Nape: Lowassa ni Kunguru hafugiki

Nape: Lowassa ni Kunguru hafugiki

Wacha naye aonekane ameitetea ccm
Ungekuwa unajua nilichowahi kuandika humu kuhusu lowassa kuja Chadema mara nyingi tu humu usingeandika huu upumbavu wako.

In God we trust
 
Watasema nini baada ya Lowassa kurudi CCM?

Monday March 11 2019

LOWASAAA+P.jpg

Kwa ufupi
  • Edward Lowassa ambaye amekuwa akibadili mwelekeo wa kisiasa, ambapo Julai 28, 2015 alitoka CCM na kwenda Chadema kisha Machi mosi, 2019 akatangaza kurudi CCM, kumekuwapo na kauli mbalimbali za wanasiasa kumzungumzia, lakini swali linabaki kwa wakati huu watasema nini?

By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Miongoni mwa viongozi wa vyama ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakichafuliwa na kusafishwa na watu haohao ni pamoja na Edward Lowassa.
Wakati akiwa CCM kabla ya kutimkia Chadema Julai 28, 2015 alikuwa akinangwa kwa ufisadi, papo hapo alipohamia Chadema aliendelea kuitwa fisadi na watu wa CCM huku watu wa Chadema wakimsafisha, lakini hivi sasa amerudi CCM watasema nini?
POLEPOLE.jpg

Mnamo Septemba 29, 2015 Humphrey Polepole akiwa kwenye kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel 10 alisema Lowassa ni tajiri hana uhusiano na masikini na hahitaji kusafishwa kisheria kama ambavyo Chadema walikuwa wanadai kwamba kama ana hatia ya ufisadi inayosemwa apelekwe mahakamani.
Alitoa kauli hiyo mara baada ya kiongozi huyo kuhamia Chadema na chama hicho kutumia nguvu nyingi kumsafisha kutoka kwenye dimbwi la tuhuma za ufisadi alizokuwa akishutumiwa.
Kwa upande wa katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba alikuwa akieleza udhaifu wa Lowassa katika mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.

makongoro.jpg

Akiwa kwenye kampeni sehemu mbalimbali aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Makongoro Nyerere alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la ufisadi na rushwa.
Alisema kwa kuwa ufisadi bado ni tatizo, wataendelea kuwaeleza Watanzania katika kampeni zao kuwa mgombea huyo wa Chadema ni fisadi.

Lowassa amekuwa na nia ya kugombea urais kwa muda mrefu tangu mwaka 1995 wakati jina lake lilipokatwa, hakuchukua fomu mwaka 2005 wakati Jakaya Kikwete, aliyekuwa rafiki yake wa karibu, alipogombea.
Lowassa alisema walikubaliana na Kikwete kwamba waunganishe nguvu ili awamu inayofuata iwe zamu ya mbunge huyo wa Monduli.
Hata hivyo, mwaka 2015 jina la Lowassa lilikatwa na makada wengine 33 na ndipo akaamua kujiunga na Chadema kuendeleza ndoto yake ya kuingia Ikulu.
Septemba 29, 2015 aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye viwanja vya Samora, mjini Iringa alitumia dakika 10 kumshambulia Lowassa.
Alisema Lowassa ni mwizi na fisadi na kwamba hakuna sehemu ambayo alipewa kufanya kazi katika ngazi za CCM na Serikali bila kuiba.
NAPE.jpg

Nape alidai Lowassa alishindwa kukaa CCM kwa kuwa hawezi kufugika "Lowassa ni kunguru, hafugiki."
MUSUKUMA.jpg

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ambaye sasa ni mbunge wa Geita, Joseph Msukuma naye alimvaa Lowassa alipohamia Ukawa kwa kusema kuwa wanashukuru chama kimetua mzigo.

“Nataka nimwambie ndugu yangu, rafiki yangu Lowassa, huu ni muziki mkubwa,” alisema Msukuma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli uliofanyika mjini Chato, mkoani Geita Septemba 21, 2015.

“Tunaomba wachukue na wengine wenye tabia kama hizo. Wenye akili timamu tutabaki CCM...Mgombea wetu (Magufuli) anatosha. Na hapa ndiyo kwao, nimetembea na Lowassa gari moja, ndege moja, tunachagua rais na sio bora rais,” alisema.

