CUF au NCCR. Msipoteze muda wenu kufikiria kudumu kwenye dola. Wenye maono tumekwisha liona hilo.