Nape: Kuhama vyama kunawaumiza wananchi, inabidi tubadili sheria

HAKUNA KUHAMA NA UONGOZI, LAZIMA AJIUZURU NA ALIYEMFUATIA KWA KURA kipindi cha uchaguzi ndio achukue uongozi/ubunge. Msituletee sanaa hapa.
 
Nape sio wa kubezwa kujiamini kulikopitiliza kunatia shaka,huenda anajua nini kilifanyika uchaguzi 2015,kwa lugha nyepesi tunaweza sema bila yeye pasingekuepo na Jiwe.
 
U

Umesema kitu kikubwa sana sana mbunge anaomba kura kwa kupitia chama inamaana chama hicho kinachukua eneo husika kwa muda wamiaka 5 sasa ikitokea mbunge au mwenyecheo chochote cha kuchaguliwa kufa kuacha au kuhama chama kilicho shika nafasi hiyo kitoe MTU mwingine kutoka kwao aongoze na ikitokea wachaguliwa hao kupishana naviongozi wao wa vyama vyao yule yule alio shinda au kuteuliwa aulizwe kwenye vyombo vya habari kama anaendelea nakazi au la iwapo atasema anapiga mzigo chama kisiwe na uwezo wa kukatisha uongozi wake nakama atasema ameshindwa ndio atafutwe mtu mwingine kutoka chama chake kumuondoa mtu kwasababu ya kichama nikukatisha mategemeo kwawananchi na chama walicho kichagua nisawa na kukatisha uhai wao
Kutumia pesa kurudiwa uchaguzi kwa hawa waliouza nafasi na kuzihitaji tena kunatuumiza wananchi mfano sikumoja nilikwenda kumtembelea jamaa yangu kilimahewa kgm nikamuona polepole wanamuonesha njia inayotuwa na walim wanafunzi na wazazi kwenda s/yamsingi kilima hewa kunakorongo kubwa hata ubakaji unaweza kutokea linatisha gharama yake haifanani na uchaguzi hata wadiwani mmoja gharama ni m5 tu wananchi wamechanga m2 bado 3 wanashindwa kuwachangia wako bize na uchaguzi na kununua wachaguliwa wa upinzani hivi hawawananchi watawapenda kweli?
Nakubaliana asilimia 100 na hoja yako,huu ndio ufumbuzi ,kama mtu anaunga mkono,chama chake kiteue mtu wa kushika nafasi hiyo hadi muda wa uchaguzi mwingine utakapofika, ili analopendekeza Nape ni bullshit,mfano mbunge katoka chama X na kwenda chama Y na ubunge wake,then baada ya muda anakuwa bored chama Y na kurudi chama Xna ubunge wake,anakaa chama x mwaka anashindwa kuelewana na mwenyekiti anahamua kwenda chama Z na ubunge wake etc etc,Ifikie wakati haya mambo yawekewe breki kuwa mtu akihama chama kilichotumia resources zake kumfanyia kampeni hadi akawa kiongozi basi akiunga mkono hoja uwe ndio mweisho wa uongozi huo na hiyo nafasi apewe mwingine katika chama hichohicho,kule alikoenda kuungia mkono juhudi basi wampe nafasi nyingine kama ni diwani apewe utendaji wa kata na kama mbunge apewe U-Dc AU u- DED au U-DAS.Ifikie wakati tue srious na haya mambo yanayolipotezea taifa muda na fedha nyingi za walipa kodi,badala ya kujenga viwanda tutakuwa kwenye kampeni kila mwaka January hadi December. Japo kwa upande mwingine hizi kampeni ni advantage kwa vyama ambavyo vimezuiwa kufanya mikutano, wanapata muda muafaka wa kujitangaza,nimefanya utafiti kdogo na kugundua vyama vya aina hii vina kuwa popular na kupata mashabiki zaidi kila eneo uchaguzi mdogo ukimalizika kuliko ilivyokuwa kabla ya uchaguzi,hizi chaguzi ndogo ni hamsha hamsha inayowapa advantage vyama vya upinzani towards 2020, anayedhani kuchukua wabunge na madiwani kunadhoofisha vyama aende Buyungu au maeneo ulikoisha uchaguzi huu wa juzi na majibu atayapata na kugundua ni kiasi gani inafanyika political blunder katika kununua wabunge na wapinzani.
 