“Katika Kanda ya Ziwa, hakuna aliye na siri za Lowassa kama mimi, naomba waniweke kwenye mdahalo nitagharimia, niwapige kavu kavu. Watu wanaokwenda kule (Ukawa) zinatangulizwa hela. Nani anachukia hela?.”
Mara baada ya Lowassa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli, Msukuma alibadilika na kumuasa kuwa, “Mi nakuomba Mzee Lowassa huku ndiyo kwenu hilo genge la wahuni hutoliweza, Lowassa kwenda kule ilikuwa ni hasira tu.”
MWAKYEMBE.jpg

Naye Dk Harrison Mwakyembe akiwa Waziri wa Afrika Mashariki, alitoa andiko la kujiapiza kupambana kufa na kupona kuhakikisha Lowassa haingii Ikulu.
Katika andishi lake alilolituma kwenye mitandao ya kijamii, Dk Mwakyembe anasema, Lowassa hana sifa ya kuwa Rais.
“Namuona Lowassa kama mtu ambaye anatapatapa huku akiujua ukweli kwamba hana nafasi hata kiduchu ndani ya CCM.”
Alisema anahaha kutumia mabilioni kuhonga na kusafirisha watu kwenye tendo la kutangaza nia tu, hivi unafikiri kamati zote za CCM zina njaa ya pesa zako za kifisadi?

Dk Mwakyembe ambaye sasa ni waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo alisema
atakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua Watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.
“Ninakusubiri kwa hamu ili nikusikie utakavyokuwa unabadili jahanam kuwa peponi, kwa manufaa ya Watanzania nitaanika hadharani uozo wako wote kwa ujasiri na bila hata chembe ya woga ili Watanzania wasipotoshwe tena kwa njia ya bwembwe za fedha,” alisema.
zitto.jpg

Kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe akiwa Singida kwenye mkutano wa kampeni Agosti 7, 2015 alisema ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa kutokana na kuwa na kashfa za ufisadi.
Hizi ni baadhi ya kauli za wanasiasa hawa kuhusu Lowassa, swali linabaki kwa sasa baada ya kurejea CCM watakuwa na kipi cha kusema juu ya mwanasiasa huyu?
Chadema mnateseka sana na Lowassa!
 
Mkuu BAK, kusema ukweli kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu, na wala sio kwamba najipendekeza kwako:
NI WEWE TU, PEKE YAKO HAPA JF AMBAYE HUKUWAHI KUMSHOBOKEA LOWASA
kama kuna kuna mtu anayebisha alete hapa comment yako hata moja tu ambayo itanikanusha. Tangu mwanzo hukuwa na mahaba na EDO.
Wewe sio kigeugeu kama wengine akina fulani......
 
Kwasababu ya upofu na upumbavu uliokujaa mpaka unyayoni umeshindwa kuelewa mantiki ya nilichoandika lofa wewe...
Nimekuambia uache unafiki balance mipasho yote uliyoitoa wewe na wanasiasa wenzio wa CCM na chadema dhidi ya lowasa kisha uiweke na sio kuusema upande mmoja...
Ikiwa unajisema ulizungumza mabaya ya lowasa kipindi hicho maana yake wewe pia ni miongoni mwa wasio CCM walimsema lowasa na yet lowasa akaja upande wenu mkaona swadakta kabisa ila leo amerudi CCM unajifanya wataka uwasemee CCM pekee kwamba ndio walimsema...Acha hizo wote ninyi mlimsema Kwa mabaya mliyoyaweka hadharani hivyo usiuhukumu upande aliorudi sasa kana kwamba wao hawastahili kumpokea isipokuwa ninyi...acha unafiki
Wanasema haki inadaiwa na walio na mikono safi lakini pia kabla hujatoa kibanzi Kwa jicho la mwenzio hebu ondoa boriti Kwa jicho lako...

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Mwenye kukuelewa ameelewa shida sana !mara nyingi kwemye majukwaa ya siasa huwa napita zangu tu bila kuchangia kwa maana huwa ni matus tui huwa nakereka sana nikisoma comment mbili au tatu lazima ukitane na matusi kejeri na uchafu watu wanatukana sana huwa kuchangia ni ngumu sana maana sipendi matusi kabisa

Afu kuna watu wanajikuta wanaabudu mtu hao wana siasa bila kujua mfano huyo Mwanasiasa (fulani namhifadhi kwa jina) hata akiongea mazuri ni sawa kusifia haya akiongea mambo yasiyo mazuri bado mtu anasifia tu kwa sababu ameshatekwa kisaikolojia bila kujitambua huyo Mwanasiasa akisemwa mapungufu yake bado hapa jf huyo aliyemsema kwa ukweli atatukwana sana wakati wanatakiwa wajibu hoja ama kweli kizazi kibaya sana hiki na wengine ni watu wazima kabisa wanatukana sasa nashindwa kukutofautisha na mtoto asiyejitambua
 
