msimamo wako kwa Lowasa mkuu tunaujua haukuwahi kubadilika na haukuwahi kumkubali tangu siku ya kwanza, kwa hilo hata mimi nakutetea.
Sent using Jamii Forums mobile app
keep it up mkuu, msimamo wako haukukuangusha ila umewaacha watu midomo wazi na kuwaumbua zaidi.Shukrani sana Mkuuna uamuzi wa kuendelea kumpinga huyu hata baada ya kujiunga na chadema haukuwa mgumu hata kidogo. Nilijiuliza kuhusu ufisadi wa zaidi ya billions 500 walioufanya yeye, Rostam na Kikwete kwenye Richmond/Dowans ambao ungeweza kabisa kuepukwa. Nilijiuliza kuhusu ukimya wake kuhusu ufisadi mbali mbali Serikalini ikiwemo IPTL, EPA, nyumba za Serikali etc nikakosa majibu. Hivyo kukosa majibu kuhusu maswali hayo kulinirahisishia uamuzi wangu wa kuendelea kumpinga.
Huu si utetezi ni ujinga uliokithiri,mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu,achaneni na Lowassa ,jengeni saccos yenuMtu anaweza akapoteza mda na lengo katika kuchambua sababu zilizomfanya Lowassa arudi nyumbani.
Kuna mambo yanayoweza kutoa mwelekeo wa kuhama huko.
Kwanza kabisa inaonekana palikuwa na ushawishi mkubwa toka CCM mzee huyo ahame. Matakwa haya sababu zake zinaweza zikafikilrika.
Ni ajabu sana timu yote nzima ya uongozi wa juu wa CCM kuweka mapokezi kiasi kile kwa mtu ambaye walishajua wamemmaliza.
Hapa ndipo palipo siri nzito!
Mapokezi yale yanaonyesha dhahiri, kuhama kule hakukuanzia kwa Lowassa. Walimtaka sana ahame; sababu, hatujui!
Sasa ukifikiria, kati ya Lowassa na Nnauye, ni nani mwenye thamani kubwa ndani hicho chama?
Sina hakika sana kama Nnauye angehama na kurudi chamani angepata mapokezi kama aliyopewa Mzee Lowassa.
Kuna jambo wana hofu nalo linalomhusisha Lowassa kuelekea 2020?
Huyu Mzee sitaki hata kusikia jina lake walahi vile, nakumbuka nlivyotoroka kazini siku ile ya Kampeni akiwa Arusha, nkaponea chupuchupu kupumzishwa na barua ya warning na Kanjbhai wangu, nakumbuka tulivyopigwa na jua ile siku, nakumbuka usafiri wa kurudi nyumbani ulivyotutesa kama haitoshi siku ua kupiga kura tulivyoamka asubuhi asubhi nkapiga magoti kumuombea, walah napata hasira isiyo kifani
Hakuna wanao wapaga kura za kuwawezesha kuongoza nchi bali wanaiba na kuwatishia wananchi
In God we trust
Ndo maana nimetoa hoja yangu maana nina heshimu mawazo yangu na ni bora kama nilivyosema ila ijulikane tu hamna aliyekurupuka hapa najitambua na ninajua nachokifanya mawazo ya mtu YaheshimiweUwe unasoma na kufuatilia mijadala kwa kina badala ya kukurupuka na dhana zako POTOFU zisizokuwa na mashiko. Na Watanzania wanaojadili kuhusu siasa haina maana ni wanasiasa bali wanatumia haki yao kikatiba kujadili mustakabali wa nchi yao.