Nape hakubaliani na hawa wahamiaji kuja kula tu kivulini wakati wa kilimo hawakushiriki.
 
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema wabunge kuhama hama kuna ukakasi kwa kuwa haliwapi nafasi wananchi ambao waliwapigia kura

Nape amesema kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kubadili sheria ili wanaoham,a wahame na ubunge wao

Pia amesema ni ngumu kuamini sababu zinazotolewa na wanaohama (kumuunga mkono Magufuli}

The reason for changing parties is clear,wameona upinzani haulipi,ndio maana wanakacha.They are looking for greener pastures. Ni wachumia tumbo tu hao.

Bado ninapata shida kuelewa kwa nini tunapokea wasaliti na wachumia tumbo hao kama CCM,for whatever reasons.Siungi kabisa mkono mawazo ya Nape kwa kuwa sioni jinsi mbunge anavyoweza kuhamia chama kingine na ubunge wake.Kwanza huko ni kuhalalisha usaliti! Mimi nadhani ni wakati muafake sasa wa kuwatendea haki wananchi wetu.Tuache kufuga usaliti kwa kutunga sheria ngumu, ili mbunge akikacha ubunge chama kimoja bila sababu za "msingi" awe barred from politics for life. Hii itawafanya watulie kwenye vyama vyao na kuwatumia wananchi in whatever circumstances.
 
Rais Magufuli ametusaidia sana kujua tabia za watu.

Alianza na Polepole aliyeshupaza shingo akisema cheo cha ukuu wa wilaya hakina maana,alipewa,akapokea,akala na akakaa kimya!

Akasema tena uchaguzi ukiwa huru na haki CCM haina chake, akapewa cheo CCM,akapokea,anakula na anatamani kufuta kauli yake.

Tumeona kwa msomi Prof Kabudi
Tumeona kwa Dr Bashiru
Tunaona kwa kina Mtatiro na wenzake.

Tunaendelea kuona kwa Nape jinsi wanasiasa walivyo wanafiki
 
Mtu ajiuzulu kwa kuwa mahututi kitandani ili kupisha walio wazima kugombea
 
Mara nyingi huwa simuekewi Nape na ninapomuelewa nabaki sana na alama mbili ! Na ?. Anyway, kanena na ni sawa japo mie nlifikiria mbunge anaejivua ubunge,sheria irekebishwe ili sasa kwa vile alichaguliwa na wananchi aitishe mikutano ya hadhara kama wakati wa kampeni awaambie wananchi waliompa kura kuwa anaachia hiyo nafasi kwa sababu ambazo atakuwa nazo na hiyo mikutano iwe kwa gharama zake,pia asiruhusiwe kugombea nafasi kama hiyo japo miaka mitano. Ili tupunguze huu upuuzi.
 
Siasa za kwetu ni kigeugeu.
Miaka ijayo utasikia walaka mwingine,kutokea watu wale wale wanaunga uhamiaji haramu kwa sasa.
Ukimuuliza Nape kwanini asiyazungumze ndani ya vikao vya chama mapema ili kuacha upuuzi huo?Na kwanini kikao cha juzi walishia kuunga hatua za wahamiaji haramu kukimbia vyama vyao vya halisi?
 
Huyu jamaa ameshawafanya wabongo wote wajinga!ni yeye aliyeshiriki bao la mkono Buyungu na leo anajifanya mtakatifu!ukiona anasema hivi ujue anapima upepo au wamemaliza watu wa kuwanunua wanatufanya mazombie
Muda wa kununua unaelekea mwisho. Bado kidogo ibaki miezi 24 ya kisheria.
 
Nakubaliana asilimia 100 na hoja yako,huu ndio ufumbuzi ,kama mtu anaunga mkono,chama chake kiteue mtu wa kushika nafasi hiyo hadi muda wa uchaguzi mwingine utakapofika, ili analopendekeza Nape ni bullshit,mfano mbunge katoka chama X na kwenda chama Y na ubunge wake,then baada ya muda anakuwa bored chama Y na kurudi chama Xna ubunge wake,anakaa chama x mwaka anashindwa kuelewana na mwenyekiti anahamua kwenda chama Z na ubunge wake etc etc,Ifikie wakati haya mambo yawekewe breki kuwa mtu akihama chama kilichotumia resources zake kumfanyia kampeni hadi akawa kiongozi basi akiunga mkono hoja uwe ndio mweisho wa uongozi huo na hiyo nafasi apewe mwingine katika chama hichohicho,kule alikoenda kuungia mkono juhudi basi wampe nafasi nyingine kama ni diwani apewe utendaji wa kata na kama mbunge apewe U-Dc AU u- DED au U-DAS.Ifikie wakati tue srious na haya mambo yanayolipotezea taifa muda na fedha nyingi za walipa kodi,badala ya kujenga viwanda tutakuwa kwenye kampeni kila mwaka January hadi December. Japo kwa upande mwingine hizi kampeni ni advantage kwa vyama ambavyo vimezuiwa kufanya mikutano, wanapata muda muafaka wa kujitangaza,nimefanya utafiti kdogo na kugundua vyama vya aina hii vina kuwa popular na kupata mashabiki zaidi kila eneo uchaguzi mdogo ukimalizika kuliko ilivyokuwa kabla ya uchaguzi,hizi chaguzi ndogo ni hamsha hamsha inayowapa advantage vyama vya upinzani towards 2020, anayedhani kuchukua wabunge na madiwani kunadhoofisha vyama aende Buyungu au maeneo ulikoisha uchaguzi huu wa juzi na majibu atayapata na kugundua ni kiasi gani inafanyika political blunder katika kununua wabunge na wapinzani.
Nakubaliana nawewe hata Mimi wapeane nafasi za uteuzi tu.tukisha piga kura iwe imetoka mpaka uchaguzi ujao baada ya miaka 5 ndio uchaguzi tena angalia kama hivi alivyosema magu siasa hadi uchaguzi mwingine ujao alafu unanunua watu alafu tunafanya uchaguzi nahauweki kura za maoni hii unaonesha wazi kuwa kumbe kunabiashara inafanyika hasara kwa sisi wananchi ccm kama kweli hakuna dili iache kuwapokea wachaguliwa kwa maslahi mapana yanchi kama wanatuhurumia wananchi kurudia uchaguzi nigharama kweli wafanyekitu nakukataa kitu kwa maslahi mapana ya nchi
 
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema wabunge kuhama hama kuna ukakasi kwa kuwa haliwapi nafasi wananchi ambao waliwapigia kura

Nape amesema kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kubadili sheria ili wanaoham,a wahame na ubunge wao

Pia amesema ni ngumu kuamini sababu zinazotolewa na wanaohama (kumuunga mkono Magufuli}

2020...wahamiaji wote inakula kwao .....wamepewa nafasi kwa muda mfupi tu....wenye chama chao ndio watafanya maamuzi ya nani awe mgombea kutokana na kukitetea chama kwa nguvu zao zote.... na sio vibaraka wa kuja ....
 
..anayehama ahame na nafasi yake.

..anayejiuzulu, aliyefariki, au aliyekosa sifa[kufungwa, etc] chama kiteue wa kuziba pengo aliloacha.
 
Huyu jamaa ameshawafanya wabongo wote wajinga!ni yeye aliyeshiriki bao la mkono Buyungu na leo anajifanya mtakatifu!ukiona anasema hivi ujue anapima upepo au wamemaliza watu wa kuwanunua wanatufanya mazombie
...na wajinga watampongeza
 
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema wabunge kuhama hama kuna ukakasi kwa kuwa haliwapi nafasi wananchi ambao waliwapigia kura

Nape amesema kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kubadili sheria ili wanaoham,a wahame na ubunge wao

Pia amesema ni ngumu kuamini sababu zinazotolewa na wanaohama (kumuunga mkono Magufuli}

huyu naye hajulikani mawio wala machweo
 
Back
Top Bottom