Ni kweli kabisa hajawahi kuwa na mahaba na lowasa ila sasa amekuwa mnafiki na mchonganishi kwa kutaka kuonyesha namna gani lowasa asiempenda alinangwa pia na wana ccm na hawakumtetea kama asemavyo kisha anasahau kuwataja wapendwa wake Wa chadema na ukawa kiujumla waliomshobokea na kumtakasa MTU waliemnanga kwa herufi kubwa sana....alipoenda kwao alikuwa mwema ila aliporudi alipotoka anatafutwa mchawi...
Mkuu BAK, kusema ukweli kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu, na wala sio kwamba najipendekeza kwako:
NI WEWE TU, PEKE YAKO HAPA JF AMBAYE HUKUWAHI KUMSHOBOKEA LOWASA
kama kuna kuna mtu anayebisha alete hapa comment yako hata moja tu ambayo itanikanusha. Tangu mwanzo hukuwa na mahaba na EDO.
Wewe sio kigeugeu kama wengine akina fulani......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo utabaki ukweli siku zote. Nilitafakari kwa kina ujio wa lowassa chadema na tuhuma zake mbali mbali za ufisadi akiwa ccm na pia Serikalini. Kulikuwa na maswali mengi kuhusu ufisadi wake ambayo alishindwa kuyajibu ikiwemo mamilioni ya pesa alizokuwa akigawa kwenye nyumba za ibada. Alipoulizwa mapesa yale anayapata toka kwa marafiki zake na alipotakiwa kuweka hadharani majina ya hao marafiki zake na kiasi ambacho kila rafiki alimpatia alishindwa kufanya hivyo. Nilimuona ni fisadi mkubwa kabla ya kuingia chadema na miaka yote karibu minne ndani ya chadema niliendelea kumuona ni fisadi mkubwa.

Mkuu BAK, kusema ukweli kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu, na wala sio kwamba najipendekeza kwako:
NI WEWE TU, PEKE YAKO HAPA JF AMBAYE HUKUWAHI KUMSHOBOKEA LOWASA
kama kuna kuna mtu anayebisha alete hapa comment yako hata moja tu ambayo itanikanusha. Tangu mwanzo hukuwa na mahaba na EDO.
Wewe sio kigeugeu kama wengine akina fulani......
 
Uwe unasoma na kufuatilia mijadala kwa kina badala ya kukurupuka na dhana zako POTOFU zisizokuwa na mashiko. Na Watanzania wanaojadili kuhusu siasa haina maana ni wanasiasa bali wanatumia haki yao kikatiba kujadili mustakabali wa nchi yao.

Asante Mwenye kukuelewa ameelewa shida sana !mara nyingi kwemye majukwaa ya siasa huwa napita zangu tu bila kuchangia kwa maana huwa ni matus tui huwa nakereka sana nikisoma comment mbili au tatu lazima ukitane na matusi kejeri na uchafu watu wanatukana sana huwa kuchangia ni ngumu sana maana sipendi matusi kabisa

Afu kuna watu wanajikuta wanaabudu mtu hao wana siasa bila kujua mfano huyo Mwanasiasa (fulani namhifadhi kwa jina) hata akiongea mazuri ni sawa kusifia haya akiongea mambo yasiyo mazuri bado mtu anasifia tu kwa sababu ameshatekwa kisaikolojia bila kujitambua huyo Mwanasiasa akisemwa mapungufu yake bado hapa jf huyo aliyemsema kwa ukweli atatukwana sana wakati wanatakiwa wajibu hoja ama kweli kizazi kibaya sana hiki na wengine ni watu wazima kabisa wanatukana sasa nashindwa kukutofautisha na mtoto asiyejitambua
 
Huyu Mzee sitaki hata kusikia jina lake walahi vile, nakumbuka nlivyotoroka kazini siku ile ya Kampeni akiwa Arusha, nkaponea chupuchupu kupumzishwa na barua ya warning na Kanjbhai wangu, nakumbuka tulivyopigwa na jua ile siku, nakumbuka usafiri wa kurudi nyumbani ulivyotutesa kama haitoshi siku ua kupiga kura tulivyoamka asubuhi asubhi nkapiga magoti kumuombea, walah napata hasira isiyo kifani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kumbuka kauli ya Kikwete kutaka kulivua gamba. Kulivua gamba ilikuwa ni kuwafukuza ccm mafisadi waliokuwa wanakichafua chama wakiwemo Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo. Nape hajawahi kutukanwa ndani ya ccm kama alivyotukanwa fisadi lowassa. Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.
Kwaiyo ccm walivua gamba cdm wakalivaa gamba?

Una credibility ya kuisemaa ccm ili hali hilo hilo gamba limeondoka juzi tu kwenu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ILA nyie wanasiasa ni wanafiki mliotukuka aisee! Hakuna wa CCM wala vyama visivyo na dola a.k.a wapinzani, nyote mmejaa unafiki uliopitiliza...
Lowasa akiwa CCM mlimuona tishio kwa style yake mkaisema ya ufisadi mkubwa mkapiga kelele kila Kona mkijinadi na ushahidi mnao mbinguni na duniani na CCM ikimuweka mtu mchafu kugombea urais ni sawa na kunajisi ikulu, CCM Kwa namna yake wakampiga chini asigombee Kwa chama Chao....wapinzani kwenu ikawa fursa mkamsafisha Kwa UBATIZO wa Moto hamkutaka kuhojiwa kana kwamba ninyi ndio mitume na manabii na makuhani wenye kutakasa dhambi, amegombea kwenu mmemsafisha Kwa gharama zote ikiwemo kuwapoteza wanachama wenu, sasa CCM wakaanza nao kuwarushia madongo juu ya unafiki wenu lakini mlipotezea kimyaaaa, Leo jamaa kawarudia tena CCM ambao walirithi propaganda zenu za kumdhalilisha lowasa nanyi mmeanza tena kumsema na bahati mbaya sana mnabadilisha magoli kana kwamba hii hoja ni ya CCM hapo awali kumbe miaka zaidi ya nane kabla hamjampokea kuwa mgombea wenu mlimsema vibaya Sana.
Sasa unapo nukuu kauli za Wana CCM waliomnanga lowasa usiwe mnafiki Kwa kuacha kuzinukuu kauli za wanaukawa waliomnanga lowasa kisha wakamsafisha akawa mgombea wao....
Japo wapo mazwazwa wanachezeshwa ngoma zenu ila wenye akili timamu na upeo huru wa kuchanganua mambo hatokaa awape nafasi ya uaminifu tena, ninyi nyote wanasiasa wabinafsi na wanafiki Kwa kiwango kisichoelezeka.
Na hizi siasa zenu za kuchafuana na kukomalia hoja chafuzi hata kama mnajuwa ni uwongo mtupu kuna siku watanzania watazinduka mtawaelewa tu endeleeni kuwatumia mkiwachezesha ngoma zenu haramu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Facts mkuu.

Umeongea facts tupu mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka kauli ya Kikwete kutaka kulivua gamba. Kulivua gamba ilikuwa ni kuwafukuza ccm mafisadi waliokuwa wanakichafua chama wakiwemo Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo. Nape hajawahi kutukanwa ndani ya ccm kama alivyotukanwa fisadi lowassa. Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.
Ogopa sana wanasiasa, na kama watu wanakufa na kwenda mbinguni, kamwe mwanasiasa hawezi kuionja pepo, lazima waingie Jehanam, nakumbuka kule Kenya watu walikufa kwa sbu ya akina Odinga, leo hii wako sahani moja na Kenyatta, huki kwetu watu waliumizwa, hadi wengine wakawa wanadeki mabara bara kwa imani yao kutoka moyoni, leo hii amewakimbia, ni maumivu makubwa amewaachia, ndo maana nasema mwanasiasa hawezi enda mbinguni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Mzee sitaki hata kusikia jina lake walahi vile, nakumbuka nlivyotoroka kazini siku ile ya Kampeni akiwa Arusha, nkaponea chupuchupu kupumzishwa na barua ya warning na Kanjbhai wangu, nakumbuka tulivyopigwa na jua ile siku, nakumbuka usafiri wa kurudi nyumbani ulivyotutesa kama haitoshi siku ua kupiga kura tulivyoamka asubuhi asubhi nkapiga magoti kumuombea, walah napata hasira isiyo kifani
Ndio siasa mkuu.

Ukiegemea na kuwasikiliza wanasiasa utakufa siku si zako kwa pressure,usipoangalia wanatutumia kama daraja kufanikiwa yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu BAK, kusema ukweli kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu, na wala sio kwamba najipendekeza kwako:
NI WEWE TU, PEKE YAKO HAPA JF AMBAYE HUKUWAHI KUMSHOBOKEA LOWASA
kama kuna kuna mtu anayebisha alete hapa comment yako hata moja tu ambayo itanikanusha. Tangu mwanzo hukuwa na mahaba na EDO.
Wewe sio kigeugeu kama wengine akina fulani......
mnyonge myongeni haki yake mpeni, kwa hili hata mi ntamtetea Bak

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom